Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 74
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako? Psaumes 95.7 Psaumes 79.13 Psaumes 100.3 Deutéronome 29.20 Psaumes 44.9
2 Ulikumbuke kusanyiko lako, Ulilolinunua zamani. Ulilolikomboa liwe kabila ya urithi wako, Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako. Exode 15.16 Jérémie 10.16 Deutéronome 32.9 Deutéronome 9.29 Psaumes 135.4
3 Upainulie miguu yako palipoharibika milele; Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu. Psaumes 79.1 Apocalypse 11.2 Psaumes 44.23 Esaïe 63.3-63.6 2 Samuel 22.39-22.43
4 Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako; Wameweka bendera zao ziwe alama. Lamentations 2.7 Matthieu 24.15 Nombres 2.2 Daniel 6.27 2 Chroniques 36.17
5 Wanaonekana kama watu wainuao mashoka, Waikate miti ya msituni. 1 Rois 5.6 Jérémie 46.22-46.23 2 Chroniques 2.14
6 Na sasa nakishi yake yote pia Wanaivunja-vunja kwa mashoka na nyundo. 1 Rois 6.18 1 Rois 6.35 1 Rois 6.29 1 Rois 6.32
7 Wamepatia moto patakatifu pako; Wamelinajisi kao la jina lako hata chini. Psaumes 89.39 2 Rois 25.9 Deutéronome 12.5 Exode 20.24 Ezéchiel 24.21
8 Walisema mioyoni mwao, Na tuwaangamize kabisa; Mahali penye mikutano ya Mungu Wamepachoma moto katika nchi pia. Psaumes 83.4 2 Rois 2.3 Psaumes 137.7 2 Chroniques 17.9 2 Rois 2.5
9 Hatuzioni ishara zetu, wala sasa hakuna nabii, Wala kwetu hakuna ajuaye, hata lini? 1 Samuel 3.1 Amos 8.11 Exode 12.13 Michée 3.6 Hébreux 2.4
10 Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini? Adui alidharau jina lako hata milele? Daniel 12.6 Psaumes 89.50-89.51 Psaumes 89.46 Apocalypse 6.10 Psaumes 79.4-79.5
11 Mbona unaurudisha mkono wako, Naam, mkono wako wa kuume, Uutoe kifuani mwako, Ukawaangamize kabisa. Lamentations 2.3 Psaumes 44.23 Esaïe 64.12 Psaumes 78.65-78.66
12 Lakini Mungu ni mfalme wangu tokea zamani, Afanyaye mambo ya wokovu katikati ya nchi. Psaumes 44.4 Esaïe 33.22 Esaïe 63.8 1 Samuel 19.5 Exode 15.2-15.15
13 Wewe umeipasua bahari kwa nguvu zako, Umevivunja vichwa vya nyangumi juu ya maji. Exode 14.21 Psaumes 78.13 Ezéchiel 29.3 Néhémie 9.11 Ezéchiel 32.2
14 Wewe uliviseta vichwa vya lewiathani, Awe chakula cha watu wa jangwani. Esaïe 27.1 Psaumes 72.9 Job 3.8 Nombres 14.9 Job 41.1-41.34
15 Wewe ulitokeza chemchemi na kijito; Wewe ulikausha mito yenye maji sikuzote. Nombres 20.11 Psaumes 105.41 Esaïe 48.21 Exode 17.5-17.6 Josué 2.10
16 Mchana ni wako, usiku nao ni wako, Ndiwe uliyeufanya mwanga na jua. Psaumes 136.7-136.9 Genèse 1.14-1.18 Genèse 1.3-1.5 Psaumes 8.3 Matthieu 5.45
17 Wewe uliiweka mipaka yote ya dunia, Kaskazi na kusi Wewe ulizitengeneza. Actes 17.26 Genèse 8.22 Deutéronome 32.8 Actes 14.17 Psaumes 24.1-24.2
18 Ee Bwana, uyakumbuke hayo, adui amelaumu, Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako. Psaumes 39.8 Apocalypse 16.19 Deutéronome 32.6 Psaumes 41.1 Deutéronome 32.27
19 Usimpe mnyama mkali nafsi ya hua wako; Usiusahau milele uhai wa watu wako walioonewa. Cantique 2.14 Psaumes 68.10 Jacques 2.5-2.6 Sophonie 3.12 Esaïe 60.8
20 Ulitafakari agano; Maana mahali penye giza katika nchi Pamejaa makao ya ukatili. Psaumes 106.45 Genèse 17.7-17.8 Lévitique 26.40-26.45 Jérémie 33.20-33.26 Psaumes 89.28
21 Aliyeonewa asirejee ametiwa haya, Mnyonge na mhitaji na walisifu jina lako. Psaumes 102.19-102.21 Esdras 3.11 Psaumes 9.18 Psaumes 103.6 Jérémie 33.11
22 Ee Mungu, usimame, ujitetee mwenyewe, Ukumbuke unavyotukanwa na mpumbavu mchana kutwa. Psaumes 74.18 Psaumes 89.50-89.51 Esaïe 52.5 Psaumes 9.19-9.20 Psaumes 53.1
23 Usiisahau sauti ya watesi wako, Ghasia yao wanaokuondokea inapaa daima. Esaïe 37.29 Psaumes 65.7 Apocalypse 17.14 Psaumes 74.4 Jonas 1.2

Cette Bible est dans le domaine public.