Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 17.1
Bible en Swahili de l’est


1 Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma, Kaburi i tayari kunipokea.Psaumes 88.3-88.5 Esaïe 38.10-38.14 Job 42.16 Job 6.11 Job 17.13-17.14
2 Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka, Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao.1 Samuel 1.6-1.7 Job 16.20 Job 12.4 Psaumes 35.14-35.16 Job 13.9
3 Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe; Kuna nani atakayeniwekea dhamana?Proverbes 11.15 Psaumes 119.122 Esaïe 38.14 Hébreux 7.22 Proverbes 20.16
4 Kwani mioyo yao imeificha ufahamu; Kwa hiyo hutawakuza.Romains 11.8 2 Samuel 15.31 Matthieu 11.25 1 Corinthiens 1.20 Esaïe 19.14
5 Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo, Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.Job 11.20 Job 32.21-32.22 1 Rois 11.12 Proverbes 20.19 Proverbes 29.5
6 Amenifanya niwe simo kwa watu; Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.Job 30.9 Psaumes 44.14 Genèse 31.27 Esaïe 5.12 1 Rois 9.7
7 Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.Job 16.16 Psaumes 6.7 Psaumes 31.9-31.10 Psaumes 109.23 Job 16.8
8 Walekevu watayastaajabia hayo, Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu.Habakuk 1.13 Actes 13.46 Psaumes 73.12-73.15 Job 22.19 Job 34.30
9 Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.Proverbes 4.18 Job 22.30 1 Jean 2.19 Psaumes 73.13 Esaïe 35.8-35.10
10 Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa; Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu.Job 42.7 Job 6.29 1 Corinthiens 1.20 Job 15.9 Job 17.4
11 Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika, Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu.Job 7.6 Ecclésiaste 9.10 Proverbes 19.21 Lamentations 3.37 Jacques 4.13-4.15
12 Wabadili usiku kuwa mchana; Wasema, Mwanga u karibu kwa sababu ya giza.Job 7.13-7.14 Job 7.3-7.4 Job 24.14-24.16 Deutéronome 28.67
13 Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu; Nikitandika malazi yangu gizani;Job 14.14 Job 30.23 Job 17.1 Psaumes 139.8 Psaumes 27.14
14 Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu; Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na umbu langu;Psaumes 16.10 1 Corinthiens 15.53-15.54 Job 24.20 Psaumes 49.9 Actes 2.27-2.31
15 Basi, tumaini langu li wapi? Na tumaini langu, ni nani atakayeliona?Job 13.15 Job 19.10 Job 7.6 Job 6.11 Job 4.6
16 Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu, Itakapokuwapo raha mavumbini.Job 3.17-3.19 Jonas 2.6 Psaumes 143.7 Job 33.18-33.28 Job 18.13-18.14

Cette Bible est dans le domaine public.