Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 80
Bible en Swahili de l’est


1 Wewe uchungaye Israeli, usikie, Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi; Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru. Psaumes 77.20 Psaumes 50.2 1 Samuel 4.4 2 Samuel 6.2 Psaumes 99.1
2 Mbele ya Efraimu, na Benyamini, na Manase, Uziamshe nguvu zako, Uje, utuokoe. Nombres 2.18-2.24 Psaumes 35.23 Esaïe 33.22 Esaïe 42.13-42.14 Nombres 10.22-10.24
3 Ee Mungu, uturudishe, Uangazishe uso wako nasi tutaokoka. Psaumes 85.4 Lamentations 5.21 Psaumes 4.6 Psaumes 80.19 Psaumes 80.7
4 Ee Bwana, Mungu wa majeshi, hata lini Utayaghadhibikia maombi ya watu wako? Psaumes 85.5 Esaïe 58.2-58.3 Lamentations 3.44 Psaumes 74.1 Luc 18.1-18.8
5 Umewalisha mkate wa machozi, Umewanywesha machozi kwa kipimo kikuu. Psaumes 42.3 Esaïe 30.20 Psaumes 102.9 Job 6.7 Ezéchiel 4.16-4.17
6 Unatufanya sababu ya ugomvi kwa jirani zetu, Na adui zetu wanacheka wao kwa wao. Psaumes 79.4 Esaïe 36.8 Jérémie 48.27 Psaumes 44.13-44.14 Ezéchiel 36.4
7 Ee Mungu wa majeshi, uturudishe, Uangazishe uso wako nasi tutaokoka. Psaumes 80.19 Esaïe 64.5 Esaïe 30.15 Psaumes 80.3 Psaumes 51.10
8 Ulileta mzabibu kutoka Misri, Ukawafukuza mataifa ukaupanda. Jérémie 2.21 Psaumes 44.2 Ezéchiel 17.6 Ezéchiel 19.10 Jean 15.1-15.8
9 Ulitengeneza nafasi mbele yake, Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi. Josué 24.12 Exode 23.28-23.30 Néhémie 9.22-9.25 1 Rois 4.20 Esaïe 27.6
10 Milima ilifunikwa kwa uvuli wake, Matawi yake ni kama mierezi ya Mungu. Psaumes 104.16
11 Nao uliyaeneza matawi yake hata baharini, Na vichipukizi vyake hata kunako Mto. Psaumes 72.8 1 Rois 4.21 1 Chroniques 18.3 1 Rois 4.24 Genèse 15.18
12 Kwa nini umezibomoa kuta zake, Wakauchuma wote wapitao njiani? Esaïe 5.5 Luc 20.16 Nahum 2.2 Esaïe 18.5-18.6 Psaumes 89.40-89.41
13 Nguruwe wa msituni wanauharibu, Na hayawani wa kondeni wanautafuna. Jérémie 5.6 2 Chroniques 36.1-36.23 2 Rois 18.1-18.19 Jérémie 4.7 Jérémie 39.1-39.3
14 Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi, Utazame toka juu uone, uujilie mzabibu huu. Esaïe 63.15 Psaumes 90.13 Malachie 3.7 Psaumes 33.13 Joël 2.14
15 Na mche ule ulioupanda Kwa mkono wako wa kuume; Na tawi lile ulilolifanya Kuwa imara kwa nafsi yako. Psaumes 80.8 Ezéchiel 17.22-17.24 Marc 12.1 Zacharie 6.12 Psaumes 89.21
16 Umechomwa moto; umekatwa; Kwa lawama ya uso wako wanapotea. Psaumes 39.11 Psaumes 76.6-76.7 Jean 15.6 2 Thessaloniciens 1.9 Ezéchiel 20.47-20.48
17 Mkono wako na uwe juu yake Mtu wa mkono wako wa kuume; Juu ya mwanadamu uliyemfanya Kuwa imara kwa nafsi yako; Psaumes 89.21 Psaumes 80.15 Daniel 7.13-7.14 Esaïe 53.5 Jean 5.21-5.29
18 Basi hatutakuacha kwa kurudi nyuma; Utuhuishe nasi tutaliitia jina lako. Ephésiens 2.1-2.5 Psaumes 119.107 Cantique 1.4 Philippiens 2.12-2.13 Psaumes 119.37
19 Ee Bwana, Mungu wa majeshi, uturudishe, Uangazishe uso wako nasi tutaokoka. Psaumes 80.3 Psaumes 80.7 Psaumes 27.4 Psaumes 44.3 Psaumes 80.1

Cette Bible est dans le domaine public.