Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Rois 13.13
Bible en Swahili de l’est


1 Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Yoashi mwana wa Ahazia, mfalme wa Yuda, Yehoahazi mwana wa Yehu alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka kumi na saba.2 Rois 10.35-10.36 2 Rois 11.21 2 Rois 8.26 2 Rois 11.4
2 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, akayafuata makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli; wala hakuyaacha.1 Rois 12.26-12.33 1 Rois 14.16 Osée 5.11 2 Rois 13.11 2 Rois 10.29
3 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, akawatia mkononi mwa Hazaeli mfalme wa Shamu, na mkononi mwa Ben-hadadi mwana wa Hazaeli, siku zote.Juges 2.14 1 Rois 19.17 2 Rois 13.24-13.25 2 Rois 12.17 2 Rois 13.22
4 Naye Yehoahazi akamsihi Bwana, Bwana akamsikiliza; kwa kuwa aliyaona mateso ya Israeli, jinsi mfalme wa Shamu alivyowatesa.2 Rois 14.26 Exode 3.7 Psaumes 78.34 Exode 3.9 Nombres 21.7
5 (Bwana akawapa Israeli mwokozi, nao wakatoka mikononi mwa Washami; wana wa Israeli wakakaa hemani mwao kama zamani za kwanza.Néhémie 9.27 2 Rois 14.27 2 Rois 14.25 2 Rois 13.25 Luc 2.11
6 Lakini hawakuyaacha makosa ya nyumba ya Yeroboamu, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli, lakini wakaendelea katika hayo; nayo ile Ashera ikakaa vivyo katika Samaria).1 Rois 16.33 2 Rois 13.2 2 Rois 17.16 2 Rois 10.29 Deutéronome 7.5
7 Kwa kuwa hakumwachia Yehoahazi watu ila wapandao farasi hamsini, na magari kumi, na askari elfu kumi waendao kwa miguu; kwa kuwa mfalme wa Shamu aliwaharibu, akawaponda mfano wa mavumbi yaliyokanyagwa.Amos 1.3 2 Rois 10.32 1 Samuel 13.15 1 Rois 20.15 Esaïe 36.8
8 Basi mambo yote ya Yehoahazi yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?1 Rois 14.19-14.20 1 Rois 14.29 1 Rois 11.4 1 Rois 14.31 2 Rois 10.34-10.35
9 Yehoahazi akalala na babaze; wakamzika katika Samaria. Na Yehoashi mwanawe akatawala mahali pake.2 Rois 13.13 2 Rois 10.35 2 Rois 13.10 2 Rois 14.8 1 Rois 14.13
10 Katika mwaka wa thelathini na saba wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yehoashi mwana wa Yehoahazi alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria, akatawala miaka kumi na sita. 11 Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli; lakini akaendelea katika hayo.2 Rois 13.2 2 Rois 3.3 2 Rois 13.6 2 Rois 10.29
12 Basi mambo yote ya Yehoashi yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake aliopigania na Amazia mfalme wa Yuda, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?2 Rois 13.14-13.25 2 Rois 14.25 2 Chroniques 25.17-25.24 2 Rois 14.8-14.16
13 Yehoashi akalala na babaze; na Yeroboamu akakaa katika kiti chake cha enzi; naye Yehoashi akazikwa huko Samaria, pamoja na wafalme wa Israeli.2 Rois 14.28-14.29 2 Samuel 7.12 1 Rois 2.10 1 Rois 11.31 1 Rois 1.21
14 Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!2 Rois 2.12 Proverbes 11.11 Genèse 48.1 Ezéchiel 14.14 Zacharie 1.5
15 Elisha akamwambia, Twaa uta na mishale; naye akatwaa uta na mishale. 16 Akamwambia mfalme wa Israeli, Weka mkono wako katika uta; naye akaweka mkono wake juu yake. Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme.2 Rois 4.34 Genèse 49.24 Psaumes 144.1
17 Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa Bwana wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza.1 Rois 20.26 1 Corinthiens 1.18 2 Samuel 5.24 Jean 2.5-2.8 Jean 11.39-11.41
18 Akasema, Itwae mishale; akaitwaa. Akamwambia mfalme wa Israeli, Piga chini; akaipiga nchi mara tatu, akaacha.Ezéchiel 4.1-4.10 Esaïe 20.2-20.4 Exode 17.11 Ezéchiel 5.1-5.4 2 Rois 4.6
19 Yule mtu wa Mungu akamkasirikia, akasema, Ingalikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.2 Rois 13.25 2 Rois 6.9 Lévitique 10.16 Marc 10.14 2 Rois 4.40
20 Elisha akafa, nao wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa mwaka.2 Rois 24.2 2 Rois 3.7 Juges 6.3-6.6 2 Rois 5.2 2 Rois 3.5
21 Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.Ezéchiel 37.1-37.10 Matthieu 27.52-27.53 Actes 19.12 Jean 5.25 2 Rois 4.35
22 Na Hazaeli mfalme wa Shamu akawaonea Israeli siku zote za Yehoahazi.2 Rois 8.12 2 Rois 13.3-13.7 Psaumes 106.40-106.42
23 Lakini Bwana akawahurumia, akawasikitikia, na kuwaangalia, kwa ajili ya agano lake na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, wala hakutaka kuwaangamiza, wala hakuwatupa usoni pake bado.2 Rois 14.27 Genèse 13.16-13.17 Genèse 17.2-17.5 Exode 2.24-2.25 1 Rois 8.28
24 Akafa Hazaeli mfalme wa Shamu, na Ben-hadadi mwanawe akatawala mahali pake.Psaumes 125.3 Luc 18.7
25 Naye Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, akaitwaa tena mkononi mwa Ben-hadadi mwana wa Hazaeli miji ile aliyoitwaa yeye mkononi mwa Yehoahazi baba yake vitani. Mara tatu Yehoashi akamshinda, akairudisha miji ya Israeli.2 Rois 13.18-13.19 2 Rois 10.32 2 Rois 14.25

Cette Bible est dans le domaine public.