Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jérémie 2.22
Bible en Swahili de l’est


1 Neno la Bwana likanijia, kusema,Jérémie 23.28 Jérémie 1.11 Jérémie 7.1 Hébreux 1.1 Ezéchiel 7.1
2 Enenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, Bwana asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa uposo wako; Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu.Ezéchiel 16.8 Ezéchiel 16.60 Deutéronome 2.7 Jérémie 11.6 Jérémie 7.2
3 Israeli walikuwa utakatifu kwa Bwana; malimbuko ya uzao wake; Wote watakaomla watakuwa na hatia; uovu utawajilia; asema Bwana.Jacques 1.18 Jérémie 50.7 Esaïe 41.11 Apocalypse 14.4 Exode 19.5-19.6
4 Lisikieni neno la Bwana, ninyi nyumba ya Yakobo, na ninyi, jamaa zote za nyumba ya Israeli.Jérémie 33.24 Jérémie 44.24-44.26 Jérémie 5.21 Jérémie 7.2 Jérémie 19.3
5 Bwana asema hivi, Baba zenu waliona dhuluma gani kwangu, hata wakafarakana nami, wakafuata ubatili, nao wakawa ubatili?2 Rois 17.15 Romains 1.21 Deutéronome 32.21 Jonas 2.8 Jérémie 51.17-51.18
6 Wala hawakusema, Yuko wapi Bwana, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu?Deutéronome 32.10 Osée 13.4 Deutéronome 8.14-8.16 Esaïe 63.11-63.13 Exode 14.1-14.15
7 Nami nikawatia katika nchi ya shibe, mpate kula matunda yake na mema yake; lakini ninyi mlipoingia katika nchi ile, mliitia unajisi nchi yangu, na urithi wangu mliufanya kuwa chukizo.Deutéronome 8.7-8.9 Jérémie 16.18 Psaumes 106.38-106.39 Nombres 13.27 Jérémie 3.1
8 Makuhani hawakusema, Yuko wapi Bwana? Wala wana-sheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.Habakuk 2.18 Jérémie 10.21 Jérémie 5.31 Jean 16.3 2 Corinthiens 4.2
9 Basi, kwa ajili ya hayo nitateta nanyi, asema Bwana, nami nitateta na watoto wa watoto wenu.Ezéchiel 20.35-20.36 Jérémie 2.35 Michée 6.2 Exode 20.5 Lévitique 20.5
10 Maana, vukeni mpaka visiwa vya Kitimu, mkaone; tumeni watu waende Kedari, mkafikiri sana; mkaone kwamba jambo kama hili limekuwa wakati wo wote.Psaumes 120.5 Esaïe 21.16 Ezéchiel 27.6 1 Corinthiens 5.1 Daniel 11.30
11 Je! Taifa wamebadili miungu yao, ingawa siyo miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidia.Jérémie 16.20 Esaïe 37.19 Romains 1.23 Psaumes 106.20 Michée 4.5
12 Enyi mbingu, staajabuni kwa ajili ya jambo hili, mkaogope sana, na kuwa ukiwa sana, asema Bwana.Esaïe 1.2 Deutéronome 32.1 Jérémie 22.29 Matthieu 27.50-27.53 Michée 6.2
13 Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.Jean 4.14 Psaumes 36.9 Jérémie 17.13 Apocalypse 22.1 Esaïe 55.2
14 Je! Israeli ni mtumwa? Je! Ni mzalia? mbona amekuwa mateka?Exode 4.22 Esaïe 50.1 Ecclésiaste 2.7 Genèse 15.3
15 Wana-simba wamenguruma juu yake, wametoa sana sauti zao; Nao wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; miji yake imeteketea, haina watu.Jérémie 4.7 Jérémie 50.17 Esaïe 5.29 Esaïe 1.7 Jérémie 9.11
16 Tena wana wa Nofu na Tahpanesi wamevunja utosi wa kichwa chako.Jérémie 46.14 Jérémie 43.7-43.9 Jérémie 44.1 Esaïe 19.13 Deutéronome 33.20
17 Je! Hukujipatia mambo haya mwenyewe, kwa kuwa umemwacha Bwana, Mungu wako, alipokuongoza njiani?Jérémie 4.18 Deutéronome 28.15-28.68 Lévitique 26.15-26.46 Jérémie 2.13 1 Chroniques 28.9
18 Na sasa una nini utakayotenda katika njia iendayo Misri, kunywa maji ya Shihori? Au una nini utakayotenda katika njia iendayo Ashuru, kunywa maji ya ule Mto?Josué 13.3 Esaïe 31.1 Jérémie 2.36 Osée 7.11 2 Rois 16.7-16.9
19 Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha Bwana, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, Bwana wa majeshi.Esaïe 3.9 Osée 5.5 Jérémie 4.18 Amos 8.10 Psaumes 36.1
20 Kwa maana tangu zamani wewe umeivunja nira yako, na kuvipasua vifungo vyako; ukasema, Mimi sitatumika; kwa maana juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi, umejiinamisha, ukafanya mambo ya ukahaba.Deutéronome 12.2 Lévitique 26.13 Esaïe 1.21 Jérémie 30.8 Jérémie 17.2
21 Nami nalikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu machoni pangu?Exode 15.17 Esaïe 5.4 Psaumes 80.8 Psaumes 44.2 Deutéronome 32.32
22 Maana ujapojiosha kwa magadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele zangu, asema Bwana MUNGU.Osée 13.12 Jérémie 17.1 Job 14.17 Psaumes 130.3 Deutéronome 32.34
23 Wawezaje kusema, Sikutiwa unajisi, sikuwafuata Mabaali? Itazame njia yako bondeni, ujue uliyoyatenda; wewe u ngamia mwepesi, apitaye katika njia zake;Jérémie 7.31 Proverbes 30.12 Esaïe 57.5-57.6 Apocalypse 3.17-3.18 Jérémie 2.33-2.35
24 punda wa mwitu aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo katika tamaa yake; katika wakati wake ni nani awezaye kumgeuza? Wote wamtafutao hawatajichokesha nafsi zao; katika mwezi wake watamwona.Jérémie 14.6 Job 11.12 Job 39.5-39.8 Osée 5.15 Jérémie 2.27
25 Zuia mguu wako usikose kiatu, na koo yako isiwe na kiu; lakini wewe ulisema, Hapana matumaini kabisa; la, maana nimewapenda wageni, nami nitawafuata.Deutéronome 32.16 Jérémie 3.13 Romains 8.24 Jérémie 18.12 Osée 2.3
26 Kama mwivi aonavyo haya akamatwapo, ndivyo waonavyo haya nyumba ya Israeli; wao, na wafalme wao, na wakuu wao, na makuhani wao, na manabii wao;Néhémie 9.32-9.34 Esdras 9.7 Jérémie 32.32 Esaïe 1.29 Jérémie 2.36
27 waliambiao gogo la mti, Wewe u baba yangu; na kuliambia jiwe, Ndiwe uliyenizaa; kwa maana wamenipa mimi visogo, wala hawakunielekezea nyuso zao; lakini wakati wa taabu watasema, Simama ukatuokoe.Esaïe 26.16 Jérémie 18.17 Osée 7.14 Osée 5.15 Jérémie 10.8
28 Lakini wako wapi miungu yako ulioifanya? Na wasimame hao, kama wakiweza kukuokoa wakati wa taabu yako; kwa maana hesabu ya miungu yako ni sawasawa na hesabu ya miji yako, Ee Yuda.Jérémie 11.13 Deutéronome 32.37 Esaïe 45.20 Juges 10.14 2 Rois 17.30-17.31
29 Mbona mnataka kuteta nami? Ninyi nyote mmeniasi, asema Bwana.Jérémie 6.13 Daniel 9.11 Jérémie 5.1 Jérémie 2.35 Jérémie 3.2
30 Nimewapiga watoto wako bure; hawakukubali kurudiwa; upanga wenu wenyewe umewala manabii wako, kama simba aharibuye.Néhémie 9.26 1 Thessaloniciens 2.15 Actes 7.52 Jérémie 26.20-26.24 Jérémie 5.3
31 Ee kizazi litazameni neno la Bwana. Je! Nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza kuu? Mbona watu wangu wanasema, Sisi tumetoroka, hatutaki kuja kwako tena?Deutéronome 32.15 Deutéronome 8.12-8.14 Malachie 3.9-3.11 Psaumes 10.4 Néhémie 9.21-9.25
32 Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake, au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu.Psaumes 106.21 Jérémie 3.21 Esaïe 17.10 Osée 8.14 Esaïe 61.10
33 Jinsi ulivyoitengeneza njia yako ili kutafuta mapenzi! Kwa sababu hiyo hata wanawake wabaya umewafundisha njia zako.Jérémie 2.23 Ezéchiel 16.27 Ezéchiel 16.47 Osée 2.5-2.7 Osée 2.13
34 Tena katika pindo za nguo zako imeonekana damu ya roho zao maskini wasio na hatia; sikuiona penye mahali palipobomoka, lakini naliiona juu ya hawa wote.2 Rois 21.16 Jérémie 19.4 2 Rois 24.4 Exode 22.2 Esaïe 59.7
35 Lakini ulisema, Sina hatia mimi; bila shaka hasira yake imegeuka na kuniacha. Tazama, nitaingia hukumuni pamoja nawe, kwa sababu unasema, Sikutenda dhambi mimi.Proverbes 28.13 Jérémie 25.31 Job 33.9 Romains 7.9 Jérémie 2.23
36 Mbona unatanga-tanga hivi upate kugeuza mwendo wako? Utaona haya kwa ajili ya Misri pia, kama ulivyoona haya kwa ajili ya Ashuru.Jérémie 31.22 Osée 5.13 2 Chroniques 28.20-28.21 Osée 12.1 Jérémie 2.23
37 Hata kwake pia utatoka, na mikono yako juu ya kichwa chako; kwa maana Bwana amewakataa uliowakimbilia, wala hutafanikiwa katika hao.2 Samuel 13.19 Jérémie 37.7-37.10 Ezéchiel 17.15-17.20 Jérémie 17.5 2 Chroniques 13.12

Cette Bible est dans le domaine public.