Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 26.5
Bible en Swahili de l’est


1 Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.Esaïe 60.18 Esaïe 27.1-27.2 Psaumes 48.12 Esaïe 25.9 Jérémie 33.11
2 Wekeni wazi malango yake, Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.Esaïe 60.11 Esaïe 54.14 Esaïe 62.2 Psaumes 118.20 Apocalypse 21.24
3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.Philippiens 4.7 Jean 14.27 Jean 16.33 Psaumes 9.10 Romains 4.18-4.21
4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.Esaïe 12.2 Esaïe 50.10 Psaumes 62.8 Philippiens 4.13 Psaumes 55.22
5 Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, Mji ule ulioinuka, aushusha, Aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini.Job 40.11-40.13 Esaïe 25.11-25.12 Esaïe 32.19 Esaïe 47.1 Jérémie 51.25-51.26
6 Mguu utaukanyaga chini, Naam, miguu yao walio maskini, Na hatua zao walio wahitaji.Apocalypse 2.26 Esaïe 3.15 Josué 10.24 Romains 16.20 Luc 1.51-1.53
7 Njia yake mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.1 Samuel 2.2-2.4 1 Jean 3.10 2 Corinthiens 1.12 Esaïe 35.8 1 Chroniques 29.17
8 Naam, katika njia ya hukumu zako Sisi tumekungoja, Ee Bwana; Shauku ya nafsi zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako.Exode 3.15 Psaumes 44.17-44.18 Esaïe 25.9 Nombres 36.13 Esaïe 56.1
9 Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.Matthieu 6.33 Psaumes 63.1 Proverbes 8.17 Psaumes 119.62 Apocalypse 11.13
10 Mtu mbaya ajapofadhiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa Bwana.Jean 5.37-5.38 Osée 11.7 Matthieu 4.5 Apocalypse 2.21 Jérémie 31.23
11 Bwana, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.Esaïe 5.24 Michée 5.9 Esaïe 11.13 Esaïe 18.3 Apocalypse 19.20
12 Bwana, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.Deutéronome 30.6 Esaïe 57.10 Psaumes 57.2 Psaumes 29.11 Jean 14.27
13 Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.Esaïe 2.8 Romains 6.22 Esaïe 51.22 Esaïe 10.11 2 Chroniques 12.8
14 Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.Esaïe 8.19 Deutéronome 4.28 Psaumes 106.28 Exode 14.30 Esaïe 14.19-14.22
15 Umeliongeza hilo taifa, Bwana, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.Esaïe 9.3 Jérémie 30.19 Esaïe 10.22 Psaumes 86.9-86.10 Jérémie 32.37
16 Bwana, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.Osée 5.15 1 Samuel 1.15 2 Chroniques 6.37-6.38 Deutéronome 4.29-4.30 Esaïe 37.3
17 Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na utungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee Bwana.Jean 16.21 Esaïe 13.8 1 Thessaloniciens 5.3 Esaïe 21.3 Jérémie 30.6
18 Tumekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wo wote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.Psaumes 17.14 Esaïe 33.11 2 Rois 19.3 Josué 7.7-7.9 1 Samuel 11.13
19 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.Daniel 12.2 Ezéchiel 37.1-37.14 Ephésiens 5.14 Osée 13.14 Esaïe 25.8
20 Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.Psaumes 30.5 Psaumes 91.4 Esaïe 54.7-54.8 Psaumes 91.1 Esaïe 10.25
21 Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.Job 16.18 2 Thessaloniciens 1.7-1.10 Luc 11.50 Ezéchiel 24.7-24.8 Luc 11.40

Cette Bible est dans le domaine public.