Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 7
Bible en Swahili de l’est


1 Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Proverbes 1.8 Apocalypse 1.3 Jean 15.20 Luc 11.28 Jean 14.23
2 Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. Psaumes 17.8 Lévitique 18.5 Esaïe 55.3 Zacharie 2.8 Deutéronome 32.10
3 Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Deutéronome 11.18-11.20 Proverbes 3.3 Esaïe 30.8 Jérémie 31.33 Proverbes 6.21
4 Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke. Proverbes 2.2-2.4 Job 17.14 Proverbes 4.6-4.8 Matthieu 12.49-12.50 Cantique 8.1
5 Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake. Proverbes 2.16 Proverbes 6.24 Proverbes 5.3
6 Maana katika dirisha la nyumba yangu Nalichungulia katika shubaka yake; Juges 5.28 Genèse 26.8 2 Samuel 6.16
7 Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili, Proverbes 6.32 Proverbes 1.22 Proverbes 1.4 Romains 16.18-16.19 Matthieu 15.16
8 Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake, Jude 1.23 Juges 16.1 Proverbes 4.14-4.15 2 Samuel 11.2-11.3 Proverbes 5.8
9 Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani. Job 24.13-24.15 Romains 13.12-13.14 Ephésiens 5.11 Exode 12.6 Genèse 39.11
10 Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo; 1 Timothée 2.9 Genèse 38.14-38.15 2 Rois 9.30 Genèse 3.1 Jérémie 4.30
11 Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake. Proverbes 9.13 Tite 2.5 Proverbes 27.14-27.15 Genèse 18.9 Proverbes 31.10-31.31
12 Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia. Proverbes 23.28 Proverbes 9.14 Apocalypse 18.3 Jérémie 2.20 Jérémie 3.2
13 Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya, Genèse 39.12 Nombres 31.16 Esaïe 50.7 Ezéchiel 2.4 Ezéchiel 2.6
14 Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu; Lévitique 7.11 Proverbes 17.1 Jean 18.28 Proverbes 15.8 1 Rois 21.9-21.10
15 Ndiyo maana nikatoka nikulaki, Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona. 16 Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari. Esaïe 19.9 Ezéchiel 27.7 Apocalypse 2.22 Cantique 1.16 Cantique 3.7-3.10
17 Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini. Psaumes 45.8 Esaïe 57.7-57.9 Cantique 4.13-4.14 Cantique 3.6 Exode 30.23
18 Haya, na tushibe upendo hata asubuhi, Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba. 19 Maana mume wangu hayumo nyumbani, Amekwenda safari ya mbali; Matthieu 20.11 Matthieu 24.48 Luc 12.39 Luc 12.45-12.46 Matthieu 24.43
20 Amechukua mfuko wa fedha mkononi; Atarudi wakati wa mwezi mpevu. 2 Chroniques 2.4
21 Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda. Proverbes 5.3 Psaumes 12.2 Actes 16.15 Juges 16.15-16.17 1 Samuel 28.23
22 Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu; Job 13.27 Actes 14.13 Jérémie 20.2 Actes 16.24
23 Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. Ecclésiaste 9.12 Nombres 25.8-25.9 Proverbes 1.17 Proverbes 9.18
24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. Proverbes 5.7 Proverbes 4.1 1 Jean 2.1 Proverbes 8.32-8.33 1 Corinthiens 4.14-4.15
25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake. Proverbes 5.8 Proverbes 23.31-23.33 Psaumes 119.176 Proverbes 5.23 Matthieu 5.28
26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa. Néhémie 13.26 2 Samuel 12.9-12.11 1 Rois 11.1-11.2 Proverbes 6.33 1 Corinthiens 10.8
27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti. Proverbes 9.18 Proverbes 5.5 Proverbes 2.18-2.19 Apocalypse 22.15 Ecclésiaste 7.26

Cette Bible est dans le domaine public.