Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 7
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe, Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye. Psaumes 31.15 Habakuk 3.1 Psaumes 3.7 1 Pierre 4.19 Psaumes 43.4
2 Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya. Psaumes 50.22 Esaïe 38.13 Psaumes 17.12 Job 10.7 Osée 13.7-13.8
3 Bwana, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu, 1 Samuel 24.11 Psaumes 59.3 2 Samuel 16.7-16.8 Job 11.14 Psaumes 66.18
4 Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;) 1 Samuel 24.7 Psaumes 109.5 Psaumes 55.20 1 Samuel 26.24 Genèse 44.4
5 Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini. Esaïe 63.3 Psaumes 60.12 Job 31.5-31.10 Job 40.12-40.13 Job 16.15
6 Bwana uondoke kwa hasira yako; Ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu. Psaumes 44.23 Psaumes 35.23 Psaumes 3.7 Esaïe 33.10 Psaumes 78.65
7 Kusanyiko la mataifa na likuzunguke, Na juu yake uketi utawale. Psaumes 58.10-58.11 Psaumes 138.6 Psaumes 48.11 Psaumes 93.4 Esaïe 57.15
8 Bwana atawaamua mataifa, Bwana, unihukumu mimi, Kwa kadiri ya haki yangu, Sawasawa na unyofu nilio nao. Psaumes 96.13 Romains 14.10-14.12 Psaumes 98.9 2 Corinthiens 1.12 Psaumes 43.1
9 Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na viuno Ndiye Mungu aliye mwenye haki. Apocalypse 2.23 Jérémie 11.20 Psaumes 37.23 1 Chroniques 28.9 Jérémie 20.12
10 Ngao yangu ina Mungu, Awaokoaye wanyofu wa moyo. Psaumes 125.4 Psaumes 18.1-18.2 Genèse 15.1 Psaumes 112.2 Job 8.6
11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku. Nahum 1.2 Psaumes 94.15 Nahum 1.6 Psaumes 50.6 Psaumes 7.8
12 Mtu asiporejea ataunoa upanga wake; Ameupinda uta wake na kuuweka tayari; Deutéronome 32.41 Psaumes 85.4 Actes 3.19 Ezéchiel 21.23 Matthieu 3.10
13 Naye amemtengenezea silaha za kufisha, Akifanya mishale yake kuwa ya moto. Psaumes 45.5 Deutéronome 32.23 Lamentations 3.12-3.13 Psaumes 11.2 Deutéronome 32.42
14 Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo. Jacques 1.15 Job 15.35 Esaïe 33.11 Esaïe 59.4-59.5 Job 15.20
15 Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoifanya! Job 4.8 Psaumes 119.85 Psaumes 141.10 Proverbes 26.27 Psaumes 35.7-35.8
16 Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini. Esther 9.25 1 Rois 2.32 Psaumes 36.4 Psaumes 36.12 1 Samuel 26.10
17 Nitamshukuru Bwana kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu. Psaumes 9.2 Psaumes 71.15-71.16 Daniel 4.17 Daniel 4.25 Daniel 4.34

Cette Bible est dans le domaine public.