Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Chroniques 7.16
Bible en Swahili de l’est


1 Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba.1 Rois 18.38 Lévitique 9.23-9.24 1 Rois 18.24 1 Chroniques 21.26 Aggée 2.7-2.9
2 Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa Bwana, kwa kuwa utukufu wa Bwana umeijaza nyumba ya Bwana.2 Chroniques 5.14 Apocalypse 15.8 Esaïe 6.5 Exode 24.17
3 Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa Bwana ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele.2 Chroniques 5.13 2 Chroniques 20.21 Esdras 3.11 Hébreux 7.24-7.25 Esaïe 63.7
4 Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana.1 Rois 8.62-8.63
5 Mfalme Sulemani akatoa sadaka ya ng’ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na watu wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Mungu.Jean 10.22 2 Chroniques 29.32-29.33 2 Chroniques 5.6 2 Chroniques 15.11 2 Chroniques 1.6
6 Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao pamoja na vinanda vya Bwana, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru Bwana, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.2 Chroniques 5.12 1 Chroniques 15.16-15.21 2 Chroniques 7.3 Psaumes 87.7 Psaumes 118.1-118.4
7 Tena Sulemani akaitakasa behewa katikati, iliyokuwa mbele ya nyumba ya Bwana; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka za kuteketezwa, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba aliyoifanya Sulemani haikutosha kuzipokea sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta.1 Rois 8.64-8.66 2 Chroniques 36.14 Hébreux 13.10-13.12 2 Chroniques 4.1 Nombres 16.37-16.38
8 Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba.Genèse 15.18 1 Rois 8.65 Nombres 29.12-29.38 Zacharie 14.16-14.19 2 Chroniques 30.13
9 Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba.Lévitique 23.36 Deutéronome 16.8 Néhémie 8.18 2 Chroniques 30.23 Joël 1.14
10 Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake.1 Rois 8.66 Psaumes 32.11-33.1 Néhémie 8.10 Deutéronome 16.11 2 Chroniques 30.26
11 Hivyo Sulemani akaimaliza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na yote yaliyomwingia Sulemani moyoni ayafanye nyumbani mwa Bwana, na nyumbani mwake mwenyewe, akayafanikisha.1 Rois 9.1-9.9 2 Chroniques 2.1 Ecclésiaste 2.4 Ecclésiaste 2.10-2.11
12 Bwana akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu.1 Rois 9.2 Deutéronome 12.11 Luc 1.13 Actes 10.31 Psaumes 10.17
13 Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni;2 Chroniques 6.26-6.28 Psaumes 107.34 Ezéchiel 14.19-14.21 Exode 10.4-10.6 Apocalypse 11.6
14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.Jacques 4.9-4.10 2 Chroniques 6.37-6.39 Esaïe 55.6-55.7 Lamentations 3.40-3.41 Proverbes 28.13
15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.2 Chroniques 6.40 2 Chroniques 6.20 Psaumes 65.2 Néhémie 1.6 Deutéronome 11.12
16 Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.2 Chroniques 7.12 2 Chroniques 6.20 1 Rois 8.35 2 Rois 21.7-21.8 Colossiens 2.9
17 Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu;Zacharie 3.7 Deutéronome 28.1-28.14 1 Rois 11.38 Psaumes 105.45 Deutéronome 4.40
18 ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli.2 Chroniques 6.16 Jérémie 33.20-33.21 Psaumes 132.11-132.12 1 Rois 9.5 Jérémie 33.25-33.26
19 Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu;Deutéronome 28.15 Lévitique 26.14 1 Samuel 12.25 1 Chroniques 28.9 Lévitique 26.33-26.46
20 ndipo nitawang’oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote.Deutéronome 28.37 Jérémie 24.9 1 Rois 9.7 2 Rois 17.20 Jérémie 45.4
21 Na nyumba hii, iliyo juu, kila apitaye ataona ushangao, atasema, Mbona Bwana ameitendea hivi nchi hii, na nyumba hii?Jérémie 22.8-22.9 Jérémie 50.13 1 Rois 9.8-9.9 Deutéronome 29.24-29.28 Jérémie 19.8
22 Nao watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine, wakaiabudu, na kuitumikia; kwa hiyo ameyaleta mabaya haya yote juu yao.Juges 2.12-2.13 Daniel 9.12 Lamentations 2.16-2.17 Ezéchiel 36.17-36.20 2 Chroniques 36.17

Cette Bible est dans le domaine public.