Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Lamentations 4
Bible en Swahili de l’est


1 Jinsi dhahabu ilivyoacha kung’aa, Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika! Mawe ya patakatifu yametupwa Mwanzo wa kila njia. Ezéchiel 7.19-7.22 Lamentations 2.19 Esaïe 1.21 Luc 21.5-21.6 Jérémie 52.13
2 Wana wa Sayuni wenye thamani, Walinganao na dhahabu safi, Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo, Kazi ya mikono ya mfinyanzi! Jérémie 19.11 Esaïe 30.14 Lamentations 2.21 2 Corinthiens 4.7 Jérémie 22.28
3 Hata mbwa-mwitu hutoa matiti, Huwanyonyesha watoto wao; Binti ya watu wangu amekuwa mkali, Mfano wa mbuni jangwani. Esaïe 49.15 Ezéchiel 5.10 Romains 1.31 Jérémie 19.9 2 Rois 6.26-6.29
4 Ulimi wa mtoto anyonyaye Wagandamana na kaakaa lake kwa kiu; Watoto wachanga waomba chakula, Wala hakuna hata mmoja awamegeaye. Psaumes 22.15 Lamentations 2.11-2.12 Lamentations 1.11 Matthieu 7.9-7.11 Psaumes 137.6
5 Wale waliokula vitu vya anasa Wameachwa peke yao njiani; Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu Wakumbatia jaa. Amos 6.3-6.7 Luc 16.19 1 Timothée 5.6 Luc 7.25 2 Samuel 1.24
6 Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwa Kuliko dhambi ya Sodoma, Uliopinduliwa kama katika dakika moja, Wala mikono haikuwekwa juu yake. Genèse 19.25 Luc 10.12 Esaïe 1.9-1.10 Luc 12.47 Matthieu 24.21
7 Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji, Walikuwa weupe kuliko maziwa; Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani, Na umbo lao kama yakuti samawi. Psaumes 51.7 Cantique 5.10 Nombres 6.2-6.21 1 Samuel 16.12 Psaumes 144.12
8 Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa; Hawajulikani katika njia kuu; Ngozi yao yagandamana na mifupa yao Imekauka, imekuwa kama mti. Psaumes 102.3-102.5 Job 30.30 Lamentations 5.10 Job 19.20 Psaumes 119.83
9 Heri wale waliouawa kwa upanga Kuliko wao waliouawa kwa njaa; Maana hao husinyaa, wakichomwa Kwa kukosa matunda ya mashamba. Lévitique 26.39 Ezéchiel 24.23 Jérémie 16.4 Ezéchiel 33.10
10 Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu. Lamentations 2.20 Esaïe 49.15 Jérémie 19.9 Lamentations 3.48 Deutéronome 28.53-28.57
11 Bwana ameitimiza kani yake, Ameimimina hasira yake kali; Naye amewasha moto katika Sayuni Ulioiteketeza misingi yake. Jérémie 7.20 Ezéchiel 22.31 Jérémie 17.27 Lamentations 2.17 Jérémie 14.15-14.16
12 Wafalme wa dunia hawakusadiki, Wala wote wakaao duniani, Ya kwamba mtesi na adui wangeingia Katika malango ya Yerusalemu. Psaumes 48.4-48.6 Jérémie 21.13 Deutéronome 29.24-29.28 1 Rois 9.8-9.9
13 Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wake Na maovu ya makuhani wake, Walioimwaga damu ya wenye haki Katikati yake. Jérémie 5.31 Jérémie 6.13 Matthieu 23.31 Jérémie 26.8-26.9 Lamentations 2.14
14 Hutanga-tanga njiani kama vipofu, Wametiwa unajisi kwa damu; Hata ikawa watu wasiweze Kuyagusa mavazi yao. Jérémie 2.34 Esaïe 1.15 Nombres 19.16 Deutéronome 28.28-28.29 Esaïe 56.10
15 Watu waliwapigia kelele, Ondokeni, Uchafu, Ondokeni, ondokeni, msiguse; Walipokimbia na kutanga-tanga, watu walisema kati ya mataifa, Hawatakaa hapa tena. Lévitique 13.45-13.46
16 Hasira ya Bwana imewatenga, Yeye hatawaangalia tena; Hawakujali nafsi za wale makuhani, Hawakuwaheshimu wazee wao. Esaïe 9.14-9.16 Lamentations 5.12 Lévitique 26.33-26.39 Genèse 49.7 Deutéronome 28.64-28.65
17 Macho yetu yamechoka Kwa kuutazamia bure msaada wetu; Katika kungoja kwetu tumengojea taifa Lisiloweza kutuokoa. Ezéchiel 29.16 Ezéchiel 29.6-29.7 Esaïe 20.5 2 Rois 24.7 Esaïe 30.1-30.7
18 Wanatuvizia hatua zetu, Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu; Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia; Maana mwisho wetu umefika. Amos 8.2 Ezéchiel 7.2-7.12 Lamentations 3.52 Jérémie 16.16 Jérémie 51.33
19 Waliotufuatia ni wepesi Kuliko tai za mbinguni; Hao walitufuatia milimani, Nao walituotea jangwani. Esaïe 5.26-5.28 Habakuk 1.8 Jérémie 4.13 Esaïe 30.16-30.17 Deutéronome 28.49
20 Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao;Ambaye kwa habari zake tulisema,Chini ya kivuli chake tukakaa kati ya mataifa. 2 Samuel 19.21 Jérémie 39.5 Genèse 2.7 Ezéchiel 12.13 Lamentations 2.9
21 Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu, Ukaaye katika nchi ya Usi; Hata kwako kikombe kitapita, Utalewa, na kujifanya uchi. Psaumes 137.7 Job 1.1 Amos 1.11 Ezéchiel 25.8 Michée 1.11
22 Uovu wako umetimia, Ee binti Sayuni; Hatakuhamisha tena; Atapatiliza uovu wako, Ee binti Edomu; Atazivumbua dhambi zako. Esaïe 40.2 Psaumes 137.7 Malachie 1.4 Lamentations 4.21 Ezéchiel 37.28

Cette Bible est dans le domaine public.