Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 36.8
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa, katika mwaka wa kumi na nne wa kumiliki kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa.2 Chroniques 32.1 2 Rois 18.13 2 Rois 18.17 Esaïe 8.7-8.8 Esaïe 7.17
2 Mfalme wa Ashuru akamtuma amiri toka Lakishi hata Yerusalemu,kwa mfalme Hezekia,pamoja na jeshi kubwa. Naye akasimama karibu na mfereji wa birika ya juu,iliyo katika njia kuu ya kuuendea uwanda wa dobi.Esaïe 7.3 2 Chroniques 32.9-32.23 2 Rois 18.17-18.37 Esaïe 22.9-22.11
3 Wakamtokea Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe.2 Samuel 20.24-20.25 Esaïe 22.15-22.21 2 Samuel 8.16-8.17
4 Yule amiri akawaambia, Haya, mwambieni Hezekia, kwamba mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, asema hivi, Ni tumaini gani hili unalolitumainia?2 Rois 18.19-18.37 Ezéchiel 31.3-31.18 Proverbes 16.18 2 Chroniques 32.7-32.10 Actes 12.22-12.23
5 Nasema, mashauri yako, na nguvu zako kwa vita, ni maneno yasiyo na maana; basi, unamtumaini nani hata ukaniasi mimi?2 Rois 18.7 Jérémie 52.3 Proverbes 21.30-21.31 Néhémie 2.19-2.20 2 Rois 24.1
6 Tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo, mtu akitegemea juu yake, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.Ezéchiel 29.6-29.7 Jérémie 37.5-37.8 Esaïe 31.3 Esaïe 20.5-20.6 2 Rois 18.21
7 Lakini ukiniambia, Tunamtumaini Bwana, Mungu wetu, je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake mlimoinuka, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii?2 Rois 18.4-18.5 Psaumes 42.5 1 Chroniques 5.20 1 Corinthiens 2.15 2 Chroniques 16.7-16.9
8 Basi sasa, tafadhali mpe bwana wangu, mfalme wa Ashuru, dhamana, nami nitakupa farasi elfu mbili, ikiwa wewe kwa upande wako waweza kupandisha watu juu yao.1 Samuel 17.40-17.43 Psaumes 20.7-20.8 Néhémie 4.2-4.5 Psaumes 123.3-123.4 1 Rois 20.18
9 Wawezaje, basi, kurudisha nyuma uso wa akida mmoja wa watumishi walio wadogo wa bwana wangu, na kuitumainia Misri upewe magari na farasi?Esaïe 10.8 2 Rois 18.24 Esaïe 30.2-30.5 Proverbes 21.31 Deutéronome 17.16
10 Je! Nimepanda mimi, ili kupigana na mahali hapa na kupaangamiza, bila shauri la Bwana? Bwana ndiye aliyeniambia, Panda upigane na nchi hii na kuiangamiza.1 Rois 13.18 Esaïe 37.28 2 Rois 18.25 Esaïe 10.5-10.7 Amos 3.6
11 Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule amiri, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa watu wote walio ukutani.Esdras 4.7 Daniel 2.4 2 Rois 18.26-18.27
12 Lakini yule amiri akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma kwa bwana wako, na kwako wewe, niseme maneno haya? Hakunituma kwa watu hawa walio ukutani, ili wale mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?Ezéchiel 4.16 Esaïe 9.20 2 Rois 18.27 Deutéronome 28.53-28.57 Lamentations 4.9-4.10
13 Kisha yule amiri akasimama akalia kwa sauti kuu kwa lugha ya Kiyahudi, akisema, Lisikieni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru.2 Chroniques 32.18 Psaumes 17.10-17.13 Psaumes 73.8-73.9 2 Rois 18.28-18.32 Esaïe 36.4
14 Mfalme asema hivi; Hezekia asiwadanganye, kwa maana hataweza kuwaokoa;Daniel 3.15-3.17 2 Rois 19.22 2 Rois 19.10-19.13 Apocalypse 13.5-13.6 2 Chroniques 32.13-32.19
15 wala msimwache Hezekia kuwatia moyo wa kumtumaini Bwana; akisema, Bwana bila shaka atatuokoa, mji huu hautatiwa katika mkono wa mfalme wa Ashuru.Matthieu 27.43 Psaumes 71.9-71.11 Psaumes 22.7-22.8 Esaïe 37.10 Psaumes 4.2
16 Msimsikilize Hezekia; maana mfalme wa Ashuru asema hivi, Fanyeni suluhu na mimi, mkatoke mnijie, mkale kila mtu matunda ya mzabibu wake na matunda ya mtini wake, mkanywe kila mmoja maji ya birika yake mwenyewe;Zacharie 3.10 1 Rois 4.25 Michée 4.4 2 Rois 5.15 Proverbes 5.15
17 hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu.2 Rois 18.32 Exode 3.8 Job 20.17 2 Rois 24.11 2 Rois 18.9-18.12
18 Jihadharini, asije Hezekia akawadanganya, akisema, Bwana atatuokoa. Je! Yuko mungu mmoja wa mataifa aliyewaokoa watu wake na mkono wa mfalme wa Ashuru?Esaïe 36.15 2 Rois 18.33-18.35 Psaumes 92.5-92.7 Esaïe 37.17-37.18 Jérémie 10.3-10.5
19 Wako wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Wako wapi miungu ya Sefarvaimu? Je! Wameiokoa Samaria na mkono wangu?Jérémie 49.23 Esaïe 10.9-10.11 2 Samuel 8.9 2 Rois 17.24 Nombres 34.8
20 Katika miungu yote ya nchi hizi ni nani waliookoa nchi yao na mkono wangu, hata Bwana auokoe Yerusalemu na mkono wangu?2 Chroniques 32.19 Esaïe 37.18-37.19 Psaumes 50.21 Esaïe 45.16-45.17 Esaïe 37.23-37.29
21 Lakini watu wakanyamaza kimya; wala hawakumjibu hata neno moja; maana ilikuwa amri ya mfalme, kwamba, Msimjibu neno.Proverbes 26.4 2 Rois 18.26 Matthieu 7.6 Amos 5.13 Proverbes 9.7-9.8
22 Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika tarehe, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule amiri.Esaïe 36.3 Esaïe 33.7 Esaïe 36.11 Matthieu 26.65 Esdras 9.3

Cette Bible est dans le domaine public.