Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Samuel 16.22
Bible en Swahili de l’est


1 Naye Daudi alipokipita punde hicho kilele cha mlima, tazama, Siba, mtumwa wa Mefiboshethi, akamkuta, na punda wawili waliotandikwa, na juu yao mikate mia mbili ya ngano, na vishada mia vya zabibu kavu, na matunda mia ya wakati wa hari, na kiriba cha divai.1 Samuel 25.18 2 Samuel 15.32 2 Samuel 9.2-9.13 2 Samuel 15.30 2 Samuel 19.32
2 Mfalme akamwambia Siba, Ni za nini hizi? Siba akasema, Punda ni za jamaa ya mfalme wazipande; na mkate na matunda ni chakula cha hawa vijana; na divai ni kwamba wanywe hao wazimiao nyikani.2 Samuel 17.29 Juges 10.4 Juges 5.10 Proverbes 31.6-31.7 1 Samuel 14.28
3 Mfalme akasema, Na mwana wa bwana wako yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Angalia, anakaa Yerusalemu; kwani alisema, Leo nyumba ya Israeli watanirudishia ufalme wa baba yangu.2 Samuel 9.9-9.10 Psaumes 101.5 Psaumes 15.3 Exode 20.16 Proverbes 21.28
4 Ndipo mfalme akamwambia Siba, Tazama, yote yaliyokuwa ni mali ya Mefiboshethi ni yako. Siba akasema, Mimi nasujudu; na nione kibali machoni pako, Ee bwana wangu, mfalme.Proverbes 18.13 Proverbes 18.17 Exode 23.8 2 Samuel 14.4 2 Samuel 14.10-14.11
5 Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; alitoka, akalaani alipokuwa akienda.2 Samuel 3.16 Exode 22.28 1 Rois 2.8-2.9 2 Samuel 17.18 1 Samuel 17.43
6 Tena akamtupia Daudi mawe, na watumishi wote wa mfalme Daudi; na watu wote na mashujaa wote walikuwako mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto. 7 Na Shimei alipolaani, alisema hivi, Nenda zako! Nenda zako! Ewe mtu wa damu! Ewe mtu usiyefaa!Psaumes 5.6 Psaumes 51.14 Deutéronome 13.13 1 Samuel 25.17 2 Samuel 12.9
8 Bwana amerudisha juu yako damu yote ya nyumba ya Sauli ambaye umetawala badala yake; naye Bwana ametia ufalme katika mkono wa Absalomu mwanao; kisha, angalia, wewe umetwaliwa katika uovu wako mwenyewe, kwa sababu umekuwa mtu wa damu.2 Samuel 1.16 2 Samuel 3.28-3.29 Juges 9.24 1 Rois 2.32-2.33 Juges 9.56-9.57
9 Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, Mbona mbwa mfu huyu amlaani mfalme bwana wangu? Na nivuke, nakusihi, nikaondoe kichwa chake.Exode 22.28 2 Samuel 9.8 2 Samuel 3.8 1 Samuel 24.14 Jérémie 40.13-40.16
10 Mfalme akasema, Nina nini na ninyi, enyi wana wa Seruya? Kwa sababu yeye analaani, na kwa sababu Bwana amemwambia, Mlaani Daudi, basi, ni nani atakayesema, Mbona umetenda haya?2 Samuel 19.22 Romains 9.20 2 Samuel 3.39 Jean 18.11 1 Pierre 2.23
11 Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; si zaidi Mbenyamini huyu sasa? Mwacheni alaani, kwa sababu Bwana ndiye aliyemwagiza.2 Chroniques 32.21 Genèse 15.4 2 Rois 19.37 Genèse 45.5 2 Samuel 7.2
12 Labda Bwana atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye Bwana atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.Romains 8.28 Deutéronome 23.5 Hébreux 12.10 Psaumes 25.18 Exode 2.24-2.25
13 Basi wakaendelea njiani Daudi na watu wake; Shimei naye akaaendelea juu ya ubavu wa kile kilima, kwa kumkabili, huku akiendelea, akilaani, akimtupia mawe, na kurusha mavumbi.Actes 23.23 2 Samuel 16.5-16.6
14 Naye mfalme na watu wake wote waliokuwa pamoja naye wakafika, wamechoka sana; naye akajiburudisha huko. 15 Absalomu, na hao watu wote wa Israeli, wakafika Yerusalemu, naye Ahithofeli alikuwa pamoja naye.2 Samuel 15.37 2 Samuel 15.12
16 Ikawa, Hushai, Mwarki, rafiki wa Daudi, alipomjia Absalomu, Hushai akamwambia Absalomu, Na aishi mfalme, aishi mfalme.2 Rois 11.12 1 Samuel 10.24 1 Rois 1.25 Daniel 6.21 1 Rois 1.34
17 Naye Absalomu akamwambia Hushai, Je! Huu ndio wema wako kwa rafiki yako? Mbona hukutoka pamoja na rafiki yako?2 Samuel 19.25 Proverbes 17.17 2 Samuel 15.32-15.37 Proverbes 18.24 Deutéronome 32.6
18 Hushai akamwambia Absalomu, La, sivyo; lakini yule Bwana aliyemchagua, na watu hawa, na watu wote wa Israeli, mimi nitakuwa wake, na pamoja naye nitakaa.1 Samuel 16.13 2 Samuel 5.1-5.3
19 Na tena, Ni nani ambaye yanipasa nimtumikie? Hainipasi kutumika mbele ya mwanawe? Kama nilivyotumika mbele ya baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mbele yako.2 Samuel 15.34 1 Samuel 29.8 1 Samuel 28.2 Galates 2.13 Psaumes 55.21
20 Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, Haya, toa shauri lako, tufanyeje.Psaumes 2.2 Esaïe 29.15 Psaumes 37.12-37.13 Esaïe 8.10 Exode 1.10
21 Naye Ahithofeli akamwambia Absalomu, Ingia wewe kwa masuria ya baba yako, hao aliowaacha ili kutunza nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako; ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe.2 Samuel 15.16 2 Samuel 20.3 Zacharie 8.13 2 Samuel 2.7 1 Rois 2.17
22 Basi wakamtandikia Absalomu hema juu ya nyumba darini; naye Absalomu akaingia kwa masuria ya babaye machoni pa Israeli wote.2 Samuel 12.11-12.12 2 Samuel 15.16 2 Samuel 20.3 Nombres 25.6 Jérémie 8.12
23 Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.2 Samuel 15.12 2 Samuel 17.14 2 Samuel 17.23 1 Pierre 4.11 Jérémie 8.9

Cette Bible est dans le domaine public.