Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Juges 14 Bible en Swahili de l’est
1 Samsoni akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. Josué 15.10 Josué 19.43 Genèse 6.2 Genèse 34.1-34.2 Genèse 38.12-38.13 2 Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake, akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi mnipatie, nimwoe. Genèse 34.4 Genèse 21.21 Genèse 38.6 Genèse 24.2-24.3 2 Rois 14.9 3 Ndipo baba yake na mama yake wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa? Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana. Juges 15.18 1 Samuel 17.36 2 Samuel 1.20 1 Samuel 14.6 1 Samuel 31.4 4 Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la Bwana; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli. Josué 11.20 Juges 13.1 Juges 15.11 2 Chroniques 22.7 2 Chroniques 25.20 5 Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia. 6 Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya. Juges 3.10 Juges 13.25 1 Samuel 11.6 Juges 11.29 Juges 16.30 7 Basi akatelemka na kuzungumza na huyo mwanamke; naye akampendeza Samsoni sana. 8 Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akageuka kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali. Genèse 29.21 Matthieu 1.20 9 Akatwaa asali mikononi mwake akaenda mbele, huku akila alipokuwa akienenda, akawafikilia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba. Proverbes 25.15 1 Samuel 14.25-14.30 10 Basi babaye akamtelemkia huyo mwanamke; Samsoni naye akafanya karamu huko; kwa kuwa vijana ndivyo walivyokuwa wakifanya. Apocalypse 19.9 Ecclésiaste 10.19 Genèse 29.22 Esther 1.7-1.22 Jean 2.9 11 Basi ikawa hapo walipomwona, wakamletea wenziwe thelathini, wawe pamoja naye. 1 Samuel 10.23 1 Samuel 16.6 Jean 3.29 Matthieu 9.15 12 Samsoni akawaambia, Mimi nitawategea ninyi kitendawili; kama mwaweza kunionyesha katika hizo siku saba za karamu, na kukitambua, ndipo hapo nitawapa mavazi thelathini ya kitani na mavao mengine thelathini; Ezéchiel 17.2 Genèse 45.22 1 Rois 10.1 2 Rois 5.5 2 Rois 5.22 13 lakini msipoweza kunionyesha ndipo hapo ninyi mtanipa mimi mavazi thelathini ya kitani na mavao mengine thelathini. Basi wakamwambia, Haya, tega kitendawili chako, ili tupate kukisikia. 14 Naye akawaambia, Katika huyo mwenye kula kikatoka chakula, Katika huyo mwenye nguvu ukatoka utamu. Jacques 1.2-1.4 1 Rois 17.6 2 Chroniques 20.25 Romains 8.37 Matthieu 13.11 15 Ikawa kwa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, Mbembeleze mumeo, ili atuonyeshe hicho kitendawili, tusije tukakuteketeza moto wewe na nyumba ya baba yako; je! Mmetuita ili mpate kuichukua mali yetu? Je! Sivyo? Juges 16.5 Juges 15.6 Proverbes 5.3 Michée 7.5 Juges 12.1 16 Basi mkewe Samsoni akalia mbele yake, akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi; wewe umewategea kitendawili hao wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye akamwambia, Angalia, sikumwambia baba yangu wala mama yangu, nami nikuambie wewe? Juges 16.15 Genèse 2.24 17 Naye akalia mbele yake hizo siku saba, wakati ulioendelea karamu yao; basi ikawa siku ya saba akamwambia, kwa sababu alikuwa akimsisitiza sana; naye akawaambia wale wana wa watu wake hicho kitendawili. Juges 16.16 Genèse 3.6 Luc 11.8 Luc 18.4-18.5 Juges 16.13 18 Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa,Ni kitu gani kilicho tamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, kwamba hamkulima na mtamba wangu,Hamngekitambua kitendawili changu. 19 Roho ya Bwana ikamjilia juu yake kwa nguvu, naye akatelemkia Ashkeloni, akapiga watu waume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavao hayo. Hasira zake zikamwaka, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake. 1 Samuel 11.6 Juges 3.10 Juges 13.25 Juges 15.14 Juges 14.6 20 Lakini huyo mke wa Samsoni aliozwa mwenzake, ambaye alikuwa amemtendea kama rafikiye. Juges 15.2 Jean 3.29 Matthieu 26.49-26.50 Psaumes 55.12-55.13 Juges 15.6