Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 48.10
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa, baada ya mambo hayo, Yusufu akaambiwa, Tazama, baba yako hawezi; akawatwaa wanawe wawili, Manase na Efraimu, pamoja naye.Genèse 46.20 Jean 11.3 Psaumes 128.6 Job 42.16 Genèse 41.50-41.52
2 Naye akaarifiwa Yakobo ya kwamba, Angalia, mwanao Yusufu anakuja kwako. Israeli akajitia nguvu, akaketi juu ya kitanda.Psaumes 41.3 Deutéronome 3.28 1 Samuel 23.16 Proverbes 23.15 Ephésiens 6.10
3 Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki,Genèse 17.1 Exode 6.3 Genèse 35.9-35.12 Genèse 35.6-35.7 Genèse 28.3
4 akaniambia, Mimi hapa, nitakuongezea uzao wako, na kukuzidisha, nami nitakufanya uwe kundi la mataifa; kisha nitawapa wazao wako nchi hii baada yako, iwe milki ya milele.Genèse 17.8 Genèse 35.11 Genèse 12.2 Amos 9.14-9.15 Genèse 13.15-13.16
5 Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.Genèse 41.50-41.52 Josué 14.4 Genèse 46.20 1 Chroniques 5.1-5.2 Josué 13.7
6 Na wazao wako utakaozaa baada ya hawa watakuwa wako; kwa jina la ndugu zao wataitwa katika urithi wao.Josué 14.4
7 Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrathi. Nikamzika katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu.Genèse 35.16-35.19 Genèse 35.9 Genèse 25.20 Michée 5.2 Ruth 1.2
8 Israeli akawaona wana wa Yusufu, akasema, Ni nani hawa? 9 Yusufu akamwambia babaye, Hawa ni wanangu, Mungu alionipa hapa. Akasema, Tafadhali uwalete kwangu nami nitawabariki.Genèse 27.4 Genèse 33.5 Hébreux 11.21 Genèse 27.28-27.29 Esaïe 56.3-56.5
10 Na macho ya Israeli yalikuwa mazito kwa uzee, wala hakuweza kuona. Akawaleta kwake, naye akawabusu, na kuwakumbatia.Genèse 27.27 Genèse 27.1 1 Samuel 3.2 Esaïe 59.1 Genèse 31.55
11 Israeli akamwambia Yusufu, Sikudhani ya kwamba nitakuona uso wako, na Mungu amenionyesha na uzao wako pia.Genèse 37.33 Genèse 45.26 Ephésiens 3.20 Genèse 37.35 Genèse 42.36
12 Yusufu akawatoa katika magoti yake, naye akainama kifudifudiGenèse 42.6 Genèse 18.2 Proverbes 31.28 Ephésiens 6.1 Exode 34.8
13 Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kuume, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kuume wa Israeli, akawasogeza karibu naye. 14 Israeli akanyosha mkono wake wa kuume akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.Genèse 41.51 Genèse 48.18 Matthieu 16.18 Nombres 8.18 1 Timothée 4.14
15 Akambariki Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Ibrahimu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo,Genèse 17.1 Hébreux 11.21 Matthieu 6.25-6.34 2 Corinthiens 1.12 Deutéronome 33.1
16 naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.Psaumes 34.22 Amos 9.12 Psaumes 121.7 Genèse 49.22 Esaïe 63.9
17 Yusufu alipoona kwamba babaye anaweka mkono wake wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, ikawa vibaya machoni pake. Akauinua mkono wa babaye auondoe katika kichwa cha Efraimu, ili auweke juu ya kichwa cha Manase.Genèse 48.14 1 Rois 16.25 1 Samuel 16.7 Genèse 28.8 Romains 9.11
18 Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake.Exode 10.11 Genèse 19.18 Actes 10.14 Matthieu 25.9 Genèse 29.26
19 Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa.Deutéronome 33.17 Apocalypse 7.8 Esaïe 7.17 Genèse 48.14 Apocalypse 7.6
20 Akawabariki siku ile akasema, Katika ninyi Waisraeli watabariki, wakisema, Mungu na akufanye kama Efraimu na Manase. Akamweka Efraimu mbele ya Manase.Ruth 4.11-4.12 Genèse 24.60 Nombres 2.18-2.21 Nombres 13.8 Nombres 13.16
21 Israeli akamwambia Yusufu, Angalia, mimi ninakufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, naye atawarudisha mpaka nchi ya baba zenu.Genèse 46.4 Genèse 50.24 Genèse 26.3 Genèse 28.15 Deutéronome 31.8
22 Nami nimekupa wewe sehemu moja zaidi kuliko ndugu zako, niliyoitwaa katika mikono ya Waamori, kwa upanga wangu na upinde wangu.Jean 4.5 Josué 24.32 Ezéchiel 47.13 Genèse 33.19 Juges 11.23

Cette Bible est dans le domaine public.