Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Chroniques 12.4
Bible en Swahili de l’est


1 Basi hawa ndio wale waliomjia Daudi huko Siklagi, alipokuwa akijificha kwa ajili ya Sauli, mwana wa Kishi; nao walikuwamo miongoni mwa wale mashujaa, waliomsaidia vitani.1 Samuel 27.2-27.6 2 Samuel 1.1 1 Chroniques 11.24-11.25 1 Chroniques 9.39 1 Chroniques 11.10
2 Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kuume na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini.Juges 20.16 Juges 3.15 1 Chroniques 12.29 1 Samuel 17.49
3 Mkubwa wao alikuwa Ahiezeri, kisha Yoashi, wana wa Shemaa Mgibeathi; na Yezieli, na Peleti, wana wa Azmawethi; na Beraka, na Yehu Mwanathothi;1 Chroniques 11.28 1 Samuel 11.4 1 Chroniques 11.33 2 Samuel 21.6
4 na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi;Josué 15.36 Josué 9.3 1 Chroniques 11.15 Josué 9.17-9.23
5 Eluzai, na Yerimothi, na Bealia, na Shemaria, na Shefatia Mharufi; 6 Elkana, na Ishia, na Azaleli, na Yoezeri, na Yashobeamu, Wakora; 7 na Yoela, na Zebadia, wana wa Yerohamu, wa Gedori.Josué 15.58 1 Chroniques 4.39 1 Chroniques 4.18
8 Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;2 Samuel 2.18 2 Samuel 17.10 Jérémie 46.9 Cantique 8.14 2 Samuel 1.23
9 Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu; 10 Mishmana wa nne, Yeremia wa tano; 11 Atai wa sita, Elieli wa saba; 12 Yohana wa nane, Elzabadi wa kenda; 13 Yeremia wa kumi, Makbanai wa kumi na moja. 14 Hao wa wana wa Gadi walikuwa maakida wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia, na yeye aliyekuwa mkuu, na elfu.Deutéronome 32.30 Lévitique 26.8
15 Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.Josué 3.15 Josué 4.18 Jérémie 49.19 Jérémie 12.5
16 Tena wakafika ngomeni kwa Daudi baadhi ya wana wa Benyamini na Yuda. 17 Naye Daudi akatoka ili kuwalaki, akajibu, akawaambia, Kama mmenijia kwa amani ili kunisaidia, basi moyo wangu utaambatana nanyi; lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu, kwa kuwa hamna udhalimu mikononi mwangu, Mungu wa baba zetu na alitazame neno hili, na kulikemea.2 Rois 10.15 Jérémie 32.39 2 Rois 9.22 2 Samuel 3.20-3.25 1 Samuel 18.1
18 Ndipo roho ikamjilia Abishai, mkuu wa wale thelathini, naye akasema, Sisi tu watu wako, Ee Daudi; Na wa upande wako, Ee mwana wa Yese; Amani, naam, amani iwe kwako, Na amani iwe kwao wakusaidiao; Maana akusaidiye ndiye Mungu wako. Ndipo Daudi akawakaribisha, akawaweka wawe maakida wa kile kikosi.Juges 6.34 2 Samuel 17.25 Juges 3.10 Galates 6.16 2 Rois 9.32
19 Wa Manase pia wengine walimwangukia Daudi, alipokwenda pamoja na Wafilisti juu ya Sauli vitani, lakini hawakuwasaidia; kwani wale mabwana wa Wafilisti wakafanya shauri, wakamfukuza, wakisema, kwa hatari ya vichwa vyetu atamwangukia bwana wake Sauli.1 Samuel 29.2-29.9
20 Naye alipokuwa akienda Siklagi, wakamwangukia hawa wa Manase, Adna, na Yozabadi, na Yediaeli, na Mikaeli, na Yozabadi, na Elihu, na Silethai, maakida wa maelfu waliokuwa wa Manase.Exode 18.21 Deutéronome 1.15 Deutéronome 33.17 1 Samuel 29.11
21 Wakamsaidia Daudi juu ya kile kikosi kilichomshambulia; kwani walikuwa waume mashujaa wote, nao wakawa maakida jeshini.1 Chroniques 11.21-11.22 1 Chroniques 12.20 1 Chroniques 5.24 1 Chroniques 11.10 1 Samuel 30.1-30.17
22 Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.Josué 5.14 Genèse 32.2 Job 17.9 Psaumes 148.2 2 Samuel 3.1
23 Na hizi ni hesabu za vichwa vya watu wenye silaha za vita, waliokuja Hebroni kwa Daudi, ili kumgeuzia ufalme wa Sauli, sawasawa na neno la Bwana.2 Samuel 2.3-2.4 1 Chroniques 11.10 1 Samuel 16.1 1 Samuel 16.3 1 Chroniques 10.14-11.3
24 Wana wa Yuda, waliochukua ngao na mkuki, walikuwa elfu sita na mia nane, wenye silaha za vita. 25 Wa wana wa Simeoni, waume mashujaa wa vita, elfu saba na mia moja. 26 Wa wana wa Lawi, elfu nne na mia sita. 27 Na Yehoyada alikuwa kichwa cha mbari ya Haruni, na pamoja naye walikuwa elfu tatu na mia saba;1 Chroniques 6.49-6.57 2 Rois 11.9 1 Chroniques 27.17 1 Chroniques 9.20 2 Rois 11.4
28 tena Sadoki, kijana shujaa, na wa nyumba ya babaye, maakida ishirini na wawili.2 Samuel 8.17 1 Chroniques 6.8 1 Chroniques 6.53 1 Rois 1.8 1 Rois 2.35
29 Na wa wana wa Benyamini nduguze Sauli, elfu tatu; kwani hata sasa walio wengi wao walikuwa wameuhifadhi uaminifu wao kwa nyumba ya Sauli.2 Samuel 2.8-2.9 1 Chroniques 12.2 Genèse 31.23
30 Na wa wana wa Efraimu, ishirini elfu na mia nane, waume mashujaa, watu wenye sifa katika mbari za baba zao.Genèse 6.4
31 Na wa nusu kabila ya Manase, kumi na nane elfu, waliotajwa majina yao, ili waje kumtawaza Daudi awe mfalme.Josué 17.1-17.18
32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.Esther 1.13 Genèse 49.14 Matthieu 16.3 Ephésiens 5.17 Proverbes 14.8
33 Wa Zabuloni, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, wenye zana za vita za kila namna, hamsini elfu; askari wastadi wasiokuwa wenye moyo wa kusita-sita.Psaumes 12.2 Jean 1.47
34 Na wa Naftali, maakida elfu, na pamoja nao watu wenye ngao na mkuki thelathini na saba elfu. 35 Na wa Wadani, watu hodari wa kupanga vita, ishirini na nane elfu na mia sita. 36 Na wa Asheri, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, arobaini elfu.1 Chroniques 12.33 Joël 2.7
37 Tena, ng’ambo ya pili ya Yordani, wa Wareubeni, na wa Wagadi, na wa nusu kabila ya Manase, wenye zana za vita za kupigania za kila namna, mia na ishirini elfu.Josué 13.7-13.32 Deutéronome 3.12-3.16 1 Chroniques 5.1-5.10 Josué 22.1-22.10 Josué 14.3
38 Hao wote, watu wa vita, askari wastadi, wakaja Hebroni wenye moyo mkamilifu, ili kumtawaza Daudi awe mfalme juu ya Israeli wote; tena wote waliosalia wa Israeli nao walikuwa na moyo mmoja kwamba wamtawaze Daudi.1 Rois 8.61 Psaumes 110.3 1 Chroniques 12.33 1 Chroniques 12.17-12.18 Psaumes 101.2
39 Nao walikuwako huko pamoja na Daudi siku tatu, wakila na kunywa; kwani ndugu zao walikuwa wamewaandalia tayari.Genèse 26.30 2 Samuel 19.42 2 Samuel 6.19 Genèse 31.54
40 Zaidi ya hayo, wale waliokuwa karibu nao, hata mpaka kwa Isakari, na Zabuloni, na Naftali, wakaleta chakula juu ya punda, na ngamia, na nyumbu, na ng’ombe, vyakula vya unga, mikate ya tini, na vichala vya zabibu kavu, na divai, na mafuta, na ng’ombe, na kondoo tele; kwa kuwa kulikuwa na furaha katika Israeli.1 Samuel 25.18 2 Samuel 16.1 Apocalypse 19.5-19.7 1 Rois 1.40 2 Samuel 17.27-17.29

Cette Bible est dans le domaine public.