Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 16.1
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Nimesikia maneno mengi mfano wa hayo; Ninyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha.Job 13.4-13.5 Job 19.2-19.3 Jacques 1.19 Psaumes 69.26 Philippiens 1.16
3 Je! Maneno yasiyo faida yatakuwa na mwisho? Au, kuna nini kinachokukasirisha, hata ukajibu?Job 6.26 Job 15.2 Tite 1.11 Tite 2.8 Matthieu 22.46
4 Mimi nami ningeweza kunena kama ninyi; Kama roho zenu zingekuwa mahali pa roho yangu, Ningeweza kutunga maneno juu yenu, Na kuwatikisia ninyi kichwa changu.Psaumes 22.7 Psaumes 109.25 Lamentations 2.15 2 Rois 19.21 Jérémie 18.16
5 Lakini ningewatia nguvu kwa kinywa changu, Na utuzo wa midomo yangu ungetuliza.Proverbes 27.9 Psaumes 27.14 Proverbes 27.17 Job 4.3-4.4 Esaïe 35.3-35.4
6 Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi; Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?Psaumes 88.15-88.18 Job 10.1 Psaumes 77.1-77.9
7 Lakini sasa amenichokesha; Jamii yangu yote umeifanya ukiwa.Job 7.3 Job 1.15-1.19 Psaumes 6.6-6.7 Proverbes 3.11-3.12 Esaïe 50.4
8 Umenishika sana, ni ushahidi juu yangu; Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.Job 10.17 Job 19.20 Ruth 1.21 Esaïe 10.16 Psaumes 106.15
9 Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesaga-saga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.Lamentations 2.16 Psaumes 35.16 Job 13.24 Actes 7.54 Job 18.4
10 Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hujikutanisha pamoja juu yangu.Psaumes 22.13 Psaumes 35.15 Michée 5.1 Lamentations 3.30 Esaïe 50.6
11 Mungu amenitia kwa hao wapotovu, Na kunitupa mikononi mwao waovu.Psaumes 31.8 Psaumes 27.12 Job 2.7 2 Corinthiens 12.7 1 Samuel 24.18
12 Nilikuwa katika raha, naye akanivunja-vunja; Naam, amenishika shingo, na kuniponda; Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.Job 7.20 Lamentations 3.4 Lamentations 3.11-3.12 Ezéchiel 29.7 Romains 16.4
13 Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote, Hunipasua viuno vyangu, asinihurumie; Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.Job 6.4 Job 20.25 Lamentations 2.11 Romains 8.32 Lamentations 3.13
14 Hunivunja kwa uvunjifu juu ya uvunjifu; Hunishambulia mfano wa jitu shujaa.Joël 2.7 Job 9.17 Psaumes 42.7 Lamentations 3.3-3.5 Juges 15.8
15 Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu, Na pembe yangu nimeidhili uvumbini.Genèse 37.34 Psaumes 7.5 Psaumes 75.5 1 Rois 21.27 Esaïe 22.12
16 Uso wangu umeharibika kwa kutoa machozi, Na giza tupu li katika kope zangu;Marc 14.34 Job 17.7 Esaïe 52.14 Psaumes 116.3 Jonas 2.1-2.10
17 Ijapokuwa hapana jeuri mikononi mwangu, Na kuomba kwangu ni safi.Job 15.20 Job 11.14 Job 22.5-22.9 Job 31.1-31.40 Proverbes 15.8
18 Ee nchi, usiifunike damu yangu, Na kilio changu kisipate mahali pa kupumzika.Ezéchiel 24.7 Esaïe 26.21 Genèse 4.11 Psaumes 66.18-66.19 Jacques 4.3-4.4
19 Hata sasa, tazama, shahidi wangu yuko mbinguni. Na huyo atakayenidhamini yuko juu.Romains 1.9 1 Samuel 12.5 1 Thessaloniciens 2.5 2 Corinthiens 11.31 Job 25.2
20 Rafiki zangu hunidharau; Lakini jicho langu humwagia Mungu machozi;Job 16.4 Job 12.4-12.5 Hébreux 5.7 Psaumes 142.2 Osée 12.4-12.5
21 Laiti angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu, Amtetee na mwanadamu mbele ya jirani yake.Job 31.35 Job 13.3 Esaïe 45.9 Job 13.22 Job 40.1-40.5
22 Kwani ikiisha pita miaka michache, Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.Job 14.10 Job 14.14 Ecclésiaste 12.5 Job 7.9-7.10 Job 14.5

Cette Bible est dans le domaine public.