Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 27.14
Bible en Swahili de l’est


1 Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.Jacques 4.13-4.16 Luc 12.19-12.20 Psaumes 95.7 Esaïe 56.12 2 Corinthiens 6.2
2 Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe.Proverbes 25.27 2 Corinthiens 10.18 2 Corinthiens 12.11 2 Corinthiens 10.12
3 Jiwe ni zito, na mchanga hulemea; Lakini ghadhabu ya mpumbavu ni nzito kuliko hivi vyote viwili.Proverbes 17.12 1 Samuel 22.18-22.19 Esther 3.5-3.6 1 Jean 3.12 Genèse 34.25-34.26
4 Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.Proverbes 6.34 Proverbes 14.30 Job 5.2 Jacques 3.14-3.16 Actes 7.9
5 Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika.Proverbes 28.23 Galates 2.14 1 Timothée 5.20 Matthieu 18.15 Lévitique 19.17
6 Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.Psaumes 141.5 Job 5.17-5.18 Proverbes 26.23-26.26 Apocalypse 3.19 2 Samuel 12.7-12.15
7 Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.Nombres 21.5 Nombres 11.4-11.9 Nombres 11.18-11.20 Jean 6.9 Job 6.7
8 Kama ndege aendaye huko na huko mbali na kitundu chake; Ndivyo alivyo mtu aendaye huko na huko mbali na mahali pake.Esaïe 16.2 Proverbes 26.2 Néhémie 6.11-6.13 Job 39.14-39.16 Jonas 1.10-1.17
9 Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.Psaumes 133.2 Cantique 4.10 Psaumes 23.5 Proverbes 16.23-16.24 Esdras 10.2-10.4
10 Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali.Proverbes 18.24 Proverbes 17.17 1 Rois 12.6-12.8 Luc 10.30-10.37 2 Samuel 21.7
11 Mwanangu, uwe na hekima na kunifurahisha moyo wangu; Ili nipate kumjibu anilaumuye.Proverbes 10.1 Psaumes 119.42 Proverbes 23.15-23.16 Philémon 1.7 2 Jean 1.4
12 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.Proverbes 22.3 2 Pierre 3.10-3.14 Proverbes 18.10 Esaïe 26.20-26.21 Matthieu 3.7
13 Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni; Mtoza rehani aliye mdhamini wa malaya.Proverbes 20.16 Exode 22.26 Proverbes 6.1-6.4 Proverbes 22.26-22.27
14 Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.2 Samuel 15.2-15.7 2 Samuel 16.16-16.19 Actes 12.22-12.23
15 Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa;Proverbes 19.13 Proverbes 21.19 Proverbes 21.9 Job 14.19 Proverbes 25.24
16 Atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo; Na mkono wake wa kuume hukuta mafuta.Jean 12.3
17 Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.Hébreux 10.24 Proverbes 27.9 Job 4.3-4.4 1 Samuel 23.16 2 Timothée 2.3
18 Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake; Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.1 Corinthiens 9.7 Cantique 8.12 Luc 12.43-12.44 2 Timothée 2.6 1 Corinthiens 3.8
19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.Jacques 1.22-1.25 Genèse 6.5 Psaumes 33.15 Marc 7.21
20 Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi.Ecclésiaste 1.8 Habakuk 2.5 Proverbes 30.15-30.16 Ecclésiaste 6.7 Ecclésiaste 2.10-2.11
21 Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake.Proverbes 17.3 1 Pierre 4.12 1 Samuel 18.7-18.8 1 Samuel 18.30 Malachie 3.3
22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.Jérémie 5.3 Proverbes 23.35 Esaïe 1.5 Apocalypse 16.10-16.11 Exode 14.5
23 Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng’ombe zako.1 Pierre 5.2 Jean 21.15-21.17 Exode 7.23 Jean 10.3 1 Chroniques 27.29-27.31
24 Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Yadumu tangu kizazi hata kizazi?Proverbes 23.5 Jacques 1.10 1 Timothée 6.17-6.18 Sophonie 1.18 2 Samuel 7.16
25 Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana, Na maboga ya milimani hukusanyika.Proverbes 10.5 Psaumes 104.14
26 Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; Na mbuzi ni thamani ya shambaJob 31.20
27 Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, Ya kukutosha kwa chakula chako, Na chakula cha watu wa nyumbani mwako, Na posho la vijakazi vyako.Proverbes 30.8-30.9 Matthieu 6.33

Cette Bible est dans le domaine public.