Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 71.6
Bible en Swahili de l’est


1 Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele.Psaumes 31.1-31.3 Psaumes 25.2-25.3 Psaumes 125.1 Psaumes 22.5 1 Pierre 2.6
2 Kwa haki yako uniponye, uniopoe, Unitegee sikio lako, uniokoe.Psaumes 17.6 Psaumes 31.1 Psaumes 17.2 Psaumes 143.1 Psaumes 43.1
3 Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Nitakakokwenda sikuzote. Umeamuru niokolewe, Ndiwe genge langu na ngome yangu.Psaumes 18.2 Psaumes 31.2-31.3 Psaumes 44.4 Psaumes 68.28 Psaumes 91.11-91.12
4 Ee Mungu wangu, uniopoe mkononi mwa mkorofi, Katika mkono wake mwovu, mdhalimu,Psaumes 59.1-59.2 Psaumes 140.1-140.4 2 Samuel 16.21-16.22 2 Samuel 17.12-17.14 2 Samuel 17.21
5 Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.Jérémie 17.7 Jérémie 17.13 1 Samuel 17.45-17.47 Psaumes 71.17 Jérémie 17.17
6 Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.Psaumes 22.9-22.10 Psaumes 139.15-139.16 Jérémie 1.5 Psaumes 34.1 Esaïe 49.5
7 Nimekuwa kitu cha ajabu kwa watu wengi, Na Wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.Esaïe 8.18 1 Corinthiens 4.9 Luc 2.34 2 Corinthiens 4.8-4.12 Zacharie 3.6
8 Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa.Psaumes 146.2 Psaumes 35.28 Psaumes 104.1 Psaumes 71.24 Psaumes 145.1-145.2
9 Usinitupe wakati wa uzee, Nguvu zangu zipungukapo usiniache.Esaïe 46.4 Psaumes 71.18 Psaumes 90.10 Psaumes 92.13-92.15 Ecclésiaste 12.1-12.7
10 Kwa maana adui zangu wananiamba, Nao wanaoniotea roho yangu hushauriana.Psaumes 56.6 Psaumes 83.3 Matthieu 27.1 Psaumes 10.9 Psaumes 37.32-37.33
11 Wakisema, Mungu amemwacha, Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya.Psaumes 7.2 Psaumes 3.2 Daniel 3.15 Psaumes 37.25 Matthieu 27.49
12 Ee Mungu, usiwe mbali nami; Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia.Psaumes 38.21-38.22 Psaumes 35.22 Psaumes 22.11 Psaumes 70.1-70.2 Psaumes 69.18
13 Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.Psaumes 109.29 Psaumes 71.24 Psaumes 35.4 Psaumes 35.26 Esther 9.2
14 Nami nitatumaini daima, Nitazidi kuongeza sifa zake zote.1 Jean 3.3 Lamentations 3.26 1 Thessaloniciens 4.10 Philippiens 1.9 Psaumes 43.5
15 Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako Mchana kutwa; maana sijui hesabu yake.Psaumes 40.5 Psaumes 35.28 Psaumes 145.2 Psaumes 71.8 Psaumes 89.16
16 Nitakuja na mambo ya ajabu ya Bwana MUNGU; Nitawakumbusha watu haki yako Wewe peke yako.Psaumes 51.14 2 Timothée 2.1 Esaïe 40.31 Romains 3.21 Romains 1.17
17 Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.Psaumes 66.16 Psaumes 119.102 1 Samuel 17.36-17.37 Psaumes 71.5 2 Samuel 22.1-22.51
18 Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.Psaumes 71.9 Esaïe 46.4 Psaumes 78.4 Exode 13.8 Psaumes 78.6
19 Na haki yako, Ee Mungu, Imefika juu sana. Wewe uliyefanya mambo makuu; Ee Mungu, ni nani aliye kama Wewe?Psaumes 35.10 Psaumes 57.10 Psaumes 36.5-36.6 Esaïe 55.9 Psaumes 89.6-89.8
20 Wewe, uliyetuonyesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Tokea pande za chini ya nchi.Psaumes 138.7 Osée 6.1-6.2 Psaumes 60.3 Psaumes 80.18 Jonas 2.6
21 Laiti ungeniongezea ukuu! Urejee tena na kunifariji moyo.2 Samuel 3.1 Esaïe 12.1 2 Corinthiens 7.13 Esaïe 49.13 Esaïe 9.7
22 Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli.2 Rois 19.22 Psaumes 89.18 Psaumes 33.2 Esaïe 60.9 Psaumes 92.1-92.3
23 Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo, Na nafsi yangu uliyoikomboa.Psaumes 103.4 Psaumes 104.33 Psaumes 34.22 2 Samuel 4.9 Genèse 48.16
24 Ulimi wangu nao utasimulia Haki yako mchana kutwa. Kwa maana wameaibishwa, Wametahayarika, wanaonitakia mabaya.Psaumes 71.13 Psaumes 35.28 Psaumes 92.11 1 Corinthiens 15.25 Psaumes 18.37-18.43

Cette Bible est dans le domaine public.