Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 5.11
Bible en Swahili de l’est


1 Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu;Proverbes 22.17 Proverbes 4.20 Proverbes 2.1 Apocalypse 3.13 Jacques 1.19
2 Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa.Proverbes 15.7 Proverbes 16.23 Psaumes 71.15 Malachie 2.6-2.7 Psaumes 119.13
3 Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;Proverbes 2.16 Psaumes 55.21 Proverbes 6.24 Proverbes 7.5 Proverbes 7.21
4 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili.Ecclésiaste 7.26 Hébreux 4.12 Psaumes 55.21 Proverbes 7.22-7.23 Psaumes 57.4
5 Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu;Proverbes 7.27 Proverbes 2.18-2.19
6 Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari.Proverbes 4.26 Psaumes 16.11 Psaumes 119.59 Proverbes 5.21 Proverbes 6.12-6.13
7 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu.Proverbes 4.1 Proverbes 7.24 Hébreux 12.25 Proverbes 3.21 Proverbes 8.32-8.36
8 Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.Proverbes 7.25 Proverbes 4.15 Matthieu 6.13 Proverbes 6.27-6.28 Ephésiens 5.11
9 Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako;Proverbes 6.29-6.35 Osée 4.13-4.14 Néhémie 13.26 Genèse 38.23-38.26 Juges 16.19-16.21
10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;Proverbes 6.35 Luc 15.30 Proverbes 31.3 Osée 7.9
11 Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;Apocalypse 22.15 Nombres 5.27 1 Corinthiens 5.4-5.5 Romains 6.21 Deutéronome 32.29
12 Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa;Proverbes 12.1 Proverbes 15.5 Proverbes 1.25 Proverbes 1.7 Proverbes 1.22
13 Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha!1 Thessaloniciens 5.12-5.13 1 Thessaloniciens 4.8 Hébreux 13.7 Luc 15.18
14 Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko.Proverbes 13.20 Osée 4.11-4.14 Nombres 25.1-25.6 2 Pierre 2.10-2.18 1 Corinthiens 10.6-10.8
15 Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako.1 Corinthiens 7.2-7.5 Hébreux 13.4 Proverbes 5.18-5.19
16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu?Psaumes 68.26 Psaumes 127.3 Deutéronome 33.28 Juges 12.9 Psaumes 128.3
17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. 18 Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.Ecclésiaste 9.9 Cantique 4.15 Cantique 4.12 Malachie 2.14-2.15
19 Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.Cantique 2.9 Cantique 4.5 Cantique 8.14 Cantique 7.3 Cantique 2.17
20 Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni?Proverbes 6.24 Proverbes 7.5 Proverbes 22.14 Proverbes 23.27-23.28 Proverbes 2.16-2.19
21 Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya Bwana, Na mienendo yake yote huitafakari.Hébreux 4.13 Job 34.21 Job 31.4 Jérémie 16.17 Proverbes 15.3
22 Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.Psaumes 7.15-7.16 Psaumes 9.15 Proverbes 11.5 Ecclésiaste 7.26 Proverbes 11.3
23 Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.Job 4.21 Job 36.12 Proverbes 10.21 Proverbes 14.14 2 Pierre 2.15-2.22

Cette Bible est dans le domaine public.