Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 27
Bible en Swahili de l’est


1 Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Jacques 4.13-4.16 Luc 12.19-12.20 Psaumes 95.7 Esaïe 56.12 2 Corinthiens 6.2
2 Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe. Proverbes 25.27 2 Corinthiens 10.18 2 Corinthiens 12.11 2 Corinthiens 10.12
3 Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili. Proverbes 17.12 Daniel 3.19 1 Samuel 22.18-22.19 Esther 3.5-3.6 1 Jean 3.12
4 Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu. Proverbes 6.34 Job 5.2 Jacques 3.14-3.16 Actes 7.9 Proverbes 14.30
5 Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika. Proverbes 28.23 Galates 2.14 1 Timothée 5.20 Matthieu 18.15 Lévitique 19.17
6 Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana. Psaumes 141.5 Job 5.17-5.18 Proverbes 10.18 2 Samuel 20.9-20.10 Proverbes 26.23-26.26
7 Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu. Nombres 21.5 Nombres 11.4-11.9 Nombres 11.18-11.20 Jean 6.9 Job 6.7
8 Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huko na huko mbali na mahali pake. Esaïe 16.2 Proverbes 21.16 1 Samuel 27.1-27.12 Jonas 1.3 Genèse 16.6-16.8
9 Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake. Cantique 4.10 Psaumes 133.2 Proverbes 7.17 2 Corinthiens 2.15-2.16 Proverbes 16.21
10 Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali. Proverbes 18.24 1 Rois 12.6-12.8 Proverbes 17.17 2 Samuel 21.7 Abdias 1.12-1.14
11 Mwanangu, uwe na hekima na kunifurahisha moyo wangu; Ili nipate kumjibu anilaumuye. Proverbes 10.1 Psaumes 119.42 Proverbes 23.15-23.16 Proverbes 29.3 Ecclésiaste 2.18-2.21
12 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. Proverbes 22.3 2 Pierre 3.10-3.14 Proverbes 18.10 Exode 9.20-9.21 2 Pierre 3.7
13 Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni; Mtoza rehani aliye mdhamini wa malaya. Proverbes 20.16 Exode 22.26 Proverbes 6.1-6.4 Proverbes 22.26-22.27
14 Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake. 2 Samuel 15.2-15.7 2 Samuel 16.16-16.19 Actes 12.22-12.23
15 Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa; Proverbes 19.13 Proverbes 21.19 Proverbes 21.9 Job 14.19 Proverbes 25.24
16 Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo; Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta. Jean 12.3
17 Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake. Hébreux 10.24 Job 4.3-4.4 Proverbes 27.9 1 Samuel 23.16 2 Timothée 2.3
18 Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake; Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa. 1 Corinthiens 9.7 Cantique 8.12 Proverbes 22.29 Luc 12.43-12.44 2 Timothée 2.6
19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake. Jacques 1.22-1.25 Genèse 6.5 Psaumes 33.15 Marc 7.21
20 Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi. Ecclésiaste 1.8 Proverbes 30.15-30.16 Habakuk 2.5 Ecclésiaste 2.10-2.11 Ecclésiaste 6.7
21 Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake. Proverbes 17.3 2 Samuel 14.25 Psaumes 12.6 2 Samuel 15.6-15.12 Psaumes 66.10
22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka. Proverbes 23.35 Jérémie 5.3 Esaïe 1.5 Exode 15.9 Jérémie 44.15-44.16
23 Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng’ombe zako. 1 Pierre 5.2 Jean 21.15-21.17 2 Chroniques 26.10 Ezéchiel 34.31 1 Samuel 17.28
24 Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Yadumu tangu kizazi hata kizazi? Proverbes 23.5 Esaïe 9.7 Jacques 1.10 1 Timothée 6.17-6.18 Sophonie 1.18
25 Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana, Na maboga ya milimani hukusanyika. Proverbes 10.5 Psaumes 104.14
26 Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; Na mbuzi ni thamani ya shamba Job 31.20
27 Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, Ya kukutosha kwa chakula chako, Na chakula cha watu wa nyumbani mwako, Na posho la vijakazi vyako. Proverbes 30.8-30.9 Matthieu 6.33

Cette Bible est dans le domaine public.