Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Corinthiens 12.16
Bible en Swahili de l’est


1 Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana.Galates 2.2 Galates 1.12 2 Corinthiens 12.7 Actes 9.10-9.17 Ephésiens 3.3
2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.2 Corinthiens 11.11 Actes 22.17 1 Thessaloniciens 4.17 Apocalypse 12.5 Romains 16.7
3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.Luc 23.43 Apocalypse 2.7 Ezéchiel 31.9
5 Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu wangu.2 Corinthiens 12.9-12.10 2 Corinthiens 11.30 1 Corinthiens 2.3
6 Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu.2 Corinthiens 11.16 Job 24.25 1 Corinthiens 3.9-3.10 2 Corinthiens 5.13 2 Corinthiens 10.8-10.10
7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.1 Corinthiens 5.5 Daniel 5.20 2 Chroniques 26.16 Nombres 33.55 2 Chroniques 32.25-32.26
8 Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.2 Samuel 12.16-12.18 1 Samuel 15.11 Hébreux 5.7 Psaumes 77.2-77.11 Matthieu 20.21-20.22
9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.2 Corinthiens 12.10 Philippiens 4.13 Ephésiens 3.16 Esaïe 40.29-40.31 1 Corinthiens 10.13
10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.2 Corinthiens 13.4 Romains 5.3 2 Corinthiens 6.4 2 Corinthiens 12.9 Jacques 1.2
11 Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lo lote, nijapokuwa si kitu.2 Corinthiens 11.5 2 Corinthiens 11.1 1 Corinthiens 3.4-3.7 2 Corinthiens 12.6 Galates 2.6-2.14
12 Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika saburi yote, kwa ishara na maajabu na miujiza.Romains 15.18-15.19 1 Corinthiens 1.5-1.7 1 Corinthiens 14.18 2 Corinthiens 11.4 2 Corinthiens 4.2
13 Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, ila kwa kuwa mimi sikuwalemea? Mnisamehe udhalimu huu.1 Corinthiens 9.12 2 Corinthiens 12.14 1 Corinthiens 9.6 1 Corinthiens 9.15-9.18 2 Corinthiens 11.7-11.9
14 Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto.Proverbes 19.14 1 Corinthiens 4.14-4.15 1 Corinthiens 10.33 2 Corinthiens 1.15 Proverbes 13.22
15 Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?1 Thessaloniciens 2.8 Philippiens 2.17 2 Corinthiens 1.6 Colossiens 1.24 2 Timothée 2.10
16 Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila.1 Thessaloniciens 2.3 2 Corinthiens 1.12 2 Corinthiens 7.2 2 Corinthiens 12.13 2 Corinthiens 10.2-10.3
17 Je! Mtu ye yote niliyemtuma kwenu, kwa mtu huyo naliwatoza kitu?1 Corinthiens 4.17 2 Rois 5.16 2 Corinthiens 12.18 2 Corinthiens 9.5 2 Rois 5.20-5.27
18 Nalimwonya Tito, nikamtuma ndugu yule pamoja naye. Je! Tito aliwatoza kitu? Je! Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile?2 Corinthiens 8.6 Romains 4.12 1 Samuel 12.3-12.4 1 Pierre 2.21 2 Corinthiens 7.6
19 Mwadhani hata sasa ya kuwa najidhuru kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.Romains 9.1 2 Corinthiens 10.8 1 Corinthiens 14.26 2 Corinthiens 11.10 2 Corinthiens 13.10
20 Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong’onezo, na majivuno, na ghasia;Romains 1.29 1 Corinthiens 1.11 1 Pierre 2.1 Galates 5.15 2 Corinthiens 12.21
21 nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya.2 Corinthiens 13.2 Galates 5.19 1 Corinthiens 5.1 Colossiens 3.5 Psaumes 119.136

Cette Bible est dans le domaine public.