Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Exode 22
Bible en Swahili de l’est


1 Mtu akiiba ng’ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng’ombe watano badala ya ng’ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. 2 Samuel 12.6 Luc 19.8 Proverbes 6.31 Nombres 5.7 Lévitique 6.1-6.6
2 Mwivi akipatikana akiwa yu hali ya kuvunja mahali, naye akapigwa hata akafa, hapatakuwa na malipizo ya damu kwa ajili yake. Matthieu 24.43 Nombres 35.27 Matthieu 6.19-6.20 1 Thessaloniciens 5.2 Joël 2.9
3 Lakini kama jua limekucha juu yake, ndipo patakuwa na malipizo ya damu kwa ajili yake; ingempasa kutoa malipo kamili; akiwa hana kitu, na auzwe kwa ajili ya wivi wake. Exode 21.2 Juges 10.7 Matthieu 18.25 Esaïe 50.1 Juges 2.14
4 Kama hicho kitu kilichoibwa chapatikana hai mkononi mwake, kama ni ng’ombe, au punda, au kondoo; atalipa thamani yake mara mbili. Exode 22.9 Exode 21.16 Exode 22.7 Exode 22.1 Proverbes 6.31
5 Mtu akilisha katika shamba, au shamba la mizabibu, akimwacha mnyama wake, akala katika shamba la mtu mwingine; atalipa katika vitu vilivyo vizuri vya shamba lake mwenyewe, au vya mizabibu yake. Job 20.18 Exode 22.3 Exode 22.12 Exode 21.34
6 Ukiwaka moto, na kushika penye miiba, na ngano zilizofungwa miganda, au ngano ambazo hazijakatwa, au shamba, likateketea; yeye aliyeuwasha huo moto lazima atalipa. Exode 22.9 Exode 21.33-21.34 Juges 15.4-15.5 Exode 22.12 2 Samuel 14.30-14.31
7 Mtu akimpa mwenziwe amana ya fedha au vitu vingine amtunzie, na vitu vile vikaibwa katika nyumba ya mtu huyo; mwivi akipatikana, atalipa thamani yake mara mbili. 1 Corinthiens 6.10 Jérémie 2.26 Jean 12.6 Proverbes 6.30-6.31 Exode 22.4
8 Mwivi asipopatikana, ndipo mwenye nyumba atakaribia mbele ya Mungu, ionekane kwamba si yeye aliyetia mkono na kutwaa vyombo vya mwenziwe. Exode 22.28 Deutéronome 16.18 Exode 21.6 Exode 22.9 Psaumes 82.1
9 Kila jambo la kukosana, kama ni la ng’ombe, au la punda, au la kondoo, au la mavazi, au la kitu cho chote kilichopotea, ambacho mtu mmoja asema ni chake, hilo jambo la watu wote wawili litaletwa mbele ya Mungu; na yeye atakayehukumiwa na Mungu kuwa ni mkosa atamlipa mwenziwe thamani yake mara mbili. Deutéronome 25.1 Exode 22.28 Nombres 5.6-5.7 Exode 22.4 Exode 23.6-23.8
10 Mtu akimpa mwenziwe punda, au ng’ombe, au kondoo, au mnyama ye yote, ili amtunzie; yule mnyama akafa, au akaumia, au akachukuliwa mtu asione; Genèse 39.8 Luc 16.11 Luc 12.48 2 Timothée 1.12
11 patakuwa na kiapo cha Bwana katikati ya watu hao wawili, kwamba alipeleka mkono wake kutwaa mali ya mwenziwe, na mwenyewe atakubali hayo, wala hatalipa. Hébreux 6.16 1 Rois 2.42-2.43 Exode 23.1 Exode 22.8 Lévitique 6.3
12 Lakini kwamba aliibiwa mnyama huyo, sharti amlipe yule mwenyewe. Genèse 31.39 Exode 22.7
13 Kwamba aliraruliwa na mnyama mkali, na amlete uwe ushahidi; hatalipa kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa. Michée 5.8 Nahum 2.12 Amos 3.12 Ezéchiel 4.14
14 Mtu akiazima mnyama kwa mwenziwe, naye akaumia huyo mnyama, au akafa, mwenyewe asipokuwapo, lazima atalipa. Exode 21.34 Néhémie 5.4 Deutéronome 15.2 Lévitique 24.18 Luc 6.35
15 Kama huyo mwenyewe alikuwapo pamoja na mnyama wake, hatalipa; kama ni mnyama aliyeajiriwa, alikwenda kwa ajili ya ujira wake. Zacharie 8.10
16 Mtu akimshawishi mwanamwali, aliyeposwa na mume, na kulala naye, lazima atatoa mahari kwa ajili yake ili awe mkewe. Deutéronome 22.28-22.29 Genèse 34.2-34.4
17 Ikiwa baba yake huyo mwanamwali akataa kabisa kumpa, atalipa fedha kama hesabu ya mahari ya mwanamwali ilivyo. Genèse 34.12 1 Samuel 18.25 Deutéronome 22.29 Deutéronome 7.3-7.4 Genèse 23.16
18 Usimwache mwanamke mchawi kuishi. 1 Samuel 28.3 Lévitique 20.27 Lévitique 19.31 Deutéronome 18.10-18.11 1 Samuel 28.9
19 Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa. Lévitique 18.23 Deutéronome 27.21 Lévitique 20.15-20.16 Lévitique 18.25
20 Mtu atakayemchinjia sadaka mungu ye yote, isipokuwa ni yeye Bwana peke yake, na angamizwe kabisa. Nombres 25.7-25.8 Deutéronome 18.20 Deutéronome 17.2-17.5 Deutéronome 13.1-13.15 Josué 23.15-23.16
21 Usimwonee mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. Deutéronome 10.19 Exode 23.9 Lévitique 19.33 Zacharie 7.10 Lévitique 25.35
22 Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima. Deutéronome 24.17 Ezéchiel 22.7 Esaïe 1.17 Deutéronome 27.19 Esaïe 1.23
23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao, Luc 18.7 Job 34.28 Jacques 5.4 Psaumes 18.6 Deutéronome 15.9
24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima. Psaumes 109.9 Psaumes 69.24 Lamentations 5.3 Nahum 1.6 Psaumes 90.11
25 Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida. Psaumes 15.5 Lévitique 25.35-25.37 Ezéchiel 18.8 Deutéronome 23.19-23.20 Proverbes 28.8
26 Ikiwa wewe kwa njia yo yote wapokea nguo ya jirani yako rehani, lazima utamrudishia mbele ya jua kuchwa; Amos 2.8 Proverbes 20.16 Deutéronome 24.6 Ezéchiel 18.7 Deutéronome 24.10-24.13
27 maana hiyo nguo ni kifuniko chake, hiyo peke yake ni nguo ya ngozi yake; je! Atalalia nini? Itakuwa, hapo atakaponililia mimi, nitasikia; kwa kuwa mimi ni mwenye rehema. Exode 34.6 2 Chroniques 30.9 Psaumes 72.12 Psaumes 136.10-136.11 Psaumes 34.6
28 Usimtukane Mungu, wala usimlaani mkuu wa watu wako. Actes 23.5 Ecclésiaste 10.20 Exode 21.17 Jude 1.8 Exode 22.8-22.9
29 Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao waume utanipa mimi. Exode 13.2 Exode 23.19 Exode 23.16 Exode 13.12 Deutéronome 26.2-26.10
30 Nawe utafanya vivyo katika ng’ombe zako, na kondoo zako; utamwacha siku saba pamoja na mama yake; siku ya nane utanipa mimi. Deutéronome 15.19 Lévitique 22.27 Lévitique 12.3 Exode 13.12
31 Nanyi mtakuwa watu watakatifu kwangu mimi; kwa hiyo msiile nyama yo yote iliyoraruliwa huko kondeni na mnyama wa mwitu; mtawatupia mbwa nyama hiyo. Ezéchiel 4.14 Deutéronome 14.21 Lévitique 19.2 Ezéchiel 44.31 Lévitique 22.8

Cette Bible est dans le domaine public.