Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Philippiens 3.1
Bible en Swahili de l’est


1 Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi.Philippiens 4.4 2 Corinthiens 13.11 1 Thessaloniciens 5.16 Philippiens 4.8 1 Pierre 4.13
2 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.2 Corinthiens 11.13 Galates 5.15 Psaumes 22.16 Tite 1.16 Esaïe 56.10-56.11
3 Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.Colossiens 2.11 Romains 2.25-2.29 Deutéronome 30.6 Romains 4.11-4.12 Galates 6.13-6.15
4 Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi.2 Corinthiens 11.18-11.22
5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,2 Corinthiens 11.22 Romains 11.1 Actes 23.6 Actes 22.3 Genèse 17.12
6 kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia.Actes 8.3 Actes 22.3-22.4 Galates 1.13-1.14 Actes 26.9-26.10 2 Samuel 21.2
7 Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.Luc 14.33 Proverbes 13.8 Matthieu 16.26 Proverbes 23.23 Philippiens 3.8-3.10
8 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;2 Pierre 1.3 Jean 17.3 Actes 20.24 Philippiens 3.10 Jérémie 9.23-9.24
9 tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;1 Corinthiens 1.30 Romains 8.1 2 Corinthiens 5.21 Esaïe 53.11 Romains 1.17
10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;Romains 8.17 Romains 6.3-6.11 Philippiens 3.8 2 Timothée 2.11-2.12 Galates 2.20
11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.Apocalypse 20.5 Luc 20.35-20.36 Actes 26.7 Jean 11.24 Actes 23.6
12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.1 Timothée 6.11-6.12 1 Timothée 6.19 Philippiens 3.13-3.14 Osée 6.3 1 Corinthiens 13.10
13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;Luc 9.62 Hébreux 12.1-12.2 Hébreux 6.1 Philippiens 3.12 Philippiens 3.8
14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.1 Corinthiens 9.24 1 Pierre 5.10 Apocalypse 3.21 2 Pierre 1.3 Hébreux 6.1
15 Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo.Galates 5.10 1 Corinthiens 2.6 Proverbes 2.3-2.6 Proverbes 3.5-3.6 Esaïe 35.8
16 Lakini, hapo tulipofika na tuenende katika lilo hilo.Galates 6.16 Apocalypse 3.3 Colossiens 2.6 Apocalypse 2.4-2.5 Romains 12.16
17 Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.Philippiens 4.9 1 Corinthiens 4.16 1 Pierre 5.3 Romains 16.17 1 Thessaloniciens 2.10-2.14
18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;Jérémie 13.17 Ephésiens 4.17 Galates 2.14 Esaïe 8.11 Galates 1.7
19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.Romains 16.18 2 Pierre 2.3 Romains 8.5-8.7 2 Pierre 2.1 2 Corinthiens 11.15
20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;Ephésiens 2.19 Colossiens 3.1-3.3 Hébreux 12.22 2 Corinthiens 4.18-5.1 Ephésiens 2.6
21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.Colossiens 3.4 1 Corinthiens 15.42-15.56 1 Jean 3.2 Romains 8.29 Ephésiens 1.19-1.20

Cette Bible est dans le domaine public.