Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Nombres 29 Bible en Swahili de l’est
Les sacrifices de la fête des trompettes
1 Tena mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; ni siku ya kupiga tarumbeta kwenu. Lévitique 23.24-23.25 Nombres 10.1-10.10 Zacharie 9.14 Marc 16.15-16.16 Psaumes 81.3 2 Nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba; Hébreux 10.10-10.14 Nombres 29.36 Nombres 28.19 Nombres 29.8 Nombres 28.27 3 pamoja na sadaka yake ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa ng’ombe, sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume, 4 na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; 5 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu; Nombres 28.30 Nombres 28.15 Nombres 28.22 6 zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto. Nombres 28.11-28.15 Nombres 28.3-28.8 Exode 29.38-29.42 Nombres 15.11-15.12 Nombres 15.24
Les sacrifices du jour des expiations
7 Tena siku ya kumi ya huo mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; nanyi mtazitesa nafsi zenu, msifanye kazi yo yote ya utumishi Lévitique 16.29-16.31 Psaumes 35.13 Actes 27.9 Esdras 8.21 2 Corinthiens 7.9-7.11 8 lakini mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza; ng’ombe mume mdogo mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu; Nombres 29.13 Nombres 28.19 Nombres 29.2 9 pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa huyo ng’ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa huyo kondoo, Nombres 15.3-15.12 10 na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo saba; 11 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji. Lévitique 16.3 Lévitique 16.5 Daniel 9.24-9.26 Nombres 29.6 Nombres 28.3-28.8
Les sacrifices de la fête des tentes
12 Tena siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi, nanyi mtamfanyia Bwana sikukuu muda wa siku saba; Deutéronome 16.13-16.14 Hébreux 11.9-11.13 Ezéchiel 45.25 Exode 34.22 Lévitique 23.33-23.43 13 nanyi mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka isongezwayo kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe waume wadogo kumi na watatu, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza kumi na wanne; wote watakuwa wakamilifu; Nombres 28.11 Esdras 3.4 Nombres 28.27 Nombres 29.8 Hébreux 10.12-10.14 14 pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng’ombe katika wale kumi na watatu na sehemu ya kumi mbili kwa kila kondoo katika hao kondoo waume wawili; 15 na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo katika wale wana-kondoo kumi na wanne; 16 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji. 17 Tena siku ya pili mtasongeza ng’ombe waume wadogo kumi na wawili, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza kumi na wanne wakamilifu; Osée 6.6 Psaumes 51.16-51.17 Romains 12.1 Nombres 29.13 Esaïe 1.11 18 pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuandama hiyo amri; Nombres 28.7 Nombres 28.14 Nombres 15.4-15.12 Nombres 29.6 Nombres 29.3-29.4 19 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji. Nombres 29.22 Nombres 29.25 Nombres 29.11 Amos 8.14 20 Tena siku ya tatu mtasongeza ng’ombe waume kumi na mmoja, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 21 pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 22 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji. Psaumes 16.4 Joël 1.13 Joël 2.14 Joël 1.9 23 Tena siku ya nne mtasongeza ng’ombe waume kumi, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 24 na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 25 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji. Hébreux 3.14 Galates 2.5 Galates 6.9 2 Thessaloniciens 3.13 Hébreux 13.15 26 Tena siku ya tano mtasongeza ng’ombe waume kenda, na kondoo Waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 27 pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 28 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji. 29 Tena siku ya sita mtasongeza ng’ombe waume wanane, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 30 pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 31 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji. 32 Tena siku ya saba mtasongeza ng’ombe waume saba, na kondoo waume wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu kumi na wanne; 33 pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa hao ng’ombe, na kwa hao kondoo, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 34 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji. 35 Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; Lévitique 23.36 Apocalypse 7.9-7.17 Jean 7.37-7.39 36 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba; 37 pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kwa huyo ng’ombe, na kwa huyo kondoo mume, na kwa wale wana-kondoo, kama hesabu yao ilivyo, kwa kuiandama amri; 38 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, na hiyo sadaka yake ya unga na sadaka yake ya kinywaji. 39 Sadaka hizo mtamsongezea Bwana katika sikukuu zenu zilizoamriwa, zaidi ya nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, kuwa sadaka zenu za kuteketezwa, na sadaka zenu za unga, na sadaka zenu za vinywaji, na sadaka zenu za amani. Lévitique 23.2 1 Chroniques 23.31 2 Chroniques 31.3 Lévitique 7.11 Néhémie 10.33 40 Naye Musa akawaambia wana wa Israeli vile vile kama hayo yote Bwana alivyomwagiza Musa. Actes 20.27 Hébreux 3.2 1 Corinthiens 15.3 Exode 40.16 Matthieu 28.20