Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Thessaloniciens 2
Bible en Swahili de l’est


1 Maana ninyi wenyewe, ndugu, mwakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure; Habakuk 2.13 2 Thessaloniciens 1.10 1 Corinthiens 15.2 1 Corinthiens 15.58 1 Thessaloniciens 1.3-1.10
2 lakini tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filipi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana. Actes 4.13 Actes 16.22-16.24 Actes 17.2-17.9 2 Timothée 1.12 Hébreux 11.36-11.37
3 Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila; 2 Corinthiens 4.2 2 Corinthiens 2.17 2 Corinthiens 7.2 Actes 20.33-20.34 1 Thessaloniciens 2.5-2.6
4 bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu. Galates 1.10 Galates 2.7 Romains 8.27 Colossiens 3.22 Jérémie 32.19
5 Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi. Actes 20.33 Romains 1.9 2 Corinthiens 12.17 1 Timothée 3.8 2 Pierre 2.3
6 Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine tulipokuwa tukiweza kuwalemea kama mitume wa Kristo; Jean 5.41 Philémon 1.8-1.9 Jean 5.44 1 Thessaloniciens 2.9 Galates 1.10
7 bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe. 1 Thessaloniciens 2.11 2 Timothée 2.24-2.25 Esaïe 66.13 Esaïe 49.23 Jacques 3.17
8 Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu. 2 Corinthiens 12.15 1 Jean 3.16 Philippiens 2.17 Romains 1.11-1.12 Hébreux 13.17
9 Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, tukawahubiri hivi Injili ya Mungu. Actes 18.3 2 Corinthiens 11.9 2 Thessaloniciens 3.7-3.9 1 Timothée 4.10 Actes 20.31
10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa; 1 Thessaloniciens 1.5 2 Corinthiens 1.12 Tite 2.7-2.8 2 Timothée 3.10 Actes 20.18
11 vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia; 1 Corinthiens 4.14-4.15 2 Timothée 4.1-4.2 1 Timothée 5.21 1 Thessaloniciens 4.1 1 Thessaloniciens 2.7
12 ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake. Ephésiens 4.1 1 Thessaloniciens 5.24 1 Jean 2.6 1 Pierre 5.10 1 Jean 1.6-1.7
13 Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini. Hébreux 4.12 Romains 10.17 Galates 4.14 1 Pierre 1.23 1 Pierre 1.25
14 Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi; 1 Thessaloniciens 3.4 Hébreux 10.33-10.34 Galates 1.22 2 Thessaloniciens 1.4 2 Corinthiens 8.1-8.2
15 ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote; Matthieu 5.12 Actes 2.23 Actes 7.52 Luc 11.48-11.53 Luc 13.33-13.34
16 huku wakituzuia tusiseme na Mataifa wapate kuokolewa; ili watimize dhambi zao siku zote. Lakini hasira imewafikia hata mwisho. Actes 13.50 Actes 17.13 Actes 14.19 2 Thessaloniciens 2.10 Matthieu 23.32
17 Lakini sisi, ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa kitambo, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu. Colossiens 2.5 1 Corinthiens 5.3 1 Thessaloniciens 3.6 Romains 1.13 Genèse 48.11
18 Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia. Romains 15.22 Romains 1.13 Zacharie 3.1-3.2 Matthieu 4.10 2 Corinthiens 11.12-11.14
19 Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake? Philippiens 4.1 Philippiens 2.16 2 Corinthiens 1.14 1 Thessaloniciens 3.13 1 Jean 2.28
20 Maana ninyi ndinyi utukufu wetu, na furaha yetu. 2 Corinthiens 1.14 Proverbes 17.6 1 Corinthiens 11.7

Cette Bible est dans le domaine public.