Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 23
Bible en Swahili de l’est


1 Ufunuo juu ya Tiro. Toeni sauti za uchungu, enyi merikebu za Tarshishi, kwa maana umeharibika kabisa, hata hapana nyumba, hapana mahali pa kuingia; toka nchi ya Kitimu wamefunuliwa habari. Joël 3.4-3.8 Jérémie 25.22 Genèse 10.4 Esaïe 2.16 Amos 1.9-1.10
2 Tulieni, enyi mkaao kisiwani; wewe ambaye wafanya biashara wa Sidoni, wavukao bahari, walikujaza. Esaïe 47.5 Ezéchiel 28.2 Habakuk 2.20 Ezéchiel 27.8-27.36 Esaïe 41.1
3 Vitu vilivyopandwa, vya Shihori, mavuno ya Nile, yaliyokuja juu ya maji mengi, ndiyo pato lake, naye alikuwa soko la mataifa. Jérémie 2.18 1 Chroniques 13.5 Apocalypse 18.11-18.13 Esaïe 32.20 Esaïe 23.8
4 Tahayari, Ee Sidoni; kwa maana bahari imenena, hiyo ngome ya bahari ilisema, Sikuona utungu, wala sikuzaa, wala sikulea vijana, wala sikulea wanawali. Jérémie 47.3-47.4 Genèse 10.15 Osée 9.11-9.14 Ezéchiel 26.3-26.6 Apocalypse 18.23
5 Habari itakapofika Misri wataona uchungu sana kwa sababu ya habari ya Tiro. Exode 15.14-15.16 Josué 2.9-2.11 Ezéchiel 28.19 Ezéchiel 26.15-26.21 Esaïe 19.16
6 Piteni mpaka Tarshishi, enyi mkaao kisiwani, toeni sauti ya uchungu. Esaïe 23.12 Esaïe 21.15 Esaïe 16.7 Esaïe 23.1-23.2 Esaïe 23.10
7 Je! Huu ndio mji wenu wa furaha, ambao mwanzo wake ulikuwako tangu siku za kale, ambao miguu yake ilimchukua akae mbali sana? Esaïe 22.2 Esaïe 32.13 Ecclésiaste 10.7 Esaïe 47.1-47.2 Josué 19.29
8 Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu taji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia? Ezéchiel 28.12-28.18 Esaïe 10.8 Jérémie 50.44-50.45 Apocalypse 18.8 Deutéronome 29.24-29.28
9 Bwana wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia. Esaïe 13.11 Esaïe 2.11 Job 40.11-40.12 Daniel 4.37 Ephésiens 1.11
10 Pita katika nchi yako, kama Nile, Ee binti wa Tarshishi, hapana tena mshipi wa kukuzuia. Job 12.21 Romains 5.6 1 Samuel 28.20 Aggée 2.22 Psaumes 18.32
11 Amenyosha mkono wake juu ya bahari, amezitikisa falme; Bwana ametoa amri katika habari za Kanaani, kuziangamiza ngome zake. Zacharie 9.3-9.4 Exode 14.21 Jérémie 47.7 Ezéchiel 31.16 Esaïe 25.2
12 Naye akasema, Usizidi kufurahi, ewe bikira uliyeaibishwa, binti wa Sidoni, haya, ondoka, uende hata Kitimu; huko nako hutapata raha. Apocalypse 18.22 Ezéchiel 26.13-26.14 Esaïe 23.1-23.2 Esaïe 47.1 Lamentations 4.15
13 Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha buruji zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu. Esaïe 10.7 Genèse 11.31 Esdras 4.9-4.10 Genèse 10.10-10.11 Ezéchiel 29.18
14 Pigeni yowe, enyi merikebu za Tarshishi; maana ngome yenu imefanywa ukiwa. Esaïe 23.1 Apocalypse 18.11-18.19 Esaïe 23.6 Ezéchiel 27.25-27.30 Esaïe 2.16
15 Basi, itakuwa katika siku ile, Tiro utasahauliwa miaka sabini, kadiri ya siku za mfalme mmoja; hata mwisho wa miaka sabini, Tiro utakuwa kama vile ulivyo wimbo wa kahaba. Jérémie 25.22 Jérémie 29.10 Apocalypse 17.10 Jérémie 27.3-27.7 Daniel 8.21
16 Twaa kinubi, tembea mjini, Ewe kahaba uliyesahauliwa; Piga vizuri, imba nyimbo nyingi, Upate kukumbukwa tena. Proverbes 7.10-7.12 Jérémie 30.14
17 Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, Bwana ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia. Nahum 3.4 Ezéchiel 27.6-27.36 Michée 1.7 Ezéchiel 16.26 Apocalypse 18.9-18.14
18 Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa Bwana, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za Bwana, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari. Psaumes 72.10 Luc 16.9-16.13 2 Chroniques 2.11-2.16 Proverbes 28.8 Proverbes 13.22

Cette Bible est dans le domaine public.