Arrangement des lampes et du chandelier 1 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
2 Nena na Haruni, ukamwambie, Utakapoziweka taa, hizo taa saba zitatoa nuru hapo mbele ya kinara cha taa.
Exode 25.37 Exode 37.18-37.19 Lévitique 24.4 Lévitique 24.1-24.2 Esaïe 8.20 3 Basi Haruni akafanya; akaziweka taa zake ili zitoe nuru hapo mbele ya kinara, kama Bwana alivyomwagiza Musa.
4 Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu tako lake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano Bwana aliokuwa amemwonyesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.
Exode 25.31-25.40 Exode 25.18 Exode 25.9 Exode 37.17-37.24 Hébreux 8.5 Consécration des Lévites 5 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
6 Watwae Walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kisha uwatakase.
2 Corinthiens 7.1 Exode 19.15 Jacques 4.8 Esaïe 52.11 7 Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa; nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kisha wazifue nguo zao, na kujitakasa.
Lévitique 8.6 Nombres 19.13 Lévitique 16.28 Lévitique 14.7-14.9 Genèse 35.2 8 Kisha na watwae ng’ombe mume mmoja mchanga, na sadaka yake ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, nawe utatwaa ng’ombe mume mchanga mwingine kuwa sadaka ya dhambi.
Lévitique 2.1 Esaïe 53.10 Lévitique 1.3 Lévitique 8.2 Exode 29.3 9 Nawe utawahudhurisha Walawi mbele ya hema ya kukutania; nawe utaukutanisha mkutano wote wa wana wa Israeli;
Exode 40.12 Lévitique 8.3 Exode 29.4-29.37 10 nawe utawahudhurisha Walawi mbele za Bwana; kisha wana wa Israeli wataweka mikono yao juu ya Walawi;
Lévitique 1.4 Actes 6.6 1 Timothée 5.22 Actes 13.2-13.3 Nombres 3.45 11 naye Haruni atawasongeza Walawi mbele za Bwana wawe sadaka ya kutikiswa, kwa ajili ya wana wa Israeli, ili wawe wenye kufanya utumishi wa Bwana.
Lévitique 7.30 Lévitique 8.29 Nombres 1.49-1.53 Exode 29.24 Lévitique 8.27 12 Kisha Walawi wataweka mikono yao juu ya vichwa vya hao ng’ombe; nawe umtoe mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa Bwana, na huyo wa pili awe sadaka ya kuteketezwa, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Walawi.
Exode 29.10 Lévitique 8.14 Lévitique 1.4 Nombres 8.8 Lévitique 8.34 13 Kisha utawaweka Walawi mbele ya Haruni, na mbele ya wanawe na kuwasongeza kwa Bwana wawe sadaka ya kutikiswa.
Nombres 8.11 Nombres 8.21 Romains 15.16 Nombres 18.6 Romains 12.1 14 Ndivyo utakavyowatenga Walawi na kuwatoa katika wana wa Israeli; na Walawi watakuwa wangu.
Nombres 3.45 Hébreux 7.26 Nombres 16.9-16.10 Nombres 18.6 Nombres 6.2 15 Kisha baadaye Walawi wataingia ndani, ili wafanye utumishi wa hema ya kukutania; nawe utawatakasa, na kuwasongeza wawe sadaka ya kutikiswa.
Nombres 8.11 Nombres 8.13 Nombres 3.23-3.37 Nombres 4.3-4.32 1 Chroniques 25.1-25.26 16 Kwa kuwa nimepewa kabisa mimi watu hawa kutoka katika wana wa Israeli; badala ya wote wafunguao mimba, maana, wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wote, nimewatwaa wawe wangu. Nombres 3.12 Nombres 3.45 Nombres 3.9 17 Kwa kuwa wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli ni wangu, wa wanadamu na wa wanyama; siku hiyo niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri niliwatakasa kwa ajili yangu mwenyewe.
Exode 13.2 Luc 2.23 Exode 13.12-13.15 Hébreux 11.28 Nombres 3.13 18 Nami nimewatwaa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote walio katika wana wa Israeli.
19 Nami nimempa Haruni hao Walawi wawe kipawa chake yeye na wanawe, kutoka kwa wana wa Israeli, ili watumike utumishi wa wana wa Israeli katika hema ya kukutania, kisha wafanye upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli; ili kusiwe na maradhi kati ya wana wa Israeli, hapo wana wa Israeli watakapopakaribia mahali patakatifu.
Nombres 1.53 Nombres 16.46 2 Chroniques 26.16-26.20 Ezéchiel 44.11-44.14 Nombres 3.6-3.9 20 Basi Musa na Haruni, na mkutano wote wa wana wa Israeli, wakawafanyia Walawi mambo hayo; kama hayo yote Bwana aliyomwagiza Musa kwa habari za hao Walawi, ndivyo wana wa Israeli walivyowafanyia.
21 Walawi wakajitakasa na dhambi, nao wakafua nguo zao; kisha Haruni akawasongeza mbele za Bwana wawe sadaka ya kutikiswa; Haruni akafanya kwa ajili yao ili kuwatakasa.
Nombres 8.7 Nombres 8.15 Nombres 8.11-8.13 Nombres 19.12 Nombres 19.19 22 Kisha baada ya hayo Walawi wakaingia ili wafanye utumishi wao ndani ya hema ya kukutania mbele ya Haruni na mbele ya wanawe; kama Bwana alivyomwagiza Musa kwa habari za hao Walawi, ndivyo walivyowafanyia.
2 Chroniques 30.15-30.17 2 Chroniques 31.2 2 Chroniques 35.8-35.15 2 Chroniques 30.27 Nombres 8.15 23 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
24 Mambo yawapasayo hao Walawi ni haya; tangu waliopata umri wa miaka ishirini na mitano na zaidi wataingia ndani ili watumike utumishi katika kazi ya hema ya kukutania;
Nombres 4.3 1 Chroniques 23.3 Nombres 4.23 2 Corinthiens 10.4 1 Corinthiens 9.7 25 tena tangu waliopata umri wa miaka hamsini wataacha kutumika huo utumishi, wasitumike tena;
Nombres 4.23 2 Timothée 4.7 26 lakini watatumika pamoja na ndugu zao katika hema ya kukutania, kushika ulinzi, lakini wasitumike katika huo utumishi tena. Ndivyo utakavyowafanyia Walawi katika mambo ya ulinzi wao.
Nombres 1.53 Nombres 3.32 Ezéchiel 44.8 Ezéchiel 44.11 1 Timothée 4.15