Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 74
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako? Psaumes 100.3 Deutéronome 29.20 Psaumes 95.7 Psaumes 79.13 Psaumes 44.9
2 Ulikumbuke kusanyiko lako, Ulilolinunua zamani. Ulilolikomboa liwe kabila ya urithi wako, Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako. Jérémie 10.16 Deutéronome 32.9 Exode 15.16 Jérémie 51.19 Psaumes 132.13-132.14
3 Upainulie miguu yako palipoharibika milele; Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu. Psaumes 79.1 Luc 21.24 Néhémie 2.3 Lamentations 1.10 Jérémie 52.13
4 Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako; Wameweka bendera zao ziwe alama. Lamentations 2.7 Nombres 2.2 Matthieu 24.15 Luc 21.20 Daniel 6.27
5 Wanaonekana kama watu wainuao mashoka, Waikate miti ya msituni. Jérémie 46.22-46.23 2 Chroniques 2.14 1 Rois 5.6
6 Na sasa nakishi yake yote pia Wanaivunja-vunja kwa mashoka na nyundo. 1 Rois 6.18 1 Rois 6.32 1 Rois 6.35 1 Rois 6.29
7 Wamepatia moto patakatifu pako; Wamelinajisi kao la jina lako hata chini. Psaumes 89.39 2 Rois 25.9 Lamentations 2.2 1 Rois 8.20 Matthieu 22.7
8 Walisema mioyoni mwao, Na tuwaangamize kabisa; Mahali penye mikutano ya Mungu Wamepachoma moto katika nchi pia. Psaumes 83.4 2 Rois 4.23 Matthieu 4.23 2 Rois 2.3 Psaumes 137.7
9 Hatuzioni ishara zetu, wala sasa hakuna nabii, Wala kwetu hakuna ajuaye, hata lini? 1 Samuel 3.1 Amos 8.11 Ezéchiel 20.12 Lamentations 2.9 Juges 6.17
10 Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini? Adui alidharau jina lako hata milele? Psaumes 44.16 Psaumes 13.1-13.2 Daniel 12.6 Psaumes 89.50-89.51 Psaumes 89.46
11 Mbona unaurudisha mkono wako, Naam, mkono wako wa kuume, Uutoe kifuani mwako, Ukawaangamize kabisa. Lamentations 2.3 Psaumes 78.65-78.66 Psaumes 44.23 Esaïe 64.12
12 Lakini Mungu ni mfalme wangu tokea zamani, Afanyaye mambo ya wokovu katikati ya nchi. Psaumes 44.4 Habakuk 3.12-3.14 Juges 4.23-4.24 Nombres 23.21-23.22 Esaïe 33.22
13 Wewe umeipasua bahari kwa nguvu zako, Umevivunja vichwa vya nyangumi juu ya maji. Exode 14.21 Ezéchiel 29.3 Psaumes 78.13 Psaumes 136.13-136.18 Psaumes 106.8-106.9
14 Wewe uliviseta vichwa vya lewiathani, Awe chakula cha watu wa jangwani. Esaïe 27.1 Psaumes 104.25-104.26 Exode 14.30 Exode 12.35-12.36 Psaumes 72.9
15 Wewe ulitokeza chemchemi na kijito; Wewe ulikausha mito yenye maji sikuzote. Nombres 20.11 Esaïe 48.21 Exode 17.5-17.6 Psaumes 105.41 Josué 2.10
16 Mchana ni wako, usiku nao ni wako, Ndiwe uliyeufanya mwanga na jua. Psaumes 136.7-136.9 Genèse 1.14-1.18 Psaumes 104.19 Genèse 1.3-1.5 Psaumes 8.3
17 Wewe uliiweka mipaka yote ya dunia, Kaskazi na kusi Wewe ulizitengeneza. Deutéronome 32.8 Actes 17.26 Genèse 8.22 Psaumes 24.1-24.2 Actes 14.17
18 Ee Bwana, uyakumbuke hayo, adui amelaumu, Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako. Psaumes 39.8 Deutéronome 32.6 Apocalypse 16.19 Esaïe 37.23-37.24 Psaumes 74.22
19 Usimpe mnyama mkali nafsi ya hua wako; Usiusahau milele uhai wa watu wako walioonewa. Cantique 2.14 Psaumes 68.10 Psaumes 68.13 Matthieu 10.16 Cantique 6.9
20 Ulitafakari agano; Maana mahali penye giza katika nchi Pamejaa makao ya ukatili. Psaumes 106.45 Genèse 17.7-17.8 Luc 1.72-1.75 2 Samuel 23.5 Psaumes 105.8
21 Aliyeonewa asirejee ametiwa haya, Mnyonge na mhitaji na walisifu jina lako. Esaïe 45.17 Psaumes 109.22 Psaumes 35.10 Psaumes 102.19-102.21 Esdras 3.11
22 Ee Mungu, usimame, ujitetee mwenyewe, Ukumbuke unavyotukanwa na mpumbavu mchana kutwa. Psaumes 74.18 Psaumes 75.4-75.5 Psaumes 79.9-79.10 Psaumes 89.50-89.51 Esaïe 52.5
23 Usiisahau sauti ya watesi wako, Ghasia yao wanaokuondokea inapaa daima. Esaïe 37.29 Psaumes 65.7 Lamentations 2.16 Psaumes 10.11-10.12 Psaumes 2.1-2.2

Cette Bible est dans le domaine public.