Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jérémie 11
Bible en Swahili de l’est


1 Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, 2 Yasikieni maneno ya maagano haya; ukaseme na watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; Jérémie 11.6 Exode 19.5 2 Chroniques 29.10 2 Chroniques 23.16 2 Rois 11.17
3 ukawaambie, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu asiyeyasikia maneno ya maagano haya, Deutéronome 27.26 Deutéronome 29.19-29.20 Deutéronome 28.15-28.68 Galates 3.10-3.13
4 niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuru ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu; Deutéronome 4.20 Lévitique 26.12 Lévitique 26.3 1 Rois 8.51 Jérémie 24.7
5 ili nipate kukitimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi ijaayo maziwa na asali, kama ilivyo leo hivi. Ndipo nikajibu, nikasema, Amina, Ee Bwana. Psaumes 105.9-105.11 Jérémie 28.6 Deutéronome 7.12-7.13 Exode 13.5 Lévitique 20.24
6 Naye Bwana akaniambia, Hubiri maneno haya yote katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ukisema, Yasikieni maneno ya maagano haya, mkayafanye. Romains 2.13 Jacques 1.22 Jean 13.17 Jérémie 7.2 Jérémie 3.12
7 Kwa maana naliwashuhudia sana baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, hata leo, nikiamka mapema na kuwashuhudia, nikisema, Itiini sauti yangu. 1 Samuel 8.9 2 Chroniques 36.15 Exode 15.26 Deutéronome 8.6 2 Thessaloniciens 3.12
8 Lakini hawakutii, wala kutega masikio yao, bali walikwenda kila mtu katika ushupavu wa moyo wake mbaya; kwa hiyo nimeleta juu yao maneno yote ya maagano haya, niliyowaamuru wayafanye; lakini hawakuyafanya. Jérémie 7.24 Jérémie 7.26 Ezéchiel 20.8 Jérémie 3.17 Jérémie 35.15
9 Naye Bwana akaniambia, Fitina imeonekana katika watu wa Yuda, na katika wenyeji wa Yerusalemu. Osée 6.9 Michée 3.11 Matthieu 26.3-26.4 Jérémie 8.10 Actes 23.12-23.15
10 Wameyarudia maovu ya baba zao, waliokataa kusikia maneno yangu; wamewafuata miungu mingine na kuwatumikia; nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, wameyavunja maagano yangu niliyoyafanya na baba zao. Deutéronome 31.16 Juges 2.17 Ezéchiel 16.59 Juges 2.19 Juges 2.12-2.13
11 Basi, Bwana asema hivi, Tazama, nitaleta mabaya juu yao, ambayo hawataweza kuyakimbia; nao watanililia, walakini sitawasikiliza. Esaïe 1.15 Proverbes 1.28 Ezéchiel 8.18 Michée 3.4 Zacharie 7.13
12 Ndipo miji ya Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, watakwenda na kuwalilia miungu wawafukiziao uvumba; lakini hawatawaokoa hata kidogo wakati wa taabu yao. Deutéronome 32.37 Jérémie 2.28 Juges 10.14 2 Chroniques 28.22 Esaïe 45.20
13 Maana hesabu ya miungu yako, Ee Yuda, ni sawasawa na hesabu ya miji yako; na kama ilivyo hesabu ya njia za Yerusalemu, ndivyo mlivyosimamisha madhabahu za kitu kile cha aibu, madhabahu za kumfukizia Baali uvumba. 2 Rois 23.13 Jérémie 2.28 Jérémie 3.1-3.2 Osée 12.11 Jérémie 3.24
14 Basi, usiwaombee watu hawa, wala usipaze sauti yako, wala kuwaombea dua watu hawa; maana sitawasikia wakati watakaponililia kwa ajili ya taabu yao. Jérémie 7.16 Jérémie 11.11 1 Jean 5.16 Jérémie 14.11 Psaumes 66.18
15 Mpenzi wangu afanya nini nyumbani mwangu, ikiwa amefanya uasherati? Je! Nadhiri zako na nyama takatifu zitakuondolea hatia? Ufanyapo maovu, ndipo uonapo furaha. Proverbes 2.14 Ezéchiel 23.2-23.21 Psaumes 50.16 Jérémie 2.2 Jérémie 12.7
16 Bwana alikuita jina lako, Mzeituni wenye majani mabichi, mzuri, wenye matunda mema; kwa kelele za mshindo mkuu amewasha moto juu yake, na matawi yake yamevunjika. Esaïe 27.11 Psaumes 52.8 Romains 11.17-11.24 Psaumes 80.16 Esaïe 1.30-1.31
17 Kwa maana Bwana wa majeshi, aliyekupanda, ametamka mabaya juu yako, kwa sababu ya maovu ya nyumba ya Israeli, na ya nyumba ya Yuda, waliyoyatenda juu ya nafsi zao wenyewe kwa kunikasirisha, wakimfukizia Baali uvumba. Esaïe 5.2 Jérémie 2.21 Jérémie 12.2 Jérémie 19.15 Jérémie 16.10-16.11
18 Tena Bwana akanijulisha haya, nami nikayajua; ndipo uliponionyesha matendo yao. 1 Samuel 23.11-23.12 2 Rois 6.9-6.10 Jérémie 11.19 2 Rois 6.14-6.20 Ezéchiel 8.6-8.18
19 Lakini mimi nalikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena. Job 28.13 Esaïe 53.7-53.8 Psaumes 83.4 Jérémie 18.18 Jérémie 20.10
20 Lakini, Ee Bwana wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye viuno na moyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu. Psaumes 7.9 Jérémie 20.12 Jérémie 17.10 1 Samuel 16.7 Genèse 18.25
21 Basi, kwa hiyo, Bwana asema hivi, juu ya watu wa Anathothi, watakao uhai wako, wakisema, Hutafanya unabii kwa jina la Bwana, usije ukafa kwa mkono wetu. Jérémie 20.10 Luc 13.33-13.34 Jérémie 12.5-12.6 Amos 2.12 Esaïe 30.10
22 Kwa sababu hiyo Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaadhibu watu hawa; vijana watakufa kwa upanga; wana wao na binti zao watakufa kwa njaa; Jérémie 18.21 2 Chroniques 36.17 Lamentations 2.21 1 Thessaloniciens 2.15-2.16 Jérémie 9.21
23 wala hapatakuwa na mtu atakayesalia kwao; maana nitaleta mabaya juu ya watu wa Anathothi, mwaka wa kujiliwa kwao. Jérémie 23.12 Luc 19.44 Osée 9.7 Michée 7.4 Jérémie 50.27

Cette Bible est dans le domaine public.