Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Esdras 6 Bible en Swahili de l’est
Édit de Darius
1 Ndipo mfalme Dario akatoa amri, na watu wakatafuta katika nyumba ya vyuo vya tarehe, hapo akiba zilipowekwa katika Babeli. Esdras 5.17 Esdras 4.15 Jérémie 36.2-36.4 Ezéchiel 2.9 Jérémie 36.32 2 Na chuo kimoja kilipatikana huko Akmetha, katika nyumba ya mfalme iliyo katika wilaya ya Umedi, na ndani yake maneno haya yameandikwa ili yakumbukwe. 2 Rois 17.6 3 Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi, mfalme Koreshi alitoa amri, Kwa habari ya nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, nyumba hiyo na ijengwe, mahali watoapo dhabihu, na misingi yake ipigwe na kufanywa imara sana; kuinuka kwake kuwe mikono sitini, na upana wake mikono sitini; 1 Rois 6.2-6.3 2 Chroniques 36.22-1.4 Esdras 5.13-5.15 Apocalypse 21.16 Deutéronome 12.5-12.6 4 ziwepo safu tatu za mawe makubwa, na safu moja ya miti mipya; gharama zake zitolewe katika nyumba ya mfalme. 1 Rois 6.36 Psaumes 72.10 Esdras 7.20-7.23 Esaïe 49.23 Psaumes 68.29 5 Na vyombo vya dhahabu na fedha, vya nyumba ya Mungu, ambavyo mfalme Nebukadreza alivitoa katika nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu, akavileta mpaka Babeli, na virudishwe, vikaingizwe tena katika hekalu lililoko Yerusalemu, kila kimoja mahali pake, na wewe uvitie katika nyumba ya Mungu. Esdras 5.14 Daniel 5.2 2 Chroniques 36.6-36.7 Jérémie 27.16 2 Rois 24.13 6 Basi sasa ninyi, Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na hao wenzi wenu wa Kiajemi, mlio ng’ambo ya Mto, jitengeni na mahali pale; Esdras 5.3 Esdras 5.6 Psaumes 76.10 Proverbes 21.1 Actes 4.26-4.28 7 iacheni kazi hii ya nyumba ya Mungu, msiizuie; waacheni liwali wa Wayahudi, na wazee wa Wayahudi, waijenge nyumba hii ya Mungu mahali pake. Actes 5.38-5.39 8 Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi, kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ng’ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe. Esdras 6.4 Esdras 7.15-7.22 Esdras 4.20-4.21 Aggée 2.8 Esdras 5.5 9 Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng’ombe wachanga, na kondoo waume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa; Lévitique 1.10 Esaïe 49.23 Lévitique 2.1-2.16 Psaumes 50.9-50.13 Marc 9.49 10 wapate kumtolea Mungu wa mbinguni sadaka zenye harufu nzuri, na kumwombea mfalme, na wanawe, wapate uzima. Jérémie 29.7 1 Timothée 2.1-2.2 Esdras 7.23 Ephésiens 5.2 Lévitique 1.13 11 Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili. Daniel 2.5 Daniel 3.29 Esdras 7.26 2 Rois 10.27 Esther 5.4 12 Na Mungu huyu, aliyelifanya jina lake likae pale, na aangamize wafalme wote, na watu wote, watakaonyosha mikono yao kulibadili neno hili, na kuiharibu nyumba hii ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. Mimi, Dario, nimetoa amri; na ifanyike kwa bidii nyingi. 1 Rois 9.3 Deutéronome 12.5 Deutéronome 12.11 Exode 20.24 Esther 3.14-3.15