Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 11.12
Bible en Swahili de l’est


1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.Esaïe 53.2 Esaïe 11.10 Jérémie 23.5 Apocalypse 22.16 Zacharie 6.12
2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;Esaïe 61.1 Jean 16.13 Esaïe 42.1 Matthieu 3.16 2 Timothée 1.7
3 na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;Jean 7.24 1 Corinthiens 2.13-2.15 Luc 2.52 Esaïe 33.6 Hébreux 5.14
4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.Job 4.9 Malachie 4.6 Esaïe 61.1 2 Thessaloniciens 2.8 Psaumes 2.9
5 Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.Ephésiens 6.14 Esaïe 25.1 Osée 2.20 Apocalypse 3.14 Esaïe 59.17
6 Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.Esaïe 65.25 Osée 2.18 Galates 3.26-3.27 Apocalypse 5.9-5.10 Romains 14.17
7 Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. 8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.Esaïe 59.5 Psaumes 140.3
9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari.Habakuk 2.14 Job 5.23 Psaumes 98.2-98.3 Esaïe 52.10 Psaumes 72.19
10 Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.Romains 15.9-15.12 Jean 12.32 Esaïe 11.1 Luc 2.32 Actes 11.18
11 Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.Genèse 10.22 Michée 7.12 Esaïe 66.19 Esaïe 42.4 Jérémie 25.25
12 Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia.Sophonie 3.10 Esaïe 11.10 Esaïe 56.8 Psaumes 147.2 Esaïe 43.6
13 Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamhusudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu.Jérémie 3.18 Osée 1.11 Ezéchiel 37.16-37.24 Esaïe 7.1-7.6 Esaïe 9.21
14 Nao watashuka, watalirukia bega la Wafilisti upande wa magharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni watawatii.Esaïe 25.10 Joël 3.19 Jérémie 49.28 Daniel 11.41 Amos 9.12
15 Na Bwana atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake uteketezao atatikisa mkono wake juu ya Mto, naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu wenye viatu vikavu.Esaïe 50.2 Esaïe 19.16 Zacharie 10.11 Esaïe 7.20 Ezéchiel 30.12
16 Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.Esaïe 19.23 Exode 14.26-14.29 Esaïe 11.11 Esaïe 35.8-35.10 Esaïe 40.3-40.4

Cette Bible est dans le domaine public.