Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Chroniques 18
Bible en Swahili de l’est


1 Basi, Yehoshafati alikuwa na mali na heshima tele, tena akafanya ujamaa na Ahabu. 2 Chroniques 17.5 2 Chroniques 21.6 2 Chroniques 19.2 2 Rois 8.18 2 Corinthiens 6.14
2 Hata baada ya miaka kadha wa kadha akamshukia Ahabu huko Samaria. Ahabu akamchinjia kondoo na ng’ombe tele, yeye na watu waliokuwa pamoja naye, akamshawishi ili apande pamoja naye waende Ramoth-gileadi. Esaïe 22.12-22.13 1 Rois 17.7 2 Chroniques 19.2 Deutéronome 4.43 2 Rois 9.1
3 Ahabu, mfalme wa Israeli, akamwambia Yehoshafati, mfalme wa Yuda, Je! Utakwenda nami mpaka Ramoth-gileadi? Akamjibu, Mimi ni kama wewe, na watu wangu kama watu wako; nasi tutakuwa pamoja nawe vitani. Psaumes 139.21 Ephésiens 5.11 1 Rois 22.4 2 Rois 3.7 2 Jean 1.10-1.11
4 Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, Uulize leo, nakusihi, kwa neno la Bwana. 1 Rois 22.5-22.6 2 Samuel 5.19 1 Samuel 23.2 1 Samuel 23.9-23.12 2 Samuel 2.1
5 Ndipo mfalme wa Israeli akawakusanya manabii, watu mia nne; akawaambia, Je! Tuende Ramoth-gileadi vitani, au niache? Wakasema, Kwea; kwa kuwa Mungu atautia mkononi mwa mfalme. Michée 3.11 Michée 2.11 Jérémie 42.20 Ezéchiel 13.3-13.16 1 Rois 18.19
6 Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hayupo hapa nabii wa Bwana tena, ili tumwulize yeye? 2 Rois 3.11-3.13 1 Rois 22.7-22.9
7 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza Bwana kwa yeye; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema kamwe, ila siku zote mabaya; naye ndiye Mikaya mwana wa Imla. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivi. Luc 6.22 1 Rois 19.10 Michée 2.7 Psaumes 69.14 1 Rois 18.17
8 Ndipo mfalme wa Israeli akamwita akida mmoja, akasema, Mlete hima Mikaya mwana wa Imla. 1 Chroniques 28.1 2 Chroniques 18.25-18.26 1 Samuel 8.15 Daniel 1.3 Esaïe 39.7
9 Basi, mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wamekaa kila mtu katika kiti chake cha enzi, wamevaa mavazi yao, wakikaa penye sakafu pa kuingilia lango la Samaria; nao manabii wote wakafanya unabii mbele yao. Jérémie 27.14-27.16 Daniel 7.9 Matthieu 11.8 Matthieu 6.29 Matthieu 19.28
10 Na Zedekia mwana wa Kenaana akajifanyia pembe za chuma, akasema, Bwana asema hivi, Kwa hizi utawasukuma Washami, hata watakapoangamia. Jérémie 28.10-28.14 Ezéchiel 13.7 Zacharie 1.18-1.21 Ezéchiel 22.28 Jérémie 27.2
11 Na manabii wote wakatoa unabii huo, wakisema, Kwea Ramoth-gileadi, ukafanikiwe, kwa kuwa Bwana atautia mkononi mwa mfalme. 2 Chroniques 18.5 2 Pierre 2.1-2.3 Apocalypse 16.13-16.14 Apocalypse 19.20 2 Chroniques 18.12
12 Na yule mjumbe, aliyekwenda kumwita Mikaya, akamwambia, akasema, Angalia, maneno ya manabii kwa kinywa kimoja yasema mema kwa mfalme; neno lako basi na liwe kama mojawapo lao, ukaseme mema. Job 22.13 Esaïe 30.10 Michée 2.6 Josué 9.2 Psaumes 10.11
13 Mikaya akasema, Kama aishivyo Bwana, neno lile atakalolinena Mungu wangu, ndilo nitakalolinena. Nombres 22.35 Nombres 22.18-22.20 Nombres 24.13 1 Corinthiens 11.23 Jérémie 42.4
14 Na alipokuja kwa mfalme, mfalme akamwambia, Je! Mikaya, tuende Ramoth-gileadi vitani, au niache? Akasema, Kweeni, mkafanikiwe; nao watatiwa mikononi mwenu. 1 Rois 22.15 Ecclésiaste 11.1 Amos 4.4-4.5 1 Rois 18.27 Matthieu 26.45
15 Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe, usiniambie neno ila yaliyo kweli, kwa jina la Bwana? Marc 5.7 1 Rois 22.16 1 Samuel 14.24 Actes 19.13 Matthieu 26.63
16 Akasema, Naliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji; Bwana akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani. Matthieu 9.36 Marc 6.34 Ezéchiel 34.8 1 Rois 22.17 Ezéchiel 34.5-34.6
17 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Je! Sikukuambia, hatanibashiria mema, ila mabaya? 2 Chroniques 18.7 1 Rois 22.18 Proverbes 29.1 Jérémie 43.2-43.3
18 Mikaya akasema, Sikieni basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi na jeshi lote la mbinguni wamesimama mkono wake wa kuume na wa kushoto. Daniel 7.9 Esaïe 6.1-6.5 1 Rois 22.19-22.23 Esaïe 1.10 Actes 7.55-7.56
19 Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu mfalme wa Israeli, ili akwee Ramoth-gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. 1 Rois 22.20 2 Chroniques 25.8 Esaïe 54.16 Esaïe 6.9-6.10 2 Thessaloniciens 2.11-2.12
20 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani? Job 1.6 2 Corinthiens 11.13-11.15 Job 2.1 2 Corinthiens 11.3
21 Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka, ukafanye hivyo. Jean 8.44 1 Jean 4.6 2 Chroniques 18.22 2 Chroniques 18.19 Job 2.6
22 Basi sasa, angalia, Bwana ametia pepo wa uongo vinywani mwa manabii wako hawa; naye Bwana amenena mabaya juu yako. Ezéchiel 14.9 Esaïe 19.14 Job 12.16 2 Thessaloniciens 2.9-2.11 1 Timothée 4.1-4.2
23 Ndipo akakaribia Zedekia mwana wa Kenaana, akampiga Mikaya kofi la shavu, akasema, Alitokaje kwangu roho ya Bwana ili aseme na wewe? Jérémie 20.2 Marc 14.65 1 Rois 22.23-22.25 Lamentations 3.30 Michée 5.1
24 Mikaya akasema, Angalia utaona siku ile, utakapoingia katika chumba cha ndani ili ujifiche. Jérémie 29.32 Jérémie 29.21-29.22 Esaïe 26.20 Jérémie 28.16-28.17 Esaïe 26.11
25 Mfalme wa Israeli akasema, Mchukueni Mikaya mkamrudishe kwa Amoni mkuu wa mji, na kwa Yoashi mwana wa mfalme; 2 Chroniques 18.8 2 Chroniques 34.8 Actes 24.25-24.27 Jérémie 37.15-37.21 Jérémie 38.6-38.7
26 mkaseme, Mfalme asema hivi, Mtieni huyu gerezani, mkamlishe chakula cha shida, na maji ya shida, hata nitakaporudi kwa amani. 2 Chroniques 16.10 Luc 3.19-3.20 Matthieu 5.12 Psaumes 102.9 1 Thessaloniciens 5.2-5.3
27 Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, Bwana hakusema kwa mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote. Marc 7.14 Amos 9.10 Matthieu 15.10 Luc 20.45-20.46 Nombres 16.29
28 Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakakwea mpaka Ramoth-gileadi. 1 Rois 22.29-22.33
29 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Nitajibadilisha, na kuingia vitani; lakini wewe uvae mavazi yako. Mfalme wa Israeli akajibadilisha; nao wakaingia vitani. 1 Samuel 28.8 1 Rois 14.2-14.6 Job 24.15 Proverbes 26.25 Psaumes 12.2
30 Basi mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru maakida wa magari yake, akisema, Msipigane na mdogo wala mkuu, ila na mfalme wa Israeli peke yake. 1 Rois 20.42 2 Chroniques 15.13 Deutéronome 1.17 1 Rois 20.33-20.34 Genèse 19.11
31 Ikawa maakida wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, Mfalme wa Israeli ni huyu. Basi wakamgeukia ili wapigane naye; lakini Yehoshafati akalia, na Bwana akamsaidia; Mungu akawafarakisha kwake. 2 Chroniques 13.14 2 Chroniques 26.7 Esdras 7.27 Psaumes 118.13 Psaumes 46.1
32 Ikawa, maakida wa magari walipoona ya kuwa siye mfalme wa Israeli, wakageuka nyuma wasimfuate. 1 Rois 22.33
33 Na mtu mmoja akavuta upinde kwa kubahatisha, akampiga mfalme wa Israeli mahali pa kuungana mavazi yake ya chuma; kwa hiyo akamwambia mwendesha gari, Geuza mkono wako, unichukue kutoka katika majeshi; kwa kuwa nimejeruhiwa sana. 2 Chroniques 35.23 1 Rois 22.34-22.35 2 Samuel 15.11
34 Pigano likazidi siku ile; lakini mfalme wa Israeli akajitegemeza garini juu ya Washami hata jioni; akafa kama wakati wa kuchwa kwa jua. Nombres 32.23 Proverbes 28.17 2 Chroniques 18.27 2 Chroniques 18.19 2 Chroniques 18.16

Cette Bible est dans le domaine public.