Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 5
Bible en Swahili de l’est


1 Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, mzisikie akili zangu; Proverbes 22.17 Proverbes 4.20 Proverbes 2.1 Proverbes 4.1 Apocalypse 3.13
2 Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa. Proverbes 15.2 Cantique 4.11 Proverbes 15.7 Proverbes 16.23 Psaumes 71.15
3 Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Proverbes 2.16 Psaumes 55.21 Proverbes 6.24 Proverbes 7.5 Proverbes 7.21
4 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Ecclésiaste 7.26 Hébreux 4.12 Psaumes 55.21 Proverbes 6.24-6.35 Proverbes 7.22-7.23
5 Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; Proverbes 7.27 Proverbes 2.18-2.19
6 Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. Proverbes 4.26 Psaumes 16.11 Psaumes 119.59 Proverbes 5.21 Proverbes 30.20
7 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. Proverbes 4.1 Proverbes 4.21 Proverbes 7.24 Hébreux 12.25 Proverbes 3.21
8 Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. Proverbes 7.25 Proverbes 4.15 Matthieu 6.13 Proverbes 6.27-6.28 Ephésiens 5.11
9 Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; Genèse 38.23-38.26 Juges 16.19-16.21 Proverbes 6.29-6.35 Osée 4.13-4.14 Néhémie 13.26
10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni; Osée 7.9 Proverbes 6.35 Luc 15.30 Proverbes 31.3
11 Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia; Apocalypse 22.15 Apocalypse 21.8 Jérémie 5.31 Nombres 5.27 1 Corinthiens 5.4-5.5
12 Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa; Proverbes 12.1 Proverbes 1.22 Proverbes 15.5 Proverbes 1.25 Proverbes 1.7
13 Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha! Luc 15.18 1 Thessaloniciens 5.12-5.13 1 Thessaloniciens 4.8 Hébreux 13.7
14 Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko. 1 Corinthiens 10.6-10.8 Proverbes 13.20 Osée 4.11-4.14 Nombres 25.1-25.6 2 Pierre 2.10-2.18
15 Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. 1 Corinthiens 7.2-7.5 Hébreux 13.4 Proverbes 5.18-5.19
16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? Psaumes 68.26 Esaïe 48.21 Genèse 24.60 Psaumes 127.3 Deutéronome 33.28
17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. 18 Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. Ecclésiaste 9.9 Malachie 2.14-2.15 Cantique 4.15 Cantique 4.12
19 Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima. Cantique 2.9 Cantique 4.5 Cantique 7.3 Cantique 8.14 Proverbes 5.15
20 Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni? Proverbes 6.24 Proverbes 7.5 1 Rois 11.1 Proverbes 23.33 Proverbes 22.14
21 Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya Bwana, Na mienendo yake yote huitafakari. Hébreux 4.13 Jérémie 16.17 Proverbes 15.3 Job 34.21 Job 31.4
22 Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake. Psaumes 7.15-7.16 Psaumes 9.15 Galates 6.7-6.8 Osée 4.11-4.14 Proverbes 11.5
23 Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake. Job 4.21 Job 36.12 Proverbes 10.21 Proverbes 14.32 Psaumes 81.12

Cette Bible est dans le domaine public.