Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Corinthiens 12.5
Bible en Swahili de l’est


1 Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana.Galates 2.2 Galates 1.12 2 Corinthiens 12.7 1 Corinthiens 6.12 2 Corinthiens 8.10
2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.2 Corinthiens 11.11 Actes 22.17 1 Thessaloniciens 4.17 Apocalypse 12.5 2 Corinthiens 5.17
3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.Luc 23.43 Apocalypse 2.7 Ezéchiel 31.9
5 Kwa habari za mtu kama huyo nitajisifu; lakini kwa ajili ya nafsi yangu sitajisifu, isipokuwa katika habari ya udhaifu wangu.1 Corinthiens 2.3 2 Corinthiens 12.9-12.10 2 Corinthiens 11.30
6 Maana kama ningetaka kujisifu singekuwa mpumbavu, kwa sababu nitasema kweli. Lakini najizuia, ili mtu asinihesabie zaidi ya hayo ayaonayo kwangu au kuyasikia kwangu.2 Corinthiens 11.16 2 Corinthiens 5.13 2 Corinthiens 10.8-10.10 Romains 9.1 2 Corinthiens 1.18
7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.1 Corinthiens 5.5 Daniel 5.20 2 Chroniques 32.25-32.26 Juges 2.3 2 Chroniques 26.16
8 Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.2 Samuel 12.16-12.18 1 Samuel 15.11 Hébreux 5.7 Matthieu 20.21-20.22 Deutéronome 3.23-3.27
9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.2 Corinthiens 12.10 Philippiens 4.13 Ephésiens 3.16 Esaïe 40.29-40.31 1 Corinthiens 10.13
10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.Romains 5.3 2 Corinthiens 13.4 2 Corinthiens 6.4 2 Corinthiens 12.9 Jacques 1.2
11 Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi; kwa sababu sikuwa duni ya mitume walio wakuu kwa lo lote, nijapokuwa si kitu.2 Corinthiens 11.5 2 Corinthiens 11.1 Galates 2.6-2.14 1 Corinthiens 15.8-15.10 1 Corinthiens 3.22
12 Kweli ishara za mtume zilitendwa katikati yenu katika saburi yote, kwa ishara na maajabu na miujiza.Romains 15.18-15.19 1 Corinthiens 14.18 2 Corinthiens 11.4 2 Corinthiens 4.2 2 Corinthiens 11.6
13 Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, ila kwa kuwa mimi sikuwalemea? Mnisamehe udhalimu huu.1 Corinthiens 9.12 1 Corinthiens 9.6 2 Corinthiens 12.14 1 Corinthiens 9.15-9.18 2 Corinthiens 11.7-11.9
14 Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto.Proverbes 19.14 1 Corinthiens 4.14-4.15 1 Corinthiens 10.33 2 Corinthiens 1.15 Proverbes 13.22
15 Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?1 Thessaloniciens 2.8 Philippiens 2.17 2 Corinthiens 1.6 Colossiens 1.24 2 Timothée 2.10
16 Lakini na iwe hivyo, mimi sikuwalemea; bali kwa kuwa mwerevu naliwapata kwa hila.2 Corinthiens 7.2 2 Corinthiens 12.13 2 Corinthiens 10.2-10.3 1 Pierre 2.3 2 Corinthiens 11.9-11.10
17 Je! Mtu ye yote niliyemtuma kwenu, kwa mtu huyo naliwatoza kitu?2 Corinthiens 12.18 2 Corinthiens 9.5 2 Rois 5.20-5.27 1 Corinthiens 16.10 1 Corinthiens 4.17
18 Nalimwonya Tito, nikamtuma ndugu yule pamoja naye. Je! Tito aliwatoza kitu? Je! Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile?2 Corinthiens 8.6 Romains 4.12 2 Corinthiens 7.6 2 Corinthiens 8.16-8.23 Actes 20.33-20.35
19 Mwadhani hata sasa ya kuwa najidhuru kwenu! Mbele za Mungu twanena katika Kristo. Na hayo yote, wapenzi, ni kwa ajili ya kuwajenga ninyi.Romains 9.1 2 Corinthiens 10.8 1 Corinthiens 14.26 2 Corinthiens 13.10 2 Corinthiens 11.31
20 Maana nachelea, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekana kwenu si kama vile mtakavyo; nisije nikakuta labda fitina na wivu, na ghadhabu, na ugomvi, na masingizio, na manong’onezo, na majivuno, na ghasia;Romains 1.29 1 Corinthiens 1.11 1 Pierre 2.1 Galates 5.15 2 Corinthiens 1.23-2.4
21 nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya.2 Corinthiens 13.2 1 Corinthiens 5.1 Colossiens 3.5 Galates 5.19 Apocalypse 22.20

Cette Bible est dans le domaine public.