13 Bwana MUNGU asema hivi; Huu ndio mpaka ambao mtaigawanya nchi iwe urithi sawasawa na kabila kumi na mbili za Israeli; kwa Yusufu, mafungu mawili. Genèse 48.5 Ezéchiel 48.4-48.6 Nombres 34.2-34.12 Jérémie 3.18 1 Chroniques 5.1 14 Nanyi mtaimiliki, mtu huyu sawasawa na huyu; ambayo naliuinua mkono wangu kuwapa baba zenu; na nchi hii itawaangukia kuwa urithi. Genèse 12.7 Ezéchiel 20.5-20.6 Ezéchiel 48.29 Nombres 14.16 Genèse 13.15 15 Na huu ndio mpaka wa nchi; upande wa kaskazini, toka bahari kubwa, kwa njia ya Hethloni, mpaka maingilio ya Sedada; Nombres 34.8 Ezéchiel 48.1 16 Hamathi, na Berotha, na Sibraimu, ulio katikati ya mpaka wa Dameski na mpaka wa Hamathi; na Haser-hatikoni, ulio karibu na mpaka wa Haurani. 2 Samuel 8.8 Nombres 13.21 Ezéchiel 48.1 Zacharie 9.2 Genèse 14.15 17 Nao mpaka toka baharini utakuwa Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, na kaskazini kuelekea upande wa kaskazini ndio mpaka wa Hamathi. Huu ndio upande wa kaskazini. Ezéchiel 48.1 Nombres 34.9 18 Na upande wa mashariki, kati ya Haurani na Dameski, na Gileadi na nchi ya sraeli, utakuwa mto Yordani; mtapima toka mpaka wa upande wa kaskazini hata bahari ya mashariki. Huu ndio upande wa mashariki. Genèse 13.10 Genèse 31.23 Juges 10.8 Job 40.23 Genèse 31.47 19 Na upande wa kusini, kuelekea kusini, utakuwa ni kutoka Tamari mpaka maji ya Meriba-Kadeshi, mpaka kijito cha Misri, mpaka bahari kubwa. Huu ndio upande wa kusini, kuelekea kusini. Deutéronome 32.51 Ezéchiel 48.28 Nombres 34.5 Nombres 20.13 Deutéronome 33.8 20 Na upande wa magharibi, utakuwa ni bahari kubwa, kutoka mpaka wa kusini mpaka mahali penye kuelekea maingilio ya Hamathi. Huu ndio upande wa magharibi. Nombres 34.6 Ezéchiel 48.1 21 Basi ndivyo mtakavyojigawanyia nafsi zenu nchi hii, sawasawa na kabila za sraeli. 22 Tena itakuwa mtaigawanya kwa kura, kuwa urithi kwenu, na kwa wageni wakaao kwenu hali ya ugeni, watakaozaa watoto kati yenu, nao watakuwa kwenu, kama wazaliwa miongoni mwa wana Israeli; watakuwa na urithi pamoja nanyi kati ya kabila za Israeli. Colossiens 3.11 Ephésiens 3.6 Romains 10.12 Esaïe 56.6-56.7 Esaïe 14.1 23 Tena itakuwa, mgeni akaaye katika kabila iwayo yote, atapewa urithi katika kabila asema Bwana MUNGU.