Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Ezéchiel 42.4 Bible en Swahili de l’est
1 Ndipo akanileta mpaka ua wa nje, njia ya kuelekea upande wa kaskazini; akaniingiza katika chumba kilichopakabili mahali palipotengeka, na kilicholikabili jengo upande wa kaskazini;Ezéchiel 40.20 Ezéchiel 40.17 Ezéchiel 42.13 Ezéchiel 42.4 Ezéchiel 41.12-41.15 2 kukabili urefu wa dhiraa mia palikuwa na mlango wa kaskazini, na upana wake ni dhiraa hamsini.Ezéchiel 41.13 3 Kukabili zile dhiraa ishirini za ua wa ndani, na kukabili sakafu ya mawe ya ua wa nje, palikuwa na baraza kukabili baraza katika orofa ya tatu.Ezéchiel 41.15-41.16 Ezéchiel 41.10 Cantique 7.5 Ezéchiel 40.17-40.18 Cantique 1.17 4 Na mbele ya vile vyumba palikuwa na njia, upana wake dhiraa kumi upande wa ndani, njia ya dhiraa mia, na milango yake ilielekea upande wa kaskazini.Ezéchiel 46.19 Matthieu 7.14 Luc 13.24 5 Basi vile vyumba vya juu vilikuwa vifupi zaidi; kwa maana baraza zile zilivipunguza kuliko zilivyovipunguza vya chini na vya katikati.Ezéchiel 41.7 6 Maana vilikuwa vina orofa tatu, wala havikuwa na nguzo kama nguzo za zile nyua; basi kila kilichokuwa cha juu kilikuwa chembamba kuliko cha chini na cha katikati, kutoka chini.Ezéchiel 41.6 1 Rois 6.8 7 Na ukuta ule uliokuwa nje, ubavuni mwa vyumba vile, ulioelekea ua wa nje, kuvikabili vyumba vile, urefu wake ni dhiraa hamsini.Ezéchiel 42.12 Ezéchiel 42.10 8 Maana urefu wa vyumba vile, vilivyokuwa katika ua wa nje, ulikuwa dhiraa hamsini; na tazama, mbele ya hekalu, dhiraa mia.Ezéchiel 41.13-41.14 9 Na toka chini ya vyumba vile palikuwa na mahali pa kuingilia upande wa mashariki, mtu aviingiavyo toka ua wa nje.Ezéchiel 46.19 Ezéchiel 44.5 10 Tena palikuwa na vyumba katika unene wa ukuta wa ua, kuukabili upande wa mashariki, kupaelekea mahali palipotengeka, na kulielekea jengo.Ezéchiel 42.1 Ezéchiel 42.13 Ezéchiel 40.17 Ezéchiel 42.7 Ezéchiel 41.12-41.15 11 Nayo njia iliyokuwa mbele yake, kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake vyumba vile vilivyokuwa upande wa kaskazini, urefu ule ule, na upana ule ule; na mahali pake pa kutokea palikuwa sawasawa na vipimo vyake, na sawasawa na milango yake.Ezéchiel 42.4 12 Na sawasawa na milango ya vyumba, vilivyoelekea upande wa kusini, palikuwa na mlango katika mwisho wa njia ile; yaani, njia iliyoukabili ukuta upande wa mashariki, mtu akiingia. 13 Kisha akaniambia, Vyumba vya upande wa kaskazini, na vyumba vya upande wa kusini, ambavyo vyaelekea mahali palipotengeka, ni vyumba vitakatifu; humo makuhani, wamkaribiao Bwana, watakula vitu vilivyo vitakatifu sana; humo wataviweka vitu vilivyo vitakatifu sana, na sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia; kwa maana mahali hapo ni patakatifu.Lévitique 7.6 Lévitique 10.17 Ezéchiel 40.46 Nombres 18.9-18.10 Lévitique 6.29 14 Makuhani watakapoingia ndani, hawatatoka mahali patakatifu kwenda hata ua wa nje; lakini wataweka mavazi yao katika mahali wahudumiapo; maana ni matakatifu; nao watavaa mavazi mengine, na kupakaribia mahali palipo mahali pa watu.Ezéchiel 44.19 Lévitique 8.7 Zacharie 3.4-3.5 Exode 29.4-29.9 Lévitique 8.13 15 Basi, alipokuwa amekwisha kuipima nyumba ya ndani, akanileta nje, kwa njia ya lango lililokabili upande wa mashariki, akalipima pande zote.Ezéchiel 43.1 Ezéchiel 41.2-41.5 Ezéchiel 40.6-40.16 Ezéchiel 41.15 16 Akaupima upande wa mashariki kwa mwanzi wa kupimia, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote.Ezéchiel 40.3 Apocalypse 11.1-11.2 Zacharie 2.1 17 Akaupima upande wa kaskazini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote. 18 Akaupima upande wa kusini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia. 19 Akageuka aelekee upande wa magharibi, akapima mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia. 20 Alipima pande zake zote nne; lilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mianzi mia tano, ili kupatenga mahali palipo patakatifu, na mahali palipo pa watu wote.Ezéchiel 45.2 Ezéchiel 22.26 Ezéchiel 40.5 Zacharie 2.5 Ezéchiel 44.23