Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 72.10
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako.1 Chroniques 22.12-22.13 Jérémie 23.5-23.6 Jean 3.34 Esaïe 11.2 Psaumes 127.1
2 Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu.Esaïe 32.1 Esaïe 9.7 Psaumes 45.6-45.7 Psaumes 72.12-72.14 1 Rois 3.5-3.10
3 Milima itawazalia watu amani, Na vilima navyo kwa haki.Esaïe 52.7 Esaïe 32.16-32.17 Psaumes 72.16 2 Corinthiens 5.19-5.21 Joël 3.18
4 Atawahukumu walioonewa wa watu, Atawaokoa wahitaji, atamseta mwenye kuonea.Esaïe 11.4 Matthieu 11.5 Job 34.24 Ezéchiel 34.15-34.16 Apocalypse 18.6-18.8
5 Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua, Na wakati wa kung’aa mwezi kizazi hata kizazi.Psaumes 89.36-89.37 Psaumes 72.17 Luc 1.32-1.33 1 Rois 3.28 Daniel 7.27
6 Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi.Osée 6.3 Deutéronome 32.2 2 Samuel 23.4 Proverbes 19.12 Psaumes 65.10
7 Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.Esaïe 2.4 Ephésiens 2.14-2.17 Psaumes 92.12 Malachie 4.2 Esaïe 55.10-55.13
8 Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka Mto hata miisho ya dunia.Zacharie 9.10 Exode 23.31 Psaumes 2.8 Psaumes 89.25 Psaumes 80.11
9 Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi.Michée 7.17 Esaïe 49.23 Psaumes 22.29 Psaumes 110.1 Psaumes 2.9
10 Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.Esaïe 60.6 Psaumes 68.29 Esaïe 49.7 1 Rois 10.1 2 Chroniques 9.21
11 Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.Psaumes 86.9 Psaumes 138.4-138.5 Esaïe 49.22-49.23 Psaumes 2.10-2.12 Romains 11.25
12 Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.Job 29.12 Psaumes 72.4 Psaumes 102.20 2 Corinthiens 8.9 Luc 7.22
13 Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa.Matthieu 5.3 Ezéchiel 34.16 Matthieu 18.10 Job 5.15-5.16 Psaumes 109.31
14 Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu, Na damu yao ina thamani machoni pake.Psaumes 116.15 Apocalypse 17.6 Genèse 48.16 2 Samuel 4.9 Luc 1.68-1.75
15 Basi na aishi; Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa.Jude 1.25 1 Rois 10.14 Apocalypse 5.8-5.14 Jean 14.19 2 Chroniques 9.4-9.8
16 Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawaye-waye kama Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi.Esaïe 35.2 Esaïe 44.3-44.5 Esaïe 32.15 Actes 1.15 Jérémie 33.22
17 Jina lake na lidumu milele, Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao; Mataifa yote na wajibariki katika yeye, Na kumwita heri.Genèse 12.3 Genèse 22.18 Psaumes 89.36 Luc 1.48 Esaïe 7.14
18 Na ahimidiwe Bwana, Mungu, Mungu wa Israeli, Atendaye miujiza Yeye peke yake;Psaumes 41.13 Psaumes 136.4 1 Chroniques 29.10 Psaumes 86.10 Exode 15.11
19 Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.Nombres 14.21 Néhémie 9.5 Psaumes 41.13 Esaïe 6.3 Zacharie 14.9
20 Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamekwisha.2 Samuel 23.1 Job 31.40 Jérémie 51.64 Luc 24.51

Cette Bible est dans le domaine public.