Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 63
Bible en Swahili de l’est


1 Ni nani huyu atokaye Edomu, Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Esaïe 34.5-34.6 Psaumes 137.7 Jude 1.24-1.25 Apocalypse 11.17-11.18 Jean 10.28-10.30
2 Kwani mavazi yako kuwa mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu? Apocalypse 19.13 Apocalypse 19.15
3 Nalikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote. Apocalypse 14.19-14.20 Apocalypse 19.13-19.15 Michée 7.10 Malachie 4.3 Esaïe 25.10
4 Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu, Na mwaka wao niliowakomboa umewadia. Esaïe 34.8 Esaïe 61.2 Esaïe 35.4 Jérémie 51.6 Apocalypse 11.13
5 Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza. Psaumes 44.3 Esaïe 40.10 Esaïe 41.28 Psaumes 98.1 Esaïe 52.10
6 Nikazikanyaga kabila za watu kwa hasira yangu, Nikawalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nikaimwaga damu yao chini. Apocalypse 14.10 Esaïe 49.26 Apocalypse 16.19 Esaïe 63.2-63.3 Psaumes 60.3
7 Nitautaja wema wa Bwana, sifa za Bwana kwa yote aliyotukirimia Bwana; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. Ephésiens 2.4 Psaumes 51.1 Psaumes 86.15 Néhémie 9.35 1 Rois 8.66
8 Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao. Exode 6.7 Esaïe 12.2 Esaïe 43.11 Sophonie 3.7 Deutéronome 33.29
9 Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. Exode 33.14 Deutéronome 7.7-7.8 Malachie 3.1 Exode 23.20-23.21 Juges 10.16
10 Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao. Psaumes 78.40 Ephésiens 4.30 Actes 7.51 Ezéchiel 20.8 Psaumes 78.56
11 Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu? Nombres 11.17 Aggée 2.5 Nombres 11.29 Psaumes 77.20 Exode 14.22
12 Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kuume wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele? Josué 3.16 Exode 15.16 Exode 15.13 Exode 15.6 Exode 14.21-14.22
13 Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae? Psaumes 106.9 Jérémie 31.9 Habakuk 3.15
14 Kama ng’ombe washukao bondeni, Roho ya Bwana akawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu. Josué 23.1 Esaïe 63.12 Ephésiens 1.12 Hébreux 4.8-4.11 Nombres 14.21
15 Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu. Deutéronome 26.15 Psaumes 123.1 Osée 11.8 Psaumes 80.14 Jérémie 31.20
16 Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako. Esaïe 64.8 Esaïe 44.6 Esaïe 41.14 Deutéronome 32.6 Job 14.21
17 Ee Bwana, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako. Nombres 10.36 Psaumes 90.13 Esaïe 6.10 Ezéchiel 14.7-14.9 Jean 12.40
18 Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako. Psaumes 74.3-74.7 Exode 19.4-19.6 Esaïe 62.12 Esaïe 64.11-64.12 Matthieu 24.2
19 Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako. Actes 15.17 Esaïe 65.1 Ephésiens 2.12 Psaumes 79.6 Actes 14.16

Cette Bible est dans le domaine public.