Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 102
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie. Exode 2.23 Psaumes 18.6 Psaumes 61.2 Juges 10.16 1 Samuel 1.15-1.16
2 Usinifiche uso wako siku ya shida yangu, Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi. Psaumes 69.17 Psaumes 27.9 Actes 12.5-12.25 Job 34.29 Psaumes 22.19
3 Maana siku zangu zinatoweka kama moshi, Na mifupa yangu inateketea kama kinga. Jacques 4.14 Psaumes 37.20 Lamentations 1.13 Job 30.30 Psaumes 31.10
4 Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu. Psaumes 37.2 Esaïe 40.7 Esdras 10.6 Job 10.1 Job 33.20
5 Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwangu Mifupa yangu imegandamana na nyama yangu. Job 19.20 Psaumes 6.8 Proverbes 17.22 Lamentations 4.8 Psaumes 32.3-32.4
6 Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani, Na kufanana na bundi wa mahameni. Sophonie 2.14 Michée 1.8 Esaïe 34.11-34.15 Apocalypse 18.2 Esaïe 38.14
7 Nakesha, tena nimekuwa kama shomoro Aliye peke yake juu ya nyumba. Psaumes 77.4 Psaumes 38.11 Job 7.13-7.16 Lamentations 3.28-3.30 Psaumes 22.2
8 Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; Wanaonichukia kana kwamba wana wazimu Huapa kwa kunitaja mimi. Actes 26.11 Actes 23.12-23.35 Jérémie 29.22 Psaumes 69.9-69.10 Psaumes 2.1
9 Maana nimekula majivu kama chakula, Na kukichanganya kinywaji changu na machozi. Psaumes 42.3 Psaumes 80.5 Lamentations 3.15-3.16 Lamentations 3.48-3.49 Job 3.24
10 Kwa sababu ya ghadhabu yako na hasira yako; Maana umeniinua na kunitupilia mbali. Psaumes 38.3 Psaumes 73.18-73.20 Daniel 9.8-9.14 Psaumes 38.18 Psaumes 30.6-30.7
11 Siku zangu zi kama kivuli kilichotandaa, Nami ninanyauka kama majani. Job 14.2 Psaumes 109.23 Psaumes 144.4 Jacques 1.10 Ecclésiaste 6.12
12 Bali Wewe, Bwana utaketi ukimiliki milele, Na kumbukumbu lako kizazi hata kizazi. Psaumes 9.7 Psaumes 135.13 Exode 3.15 Lamentations 5.19 Esaïe 60.15
13 Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia. Galates 4.4 Psaumes 44.26 Esaïe 40.2 Esdras 1.1-1.11 Apocalypse 11.15-11.18
14 Maana watumishi wako wameyaridhia mawe yake, Na kuyaonea huruma mavumbi yake. Néhémie 4.2 Esdras 7.27 Esdras 1.5 Esdras 3.1-3.3 Psaumes 79.7-79.10
15 Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana, Na wafalme wote wa dunia utukufu wako; 1 Rois 8.43 Psaumes 138.4 Psaumes 86.9 Psaumes 72.11 Psaumes 67.2-67.4
16 Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni, Atakapoonekana katika utukufu wake, Esaïe 60.1-60.2 Psaumes 147.2 Michée 2.9 Psaumes 51.18 Psaumes 97.6
17 Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao. Néhémie 1.6 Psaumes 22.24 Daniel 9.3-9.21 Psaumes 9.18 Psaumes 72.12
18 Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo, Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana. Romains 15.4 1 Corinthiens 10.11 Psaumes 22.30-22.31 Esaïe 43.21 2 Timothée 3.16-3.17
19 Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi, Deutéronome 26.15 Psaumes 14.2 Job 22.12 Hébreux 8.1-8.2 1 Rois 8.43
20 Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa. Psaumes 79.11 Psaumes 146.7 2 Chroniques 33.11-33.13 Job 24.12 Zacharie 9.9-9.12
21 Watu walitangaze jina la Bwana katika Sayuni, Na sifa zake katika Yerusalemu, Psaumes 22.22 Psaumes 79.13 Esaïe 51.11 Psaumes 51.14-51.15 1 Pierre 2.9
22 Pindi mataifa watapokusanyika pamoja, Falme nazo ili kumtumikia Bwana. Zacharie 8.20-8.23 Psaumes 72.8-72.11 Esaïe 49.22-49.23 Matthieu 24.14 Romains 15.19
23 Amezipunguza nguvu zangu njiani; Amezifupisha siku zangu. Job 21.21 Psaumes 89.38-89.47 2 Thessaloniciens 2.3-2.12 2 Timothée 3.1-3.17 Apocalypse 11.2-11.19
24 Nitasema, Ee Mungu wangu, usiniondoe katikati ya siku zangu; Miaka yako ni tangu kizazi hata kizazi. Habakuk 1.12 Psaumes 102.12 Psaumes 39.13 Job 36.26 Psaumes 9.7
25 Hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi, Na mbingu ni kazi ya mikono yako. Genèse 1.1 Hébreux 1.10-1.12 Genèse 2.1 Exode 20.11 Hébreux 3.3-3.4
26 Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumu Naam, hizi zitachakaa kama nguo; Na kama mavazi utazibadilisha, Nazo zitabadilika. Esaïe 34.4 Esaïe 51.6 Apocalypse 20.11 Matthieu 24.35 Romains 8.20
27 Lakini Wewe U Yeye yule; Na miaka yako haitakoma. Jacques 1.17 Malachie 3.6 Hébreux 13.8 Job 36.26 Psaumes 90.4
28 Wana wa watumishi wako watakaa, Na wazao wao wataimarishwa mbele zako. Psaumes 45.16-45.17 Psaumes 69.35-69.36 Esaïe 59.20-59.21 Psaumes 22.30-22.31 Esaïe 66.22

Cette Bible est dans le domaine public.