Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Romains 10
Bible en Swahili de l’est


1 Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe. 1 Corinthiens 9.20-9.22 Jean 5.34 1 Samuel 15.11 Romains 9.1-9.3 Jérémie 18.20
2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Actes 21.20 Philippiens 1.9 Philippiens 3.6 Romains 9.31-9.32 2 Corinthiens 4.6
3 Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Luc 16.15 Philippiens 3.9 Apocalypse 3.17-3.18 Romains 1.17 Néhémie 9.33
4 Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki. Galates 3.24 Romains 8.3-8.4 Hébreux 9.7-9.14 Romains 7.1-7.4 Actes 13.38-13.39
5 Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo. Lévitique 18.5 Ezéchiel 20.21 Ezéchiel 20.13 Néhémie 9.29 Galates 3.12
6 Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini), Deutéronome 30.11-30.14 Ephésiens 4.8-4.10 Jean 6.38 Philippiens 3.9 Jean 6.33
7 au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.) Hébreux 13.20 Romains 4.25 Apocalypse 1.18 1 Pierre 3.22 1 Pierre 3.18
8 Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. Deutéronome 30.14 Romains 1.16-1.17 1 Timothée 4.6 1 Pierre 1.25 Romains 10.17
9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Luc 12.8 Philippiens 2.11 1 Jean 4.2-4.3 1 Corinthiens 15.14-15.18 Actes 16.31
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Philippiens 3.9 Hébreux 3.12 Jean 3.19-3.21 Romains 10.9 Hébreux 10.22
11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Esaïe 28.16 1 Pierre 2.6 Romains 9.33 Esaïe 49.23 Jérémie 17.7
12 Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; Romains 3.22 Galates 3.28 Romains 2.4 Psaumes 86.5 Psaumes 145.18
13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Actes 2.21 Joël 2.32
14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Marc 16.15-16.16 Tite 1.3 Luc 24.46-24.47 Ephésiens 4.21 Jonas 3.5-3.9
15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema! Esaïe 52.7 Nahum 1.15 Esaïe 61.1 Ephésiens 6.15 Ephésiens 3.8
16 Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu? Esaïe 53.1 Romains 3.3 1 Pierre 2.8 Jean 12.38-12.40 Hébreux 4.2
17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Galates 3.2 Galates 3.5 Marc 4.24 Romains 1.16 Jacques 1.18-1.21
18 Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Psaumes 19.4 Romains 1.8 Colossiens 1.23 Colossiens 1.6 Matthieu 24.14
19 Lakini nasema, Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena, Nitawatia wivu kwa watu ambao si taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhibisha. Deutéronome 32.21 Romains 11.11 Romains 11.14 Tite 3.3 1 Corinthiens 10.19
20 Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia. Romains 9.30 Esaïe 65.1-65.2 Matthieu 22.9-22.10 Esaïe 49.6 Luc 14.23
21 Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi. Jérémie 35.15 Esaïe 65.2-65.5 1 Samuel 8.7-8.8 Actes 13.46-13.47 Deutéronome 9.13

Cette Bible est dans le domaine public.