Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Josué 7
Bible en Swahili de l’est


1 Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana wa Israeli. Josué 22.20 Josué 6.17-6.18 Josué 7.20-7.21 1 Chroniques 2.6-2.7 Hébreux 12.15-12.16
2 Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu na Bethaveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, Pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai. Josué 18.12 1 Samuel 14.23 1 Samuel 13.5 Osée 4.15 Néhémie 11.31
3 Wakarejea kwa Yoshua wakamwambia, Wasiende watu wote, ila waende watu kama elfu mbili, tatu, wakaupige Ai; usiwataabishe watu wote kwa kuwaendesha huko; maana watu hao ni wachache tu. Hébreux 4.11 Luc 13.24 Proverbes 21.25 Proverbes 13.4 2 Pierre 1.10
4 Basi watu wakaenda huko wapata elfu tatu tu; nao wakakimbia mbele ya watu wa Ai. Deutéronome 28.25 Lévitique 26.17 Esaïe 59.2 Esaïe 30.17 Deutéronome 32.30
5 Watu wa Ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye matelemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji. Josué 2.11 Josué 2.9 Lévitique 26.36 Esaïe 13.7 Ezéchiel 21.7
6 Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Bwana hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao. Genèse 37.29 Nombres 14.6 2 Samuel 13.31 Genèse 37.34 Job 1.20
7 Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tungelikuwa radhi kukaa ng’ambo ya Yordani 2 Rois 3.10 Psaumes 116.11 Matthieu 17.17 Jérémie 12.1-12.2 Nombres 20.4-20.5
8 Ee Bwana, niseme nini baada ya Israeli kuwapa visogo adui zao? Habakuk 2.1 Esdras 9.10 Romains 3.5-3.6
9 Maana Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watasikia habari hii, nao watatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu? Psaumes 83.4 Exode 32.12 Joël 2.17 Psaumes 106.6-106.8 Psaumes 124.2-124.3
10 Bwana akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi? 1 Samuel 15.22 1 Samuel 16.1 1 Chroniques 22.16 Exode 14.15
11 Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe. Actes 5.1-5.2 Josué 6.17-6.19 Zacharie 5.4 Osée 6.7 Jean 12.5-12.6
12 Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu. Nombres 14.45 Josué 6.18 Psaumes 5.4-5.5 Juges 2.14 Habakuk 1.13
13 Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe tayari kesho; maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu. Josué 3.5 2 Chroniques 28.10 Exode 19.10-19.15 1 Corinthiens 5.1-5.6 Matthieu 7.5
14 Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa Bwana itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa Bwana itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa Bwana itakaribia mtu kwa mtu. Proverbes 16.33 1 Samuel 14.38-14.42 1 Samuel 10.19-10.21 Actes 1.24-1.26 Josué 7.17-7.18
15 Tena itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye anacho kitu kile kilichowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote alivyo navyo; kwa sababu amelivunja agano la Bwana, na kwa sababu ametenda upumbavu katika Israeli. Genèse 34.7 1 Samuel 14.38-14.39 Juges 20.6 1 Samuel 26.21 Deutéronome 13.15-13.16
16 Basi Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasogeza Israeli kabila kwa kabila; kabila ya Yuda ikatwaliwa. Ecclésiaste 9.10 Genèse 22.3 Psaumes 119.60 Josué 3.1
17 Akazisogeza jamaa za Yuda, akaitwaa jamaa ya Wazera; akaisogeza jamaa ya Wazera mtu kwa mtu; Zabdi akatwaliwa. Nombres 26.20 1 Chroniques 2.4-2.7 Genèse 38.30
18 Akawasogeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda akatwaliwa. Nombres 32.23 Actes 5.1-5.10 1 Samuel 14.42 Jérémie 2.26 Proverbes 13.21
19 Yoshua akamwambia Akani, Mwanangu, nakusihi, umtukuze Bwana, Mungu wa Israeli, ukaungame kwake; uniambie sasa ulilolitenda; usinifiche. 1 Samuel 6.5 Jérémie 13.16 Jean 9.24 2 Chroniques 30.22 1 Samuel 14.43
20 Akani akamjibu Yoshua, akasema, Kweli nimefanya dhambi juu ya Bwana, Mungu wa Israeli, nami nimefanya mambo haya na haya. Psaumes 38.18 Genèse 42.21 Exode 10.16 Matthieu 27.4 Job 7.20
21 Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake. Jacques 1.15 2 Pierre 2.15 Luc 12.15 Esaïe 29.15 1 Jean 2.15-2.16
22 Basi Yoshua akatuma wajumbe wakapiga mbio mpaka hemani; na tazama, vile vitu vilikuwa vimefichwa hemani mwake, na ile fedha chini yake. 23 Wakavitoa kutoka hapo katikati ya hema, wakavileta kwa Yoshua, na kwa wana wa Israeli wote, nao wakaviweka chini mbele za Bwana. 24 Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori. Josué 15.7 Osée 2.15 Esaïe 65.10 Josué 7.26 Proverbes 15.27
25 Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? Bwana atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe. Josué 6.18 1 Chroniques 2.7 Deutéronome 17.5 Lévitique 20.2 Lévitique 24.14
26 Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa ya mawe hata leo; naye Bwana akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata hivi leo. Esaïe 65.10 Osée 2.15 Deutéronome 13.17 2 Samuel 18.17 Josué 7.24

Cette Bible est dans le domaine public.