Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 72
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako. 1 Chroniques 22.12-22.13 Jean 3.34 Esaïe 11.2 Psaumes 127.1 1 Rois 1.39-2.4
2 Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu. Esaïe 32.1 Esaïe 9.7 1 Rois 3.5-3.10 Esaïe 11.2-11.5 Psaumes 82.3-82.4
3 Milima itawazalia watu amani, Na vilima navyo kwa haki. Esaïe 52.7 2 Corinthiens 5.19-5.21 Joël 3.18 Psaumes 65.12 Psaumes 98.8-98.9
4 Atawahukumu walioonewa wa watu, Atawaokoa wahitaji, atamseta mwenye kuonea. Esaïe 11.4 Esaïe 51.12-51.13 Apocalypse 18.20 Apocalypse 19.2 Psaumes 2.9
5 Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua, Na wakati wa kung’aa mwezi kizazi hata kizazi. Psaumes 89.36-89.37 Psaumes 72.17 Daniel 7.27 Esaïe 9.7 Ephésiens 3.21
6 Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi. Osée 6.3 Deutéronome 32.2 2 Samuel 23.4 Psaumes 65.10 Ezéchiel 34.23-34.26
7 Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma. Esaïe 2.4 Ephésiens 2.14-2.17 Psaumes 92.12 Esaïe 35.1-35.10 Actes 4.32
8 Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka Mto hata miisho ya dunia. Zacharie 9.10 Exode 23.31 Psaumes 89.25 Psaumes 80.11 Psaumes 2.8
9 Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. Michée 7.17 Esaïe 49.23 Psaumes 2.9 Psaumes 21.8-21.9 1 Rois 9.20-9.21
10 Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa. Psaumes 68.29 Esaïe 49.7 1 Rois 10.1 Esaïe 60.6 2 Chroniques 9.21
11 Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie. Psaumes 86.9 Psaumes 138.4-138.5 Esaïe 49.22-49.23 Esaïe 11.9 Esaïe 54.5
12 Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Job 29.12 Psaumes 72.4 Luc 7.22 Psaumes 82.3-82.4 Luc 4.18
13 Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa. Matthieu 18.10 Job 5.15-5.16 Psaumes 109.31 Jacques 2.5-2.6 Matthieu 5.3
14 Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu, Na damu yao ina thamani machoni pake. Psaumes 116.15 2 Samuel 4.9 Luc 1.68-1.75 Psaumes 130.8 Psaumes 25.22
15 Basi na aishi; Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa. 1 Rois 10.14 Apocalypse 5.8-5.14 Jude 1.25 Jean 16.23-16.24 Psaumes 21.4
16 Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawaye-waye kama Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi. Jérémie 33.22 Job 8.7 Apocalypse 7.9 1 Rois 4.20 Esaïe 2.2-2.3
17 Jina lake na lidumu milele, Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao; Mataifa yote na wajibariki katika yeye, Na kumwita heri. Genèse 12.3 Genèse 22.18 Psaumes 89.36 Luc 1.48 Esaïe 7.14
18 Na ahimidiwe Bwana, Mungu, Mungu wa Israeli, Atendaye miujiza Yeye peke yake; Psaumes 41.13 Psaumes 136.4 1 Chroniques 29.10 Psaumes 86.10 Exode 15.11
19 Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina. Nombres 14.21 Néhémie 9.5 Psaumes 41.13 Zacharie 14.9 Habakuk 2.14
20 Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamekwisha. 2 Samuel 23.1 Jérémie 51.64 Luc 24.51 Job 31.40

Cette Bible est dans le domaine public.