Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jérémie 8
Bible en Swahili de l’est


1 Wakati ule, asema Bwana, watatoa mifupa ya wafalme wa Yuda, na mifupa ya wakuu wake, na mifupa ya makuhani, na mifupa ya manabii na mifupa ya wenyeji wa Yerusalemu, itoke makaburini mwao; Ezéchiel 6.5 1 Rois 13.2 2 Rois 23.16 Amos 2.1 2 Rois 23.20
2 nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi. 2 Rois 23.5 Jérémie 9.22 Actes 7.42 Sophonie 1.5 Deutéronome 4.19
3 Na kufa kutachaguliwa kuliko kuishi na mabaki yote waliosalia katika jamaa hii mbovu, waliosalia kila mahali nilikowafukuza, asema Bwana wa majeshi. Apocalypse 9.6 Jérémie 23.3 Jérémie 23.8 Job 7.15-7.16 Jérémie 29.14
4 Tena utawaambia, Bwana asema hivi, Je! Watu wataanguka, wasisimame tena? Je! Mtu atageuka aende zake, asirudi tena? Proverbes 24.16 Osée 6.1 Michée 7.8 Osée 7.10 Osée 14.1
5 Mbona, basi, watu hawa wa Yerusalemu wamegeuka waende nyuma, wasikome kugeuka hivyo? Hushika udanganyifu sana, hukataa kurudi. Jérémie 9.6 Zacharie 7.11 Hébreux 12.25 Esaïe 30.10 2 Thessaloniciens 2.9-2.12
6 Nalisikiliza nikasikia, lakini walisema yasiyo sawa; hapana mtu aliyetubia maovu yake, akisema, Nimefanya nini? Kila mtu hurudia mwendo wake mwenyewe, kama farasi aendavyo kasi vitani. Psaumes 14.2 2 Pierre 3.9 Ezéchiel 22.30 Malachie 3.16 Michée 7.2
7 Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za Bwana. Esaïe 1.3 Cantique 2.12 Jérémie 5.4-5.5 Proverbes 6.6-6.8 Esaïe 5.12
8 Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo. Job 5.12-5.13 Romains 1.22 Job 11.12 Romains 2.17-2.29 Proverbes 17.6
9 Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la Bwana, wana akili gani ndani yao? Jérémie 6.15 Psaumes 119.98-119.100 Jérémie 6.19 Deutéronome 4.6 Esaïe 19.11
10 Basi, kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao na mashamba yao nitawapa wale watakaowamiliki; maana kila mmoja wao, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa, ni mtamanifu; tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu. Jérémie 6.12-6.13 Jérémie 23.11-23.17 Esaïe 28.7 Amos 5.11 Ezéchiel 22.27-22.28
11 Kwa maana wameiponya jeraha ya binti ya watu wangu kwa juu-juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani. Jérémie 6.14 Lamentations 2.14 1 Rois 22.6 Michée 2.11 Ezéchiel 13.10-13.16
12 Je! Walitahayarika, walipokuwa wametenda machukizo? La! Hawakutahayarika, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi wataanguka miongoni mwao waangukao; wakati wa kujiliwa kwao wataangushwa chini, asema Bwana. Jérémie 3.3 Esaïe 3.9 Jérémie 6.15 Psaumes 52.7 Deutéronome 32.35
13 Nitawaangamiza kabisa, asema Bwana; hapana zabibu katika mizabibu, wala tini katika mitini, hata jani lake litanyauka; na vitu vile nilivyowapa vitawapotea. Joël 1.7 Matthieu 21.19 Luc 13.6-13.9 Psaumes 1.3-1.4 Habakuk 3.17
14 Mbona tunakaa kimya? Jikusanyeni, tukaingie ndani ya miji yenye maboma, tukanyamaze humo kwa maana Bwana, Mungu wetu, ametunyamazisha, naye ametupa maji yenye uchungu tunywe, kwa sababu tumemwasi Bwana. Jérémie 23.15 Jérémie 9.15 Lamentations 3.19 Jérémie 35.11 Matthieu 27.34
15 Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yo yote; tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu! Jérémie 14.19 Jérémie 8.11 1 Thessaloniciens 5.3 Jérémie 4.10 Michée 1.12
16 Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi zake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi zake za vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake. Juges 5.22 Juges 18.29 Psaumes 24.1 1 Corinthiens 10.28 Jérémie 6.23
17 Maana, tazama, nitatuma nyoka, naam, fira, kati yenu, wasioweza kutumbuizwa kwa uganga; nao watawauma, asema Bwana. Deutéronome 32.24 Psaumes 58.4-58.5 Ecclésiaste 10.11 Nombres 21.6 Amos 5.19
18 Laiti ningeweza kujifariji, nisione huzuni! Moyo wangu umezimia ndani yangu. Lamentations 1.16-1.17 Lamentations 5.17 Esaïe 22.4 Jérémie 6.24 Daniel 10.16-10.17
19 Tazama, sauti ya kilio cha binti ya watu wangu, itokayo katika nchi iliyo mbali sana; Je! Bwana hayumo katika Sayuni? Mfalme wake hayumo ndani yake? Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao walizochonga, na kwa ubatili wa kigeni? Esaïe 39.3 Esaïe 13.5 Deutéronome 32.16-32.21 Esaïe 12.6 Jérémie 31.6
20 Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka. Luc 13.25 Matthieu 25.1-25.12 Hébreux 3.7-3.15 Proverbes 10.5 Luc 19.44
21 Kwa sababu ya maumivu ya binti ya watu wangu nimeumia mimi; nimevaa kaniki; ushangao umenishika. Jérémie 14.17 Nahum 2.10 Joël 2.6 Jérémie 4.19 Romains 9.1-9.3
22 Je! Hapana zeri katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu? Jérémie 46.11 Genèse 37.25 Jérémie 30.12-30.17 Jérémie 51.8 Luc 8.43

Cette Bible est dans le domaine public.