24 Wana wa Yuda, waliochukua ngao na mkuki, walikuwa elfu sita na mia nane, wenye silaha za vita. 25 Wa wana wa Simeoni, waume mashujaa wa vita, elfu saba na mia moja. 26 Wa wana wa Lawi, elfu nne na mia sita. 27 Na Yehoyada alikuwa kichwa cha mbari ya Haruni, na pamoja naye walikuwa elfu tatu na mia saba; 1 Chroniques 6.49-6.57 2 Rois 11.9 1 Chroniques 27.17 1 Chroniques 9.20 2 Rois 11.4 28 tena Sadoki, kijana shujaa, na wa nyumba ya babaye, maakida ishirini na wawili. 2 Samuel 8.17 1 Chroniques 6.8 1 Chroniques 6.53 1 Rois 1.8 1 Rois 2.35 29 Na wa wana wa Benyamini nduguze Sauli, elfu tatu; kwani hata sasa walio wengi wao walikuwa wameuhifadhi uaminifu wao kwa nyumba ya Sauli. 2 Samuel 2.8-2.9 1 Chroniques 12.2 Genèse 31.23 30 Na wa wana wa Efraimu, ishirini elfu na mia nane, waume mashujaa, watu wenye sifa katika mbari za baba zao. Genèse 6.4 31 Na wa nusu kabila ya Manase, kumi na nane elfu, waliotajwa majina yao, ili waje kumtawaza Daudi awe mfalme. Josué 17.1-17.18 32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao. Esther 1.13 Luc 12.56-12.57 Esaïe 22.12-22.14 Ecclésiaste 9.18 Genèse 49.14 33 Wa Zabuloni, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, wenye zana za vita za kila namna, hamsini elfu; askari wastadi wasiokuwa wenye moyo wa kusita-sita. Psaumes 12.2 Jean 1.47 34 Na wa Naftali, maakida elfu, na pamoja nao watu wenye ngao na mkuki thelathini na saba elfu. 35 Na wa Wadani, watu hodari wa kupanga vita, ishirini na nane elfu na mia sita. 36 Na wa Asheri, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, arobaini elfu. 1 Chroniques 12.33 Joël 2.7 37 Tena, ng’ambo ya pili ya Yordani, wa Wareubeni, na wa Wagadi, na wa nusu kabila ya Manase, wenye zana za vita za kupigania za kila namna, mia na ishirini elfu. Josué 13.7-13.32 Deutéronome 3.12-3.16 1 Chroniques 5.1-5.10 Josué 22.1-22.10 Josué 14.3 38 Hao wote, watu wa vita, askari wastadi, wakaja Hebroni wenye moyo mkamilifu, ili kumtawaza Daudi awe mfalme juu ya Israeli wote; tena wote waliosalia wa Israeli nao walikuwa na moyo mmoja kwamba wamtawaze Daudi. 1 Rois 8.61 2 Rois 20.3 2 Chroniques 30.12 Genèse 49.8-49.10 Psaumes 110.3 39 Nao walikuwako huko pamoja na Daudi siku tatu, wakila na kunywa; kwani ndugu zao walikuwa wamewaandalia tayari. Genèse 26.30 2 Samuel 19.42 2 Samuel 6.19 Genèse 31.54 40 Zaidi ya hayo, wale waliokuwa karibu nao, hata mpaka kwa Isakari, na Zabuloni, na Naftali, wakaleta chakula juu ya punda, na ngamia, na nyumbu, na ng’ombe, vyakula vya unga, mikate ya tini, na vichala vya zabibu kavu, na divai, na mafuta, na ng’ombe, na kondoo tele; kwa kuwa kulikuwa na furaha katika Israeli. 1 Samuel 25.18 2 Samuel 16.1 Proverbes 11.10 Proverbes 29.2 Luc 19.37-19.38