Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 16.19
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Nimesikia maneno mengi mfano wa hayo; Ninyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha.Job 13.4-13.5 Job 6.25 Job 11.2-11.3 Job 19.2-19.3 Jacques 1.19
3 Je! Maneno yasiyo faida yatakuwa na mwisho? Au, kuna nini kinachokukasirisha, hata ukajibu?Job 6.26 Job 15.2 Job 8.2 Tite 1.11 Tite 2.8
4 Mimi nami ningeweza kunena kama ninyi; Kama roho zenu zingekuwa mahali pa roho yangu, Ningeweza kutunga maneno juu yenu, Na kuwatikisia ninyi kichwa changu.Psaumes 22.7 Psaumes 109.25 Lamentations 2.15 2 Rois 19.21 Jérémie 18.16
5 Lakini ningewatia nguvu kwa kinywa changu, Na utuzo wa midomo yangu ungetuliza.Galates 6.1 Job 6.14 Proverbes 27.9 Psaumes 27.14 Proverbes 27.17
6 Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi; Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?Job 10.1 Psaumes 88.15-88.18 Psaumes 77.1-77.9
7 Lakini sasa amenichokesha; Jamii yangu yote umeifanya ukiwa.Job 7.3 Job 1.15-1.19 Michée 6.13 Psaumes 6.6-6.7 Proverbes 3.11-3.12
8 Umenishika sana, ni ushahidi juu yangu; Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.Job 10.17 Job 19.20 Ruth 1.21 Psaumes 109.24 Esaïe 10.16
9 Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesaga-saga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.Lamentations 2.16 Psaumes 35.16 Job 13.24 Actes 7.54 Job 18.4
10 Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hujikutanisha pamoja juu yangu.Psaumes 22.13 Psaumes 35.15 Esaïe 50.6 Actes 23.2 Michée 5.1
11 Mungu amenitia kwa hao wapotovu, Na kunitupa mikononi mwao waovu.Psaumes 31.8 Psaumes 27.12 Romains 11.32 Job 1.13-1.19 Job 2.7
12 Nilikuwa katika raha, naye akanivunja-vunja; Naam, amenishika shingo, na kuniponda; Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.Job 7.20 Lamentations 3.4 Lamentations 3.11-3.12 Job 4.10 Job 29.3
13 Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote, Hunipasua viuno vyangu, asinihurumie; Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.Job 20.25 Job 6.4 Lamentations 2.11 2 Pierre 2.5 Romains 8.32
14 Hunivunja kwa uvunjifu juu ya uvunjifu; Hunishambulia mfano wa jitu shujaa.Lamentations 3.3-3.5 Juges 15.8 Joël 2.7 Job 9.17 Psaumes 42.7
15 Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu, Na pembe yangu nimeidhili uvumbini.Genèse 37.34 Psaumes 7.5 Esaïe 22.12 Psaumes 75.5 1 Rois 21.27
16 Uso wangu umeharibika kwa kutoa machozi, Na giza tupu li katika kope zangu;Psaumes 102.9 Psaumes 31.9 Marc 14.34 Job 17.7 Esaïe 52.14
17 Ijapokuwa hapana jeuri mikononi mwangu, Na kuomba kwangu ni safi.Job 15.34 Job 8.5-8.6 Job 15.20 Job 11.14 Job 22.5-22.9
18 Ee nchi, usiifunike damu yangu, Na kilio changu kisipate mahali pa kupumzika.Ezéchiel 24.7 Esaïe 26.21 Genèse 4.11 Psaumes 66.18-66.19 Néhémie 4.5
19 Hata sasa, tazama, shahidi wangu yuko mbinguni. Na huyo atakayenidhamini yuko juu.Romains 1.9 Genèse 31.50 1 Samuel 12.5 1 Thessaloniciens 2.5 2 Corinthiens 11.31
20 Rafiki zangu hunidharau; Lakini jicho langu humwagia Mungu machozi;Psaumes 109.4 Luc 6.11-6.12 Job 16.4 Job 12.4-12.5 Hébreux 5.7
21 Laiti angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu, Amtetee na mwanadamu mbele ya jirani yake.Job 31.35 Romains 9.20 Job 9.34-9.35 Job 13.3 Esaïe 45.9
22 Kwani ikiisha pita miaka michache, Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.Job 14.10 Job 14.14 Job 14.5 Ecclésiaste 12.5 Job 7.9-7.10

Cette Bible est dans le domaine public.