Mort et ensevelissement de Sara
1 Basi umri wake Sara ulikuwa miaka mia na ishirini na saba ndio umri wake Sara.
Genèse 17.17
2 Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Ibrahimu akaja kumlilia Sara na kumwombolezea.
Genèse 23.19 Juges 1.10 Genèse 13.18 Jean 11.31 2 Chroniques 35.25
3 Akaondoka Ibrahimu kutoka mbele ya maiti wake, akasema na wazawa wa Hethi, akinena,
Genèse 10.15 2 Samuel 23.39 Genèse 27.46 Genèse 23.7 Genèse 23.5
4 Mimi ni mgeni, ninatembea kwenu; nipeni mahali pa kuzikia kwenu, pawe pangu, nimzike maiti wangu atoke mbele yangu.
1 Chroniques 29.15 Genèse 17.8 Hébreux 11.9 Actes 7.5 Lévitique 25.23
5 Wazawa wa Hethi wakamjibu Ibrahimu, wakamwambia,
6 Utusikie, Ee bwana, ndiwe mtu mkuu sana kwetu, uzike maiti wako katika kaburi lile utakalochagua katika makaburi yetu. Hapana mtu kwetu atakayekuzuilia kaburi lake, usizike maiti wako.
Genèse 24.35 Genèse 14.14 1 Jean 3.1-3.2 Genèse 24.18 Esaïe 45.14
7 Ibrahimu akaondoka, akainama mbele ya watu wa nchi, mbele ya hao wazawa wa Hethi.
Romains 12.17-12.18 1 Pierre 3.8 Proverbes 18.24 Hébreux 12.14 Genèse 19.1
8 Naye akazungumza nao, akisema, Ikiwa nia yenu nimzike maiti wangu atoke mbele yangu, mnisikie, mkaniombee kwa Efroni bin Sohari,
1 Rois 2.17 Luc 7.3-7.4 Genèse 25.9 Hébreux 7.26 1 Jean 2.1-2.2
9 ili kwamba anipe pango ya Makpela, iliyo katika mpaka wa shamba lake, na anipe kwa kima kilicho kamili, katikati yenu, iwe milki yangu ya kuzikia.
Romains 12.17 Romains 13.8
10 Basi Efroni alikuwa akiketi kati ya wazawa wa Hethi. Efroni Mhiti akamjibu Ibrahimu, na wazawa wa Hethi wanasikiliza, hata watu wote waingiao mlango wa mji wake, akisema,
Genèse 34.24 Genèse 34.20 Genèse 23.18 Job 29.7 Matthieu 9.1
11 Sivyo, bwana wangu, unisikilize. Lile shamba nakupa, na pango iliyomo nakupa; mbele ya wana wa watu wangu nakupa, uzike maiti wako.
Nombres 35.30 Jérémie 32.7-32.12 Ruth 4.1 Ruth 4.11 Genèse 23.6
12 Ibrahimu akainama mbele ya watu wa nchi.
Genèse 23.7 Genèse 18.2 Genèse 19.1
13 Akamwambia Efroni, na watu wa nchi wanasikiliza, akisema, Tafadhali unisikilize; nitatoa kima cha shamba, nawe ukipokee kwangu, nami nitamzika humo maiti wangu.
Genèse 14.22-14.23 Hébreux 13.5 Actes 20.35 Colossiens 4.5 Philippiens 4.5-4.8
14 Efroni akamjibu Ibrahimu, akamwambia,
15 Bwana wangu, unisikilize. Sehemu ya nchi, ambayo thamani yake ni shekeli za fedha mia nne, n’nini hii baina yako na yangu? Basi uzike maiti wako.
Ezéchiel 45.12 Exode 30.15 Exode 30.13
16 Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara.
Zacharie 11.12 Jérémie 32.9 1 Thessaloniciens 4.6 Genèse 23.15 Exode 30.13
17 Basi shamba la Efroni lililokuwa katika Makpela kuelekea Mamre, shamba, na pango iliyokuwamo, na miti yote iliyokuwamo shambani, iliyokuwa katika mipaka yake pande zote, vyote viliyakinishwa
Genèse 25.9 Genèse 50.13 Genèse 23.20 Actes 7.16 Ephésiens 5.15
18 kuwa mali yake Ibrahimu, mbele ya wazawa wa Hethi, mbele ya watu wote waingiao katika mlango wa mji wake.
Genèse 34.20 Jérémie 32.12 Ruth 4.1
19 Basi baada ya hayo Ibrahimu akamzika Sara mkewe katika pango ya shamba la Makpela kuelekea Mamre, ndiyo Hebroni, katika nchi ya Kanaani.Genèse 50.25 Ecclésiaste 12.7 Genèse 50.13 Genèse 47.30 Genèse 49.29-49.32
20 Na lile shamba, na pango iliyomo, iliyakinishwa kuwa mali yake Ibrahimu na wazawa wa Hethi, kuwa mahali pa kuzikia.
Ruth 4.7-4.10 2 Samuel 24.24 Genèse 49.31-49.32 Genèse 25.9 2 Rois 21.18