Loi sur le divorce 1 Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.
Matthieu 19.7-19.9 Jérémie 3.8 Deutéronome 22.19 Deutéronome 22.13 Exode 21.10 2 Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine.
Ezéchiel 44.22 Nombres 30.9 Lévitique 22.13 Lévitique 21.7 Lévitique 21.14 3 Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe;
4 yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za Bwana; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi.
Jérémie 3.1 Lévitique 18.24-18.28 Josué 22.17-22.18 Ordonnances diverses 5 Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yo yote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.
Deutéronome 20.7 Proverbes 5.18 Genèse 2.24 1 Corinthiens 7.29 Ecclésiaste 9.9 6 Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani.
Deutéronome 20.19 Luc 12.15 Genèse 44.30 Exode 22.26-22.27 Apocalypse 18.22 7 Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwivi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
Exode 21.16 1 Timothée 1.10 Deutéronome 19.19 Exode 22.1-22.4 Apocalypse 18.13 8 Angalia katika pigo la ukoma, utunze kwa bidii, kwa kufanya mfano wa yote watakayowafundisha makuhani Walawi; tunzeni kwa kuyafanya vile vile kama nilivyowaamuru wao.
Lévitique 14.2 Matthieu 8.4 Luc 5.14 Marc 1.44 Lévitique 13.57 9 Kumbukeni na Bwana, Mungu wako alivyomtenda Miriamu katika njia mlipotoka Misri.
Nombres 12.10-12.15 Luc 17.32 Nombres 5.2 2 Rois 7.3 1 Corinthiens 10.11 10 Umkopeshapo jirani yako cho chote kikopeshwacho usiingie katika nyumba yake kwenda kutwaa rehani kwake.
Deutéronome 15.8 Exode 22.27 11 Simama nje, yule umkopeshaye akuletee nje ile rehani.
12 Naye akiwa ni mtu maskini, usilale na rehani yake.
Deutéronome 24.17 Job 24.9 Job 22.6 Job 24.3 13 Sharti umrudishie rehani lichwapo jua, apate kulala na mavazi yake, na kukubarikia; nayo itakuwa ni haki kwako mbele za Bwana, Mungu wako.
Deutéronome 6.25 Daniel 4.27 Psaumes 112.9 Deutéronome 24.15 Exode 22.26-22.27 14 Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako;
Malachie 3.5 Proverbes 14.31 Amos 4.1 Deutéronome 15.12-15.18 Amos 2.7 15 mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako.
Jacques 5.4 Lévitique 19.13 Deutéronome 15.9 Jérémie 22.13 Proverbes 3.27-3.28 16 Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.
Ezéchiel 18.20 Jérémie 31.29-31.30 2 Chroniques 25.4 2 Rois 14.5-14.6 17 Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;
Deutéronome 16.19 Exode 23.6 Exode 22.21-22.22 Deutéronome 27.19 Job 29.11-29.17 18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.
Deutéronome 5.15 Deutéronome 15.15 Deutéronome 16.12 Deutéronome 24.22 Solidarité avec les plus démunis 19 Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili Bwana, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.
Lévitique 23.22 Lévitique 19.9-19.10 Deutéronome 14.29 Proverbes 19.17 Esaïe 58.7-58.11 20 Utakapochuma matunda ya mizeituni yako, usirudi kuchuma mara ya pili; yaliyobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane.
Lévitique 19.10 21 Uchumapo zabibu katika shamba lako la mizabibu, usichume mara ya pili; zilizobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane.
Lévitique 19.9-19.10 Deutéronome 24.19 22 Nawe kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.
Deutéronome 24.18 Ephésiens 5.1-5.2 Deutéronome 5.14-5.15 1 Jean 4.10-4.11 Deutéronome 7.8