5 Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga. Esdras 5.17 2 Samuel 14.22 Esther 1.19 Proverbes 3.4 Esther 7.3 6 Mfalme akaniuliza, (malkia naye ameketi karibu naye), Safari yako itakuwa ya siku ngapi? Nawe utarudi lini? Hivyo mfalme akaona vema kunipeleka; nami nikampa muda. Néhémie 13.6 Néhémie 5.14 Néhémie 2.4 Esaïe 65.24 Esaïe 58.12 7 Tena nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa maliwali walio ng’ambo ya Mto, ili waniache kupita mpaka nifike Yuda; Esdras 7.21 Esdras 8.36 Esdras 6.6 Néhémie 2.9 Esdras 8.22 8 nipewe na waraka kwa Asafu, mwenye kuutunza mwitu wa mfalme, ili anipe miti ya kufanyizia boriti kwa malango ya ngome ya nyumba, na kwa ukuta wa mji; na kwa nyumba ile nitakayoingia mimi. Naye mfalme akanipa, kama mkono mwema wa Mungu wangu ulivyokuwa juu yangu. Esdras 7.6 Néhémie 7.2 Esdras 5.5 Daniel 1.9 Esaïe 66.14 9 Ndipo nikafika kwa maliwali walio ng’ambo ya Mto, nikawapa hizo nyaraka za mfalme. Naye mfalme alikuwa amepeleka maakida wa jeshi lake na wapanda farasi pamoja nami. Esdras 8.22 10 Hata Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, waliposikia habari hizi, ziliwahuzunisha sana, kwa kuwa amekuja mtu kuwatakia heri wana wa Israeli. Néhémie 2.19 Néhémie 4.7 Néhémie 6.1 Actes 19.26-19.27 Néhémie 4.1-4.3 11 Basi nikafika Yerusalemu, nikakaa huko muda wa siku tatu. Esdras 8.32 12 Kisha nikaondoka usiku, mimi na watu wachache pamoja nami; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe. Esdras 7.27 Apocalypse 17.17 Juges 6.27 Jérémie 31.33 Jérémie 32.40 13 Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto. Néhémie 1.3 2 Chroniques 26.9 Néhémie 2.17 Néhémie 2.3 Néhémie 12.31 14 Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; lakini hapakuwa na nafasi ya kupita kwa yule mnyama aliyekuwa chini yangu. Néhémie 3.15 2 Rois 20.20 2 Rois 18.17 2 Chroniques 32.30 15 Kisha nikapanda usiku kando ya kijito, nikautazama ukuta; kisha nikarudi nyuma, nikaingia kwa lango la bondeni, nikarejea hivyo. 2 Samuel 15.23 Jérémie 31.38-31.40 Jean 18.1 16 Wala mashehe hawakujua nilikokwenda, wala nilivyotenda; wala sijawaambia Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala mashehe, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo. 17 Kisha nikawaambia, Mnaona hali hii dhaifu tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa, na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto; haya! Na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe shutumu tena. Néhémie 1.3 Ezéchiel 5.14 Lamentations 3.45-3.46 Jérémie 24.9 Psaumes 44.13 18 Nikawaeleza habari ya mkono wa Mungu wangu ulivyokuwa mwema juu yangu; pia na maneno ya mfalme aliyoniambia. Nao wakasema, Haya! Na tuondoke tukajenge. Basi wakaitia mikono yao nguvu kwa kazi hiyo njema. 2 Samuel 2.7 1 Chroniques 11.10 2 Chroniques 32.5 Aggée 1.13-1.14 Ephésiens 6.10 19 Lakini waliposikia Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Mtaasi ninyi juu ya mfalme? Néhémie 6.6 Psaumes 44.13-44.14 Néhémie 6.1-6.2 Hébreux 11.36 Jean 19.12 20 Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu. Esdras 4.3 Néhémie 2.4 Actes 8.21 Ecclésiaste 7.18 Psaumes 20.5