Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
1 Samuel 6 Bible en Swahili de l’est
Retour de l’arche de l’alliance en Israël
1 Basi, hilo sanduku la Bwana lilikuwamo katika nchi ya Wafilisti muda wa miezi saba. 1 Samuel 5.10-5.11 Psaumes 78.61 1 Samuel 5.3 1 Samuel 5.1 2 Nao Wafilisti wakawaita makuhani na waaguzi, wakasema, Tulifanyieje sanduku la Bwana? Tuonyesheni jinsi tuwezavyo kulirudisha mahali pake. Genèse 41.8 Exode 7.11 Daniel 2.2 Daniel 5.7 Esaïe 2.6 3 Nao wakajibu, Mkilirudisha hilo sanduku la Mungu wa Israeli, msilirudishe kitupu; lakini msikose kumpelekea na matoleo ya kosa; hivyo mtapona, tena mtafunuliwa ni kwa sababu gani mkono wake haukuondolewa kwenu. 1 Samuel 6.9 Exode 23.15 Deutéronome 16.16 Exode 34.20 Lévitique 5.15-5.19 4 Ndipo wakauliza, Na hayo matoleo ya kosa yatakuwa ya namna gani, hayo tutakayompelekea? Nao wakajibu, Na yawe majipu ya dhahabu matano, na panya wa dhahabu watano, sawasawa na idadi ya mashehe wa Wafilisti; kwa kuwa tauni moja ilikuwa juu yenu nyote, na juu ya mashehe wenu. Juges 3.3 Josué 13.3 1 Samuel 6.17-6.18 1 Samuel 5.9 1 Samuel 5.6 5 Kwa hiyo mtafanyiza sanamu za majipu yenu, na sanamu za panya wenu waiharibuo nchi; nanyi mtamtukuza huyo Mungu wa Israeli; huenda ataupunguza uzito wa mkono wake juu yenu, na juu ya miungu yenu, na juu ya nchi yenu. Josué 7.19 1 Samuel 5.6-5.7 1 Samuel 5.11 1 Samuel 5.3-5.4 Esaïe 42.12 6 Mbona, basi, mnaifanya migumu mioyo yenu, kama vile wale Wamisri, naye yule Farao, walivyoifanya migumu mioyo yao? Hata na hao, hapo alipokwisha kuwadhihaki, je! Hawakuwaruhusu watu, nao wakaenda zao? Exode 14.17 Exode 7.13 Exode 8.15 Exode 9.34 Exode 14.23 7 Basi sasa jifanyizieni gari jipya, mtwae na ng’ombe wake wawili wakamwao, ambao hawajafungwa nira, nanyi mkawafunge hao ng’ombe garini, na kuwaondoa ndama zao na kuwatia zizini; 2 Samuel 6.3 Nombres 19.2 1 Chroniques 13.7 8 kisha, litwaeni hilo sanduku la Bwana, na kuliweka juu ya gari; na hivyo vitu vya dhahabu, mtakavyompelekea kuwa matoleo ya kosa, mvitie katika kasha kando yake; mkalipeleke sanduku, lipate kwenda. 1 Samuel 6.3-6.5 9 Kisha angalieni, likikwea kwa njia ya mpakani mwake kwenda Beth-shemeshi, basi, ndiye aliyetutenda uovu huo mkuu; la, sivyo, ndipo tutakapojua ya kwamba si mkono wake uliotupiga; ilikuwa ni ajali iliyotupata. Josué 15.10 Josué 21.16 1 Samuel 6.3 2 Samuel 1.6 Luc 10.31 10 Basi watu wale walifanya hivyo; wakatwaa ng’ombe wawili wakamwao, wakawafunga garini, na ndama zao wakawafunga zizini; 11 kisha wakaliweka sanduku la Bwana juu ya gari, pamoja na kasha lenye panya wa dhahabu na sanamu za majipu yao. 1 Chroniques 15.13-15.15 2 Samuel 6.3 1 Chroniques 13.7 12 Na hao ng’ombe wakashika njia moja kwa moja kwenda Beth-shemeshi; wakaiandama njia ya barabara, wakaenda wakilia, lakini hawakugeukia upande wa kuume wala wa kushoto; na mashehe wa Wafilisti wakawafuata hata kuufikia mpaka wa Beth-shemeshi. Nombres 20.19 13 Nao watu wa Beth-shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao bondeni; wakainua macho yao, wakaliona sanduku, wakafurahi sana kuliona. 14 Na lile gari likaingia katika konde la Yoshua wa Beth-shemeshi, na kusimama pale pale, palipokuwapo jiwe kubwa; basi wakaipasua miti ya lile gari, wakawatoa wale ng’ombe kuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. 2 Samuel 24.22 1 Samuel 20.29 1 Rois 18.30-18.38 Juges 21.4 2 Samuel 24.18 15 Nao Walawi walilishusha sanduku la Bwana, na lile kasha lililokuwa pamoja nalo, lenye vile vitu vya dhahabu; wakaviweka juu ya lile jiwe kubwa; nao watu wa Beth-shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja dhabihu siku iyo hiyo kwa Bwana. Josué 3.3 16 Na hao mashehe watano wa Wafilisti, hapo walipokwisha kuyaona hayo, walirejea Ekroni siku iyo hiyo. Juges 3.3 Josué 13.3 1 Samuel 6.4 Juges 16.5 1 Samuel 6.12 17 Hii ndiyo hesabu ya yale majipu waliyoyapeleka wale Wafilisti, yawe matoleo ya kosa kwa Bwana; kwa Ashdodi moja, kwa Gaza moja, kwa Ashkeloni moja, kwa Gathi moja, na kwa Ekroni moja; 2 Samuel 1.20 Amos 6.2 2 Samuel 21.22 2 Chroniques 26.6 Juges 16.1 18 na panya wa dhahabu, kwa idadi ya miji yote ya Wafilisti, milki zao wale mashehe watano, miji yenye maboma na vijiji vya mashamba pia. Nalo lile jiwe kubwa, ambalo juu yake waliliweka sanduku la Bwana, liko hata hivi leo hapo kondeni pa Yoshua wa Beth-shemeshi. Josué 13.3 1 Samuel 6.14-6.16 Deutéronome 3.5 19 Basi Bwana aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-shemeshi, kwa sababu wamechungulia ndani ya hilo sanduku la Bwana, wapata watu sabini, na watu hamsini elfu; nao watu wakalalamika, kwa kuwa Bwana amewapiga watu kwa uuaji mkuu. Nombres 4.15 Nombres 4.20 2 Samuel 6.7 Exode 19.21 1 Chroniques 13.9-13.10 20 Nao watu wa Beth-shemeshi wakasema, Ni nani awezaye kusimama mbele za Bwana, huyu Mungu mtakatifu? Naye atapanda kwenda kwa nani kutoka kwetu? 2 Samuel 6.9 Malachie 3.2 Apocalypse 6.17 Luc 5.8 Luc 8.37 21 Nao wakatuma wajumbe waende kwa wenyeji wa Kiriath-yearimu, kusema, Wafilisti wamelirudisha sanduku la Bwana; basi shukeni, mkalichukue kwenu. 1 Chroniques 13.5-13.6 Josué 9.17 Josué 18.14 Jérémie 7.14 Psaumes 78.60