Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Zacharie 8.12
Bible en Swahili de l’est


1 Neno la Bwana wa majeshi likanijia, kusema, 2 Bwana wa majeshi asema hivi, Mimi nina wivu kwa ajili ya Sayuni, wivu mkuu, nami nina wivu kwa ajili yake kwa ghadhabu kuu.Nahum 1.2 Esaïe 63.15 Zacharie 1.14-1.16 Esaïe 59.17 Ezéchiel 36.5-36.6
3 Bwana asema hivi, Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji wa kweli; na Mlima wa Bwana wa majeshi utaitwa, Mlima mtakatifu.Zacharie 1.16 Zacharie 2.10-2.11 Esaïe 1.26 Esaïe 65.25 Esaïe 11.9
4 Bwana wa majeshi asema hivi, Wazee wanaume na wazee wanawake watakaa tena katika njia za Yerusalemu, kila mtu ana mkongojo wake mkononi, kwa kuwa ni mzee sana.Lamentations 2.20-2.22 Job 5.26 Hébreux 12.22 Job 42.17 Lamentations 5.11-5.15
5 Na hizo njia za mji zitajaa wavulana, na wasichana, wakicheza katika njia zake.Jérémie 30.19-30.20 Jérémie 31.13 Jérémie 31.27 Psaumes 128.3-128.4 Lamentations 2.19
6 Bwana wa majeshi asema hivi, Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki ya watu hawa katika siku hizo, je! Liwe neno gumu mbele ya macho yangu? Asema Bwana wa majeshi.Jérémie 32.27 Jérémie 32.17 Genèse 18.14 Psaumes 118.23 Luc 1.20
7 Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaokoa watu wangu toka nchi ya mashariki, na toka nchi ya magharibi;Esaïe 27.12-27.13 Esaïe 49.12 Esaïe 66.19-66.20 Psaumes 107.2-107.3 Malachie 1.11
8 nami nitawaleta, nao watakaa katikati ya Yerusalemu; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, katika kweli na katika haki.Ezéchiel 36.28 Jérémie 4.2 Ezéchiel 11.20 Jérémie 31.33 Zacharie 13.9
9 Bwana wa majeshi asema hivi, Mikono yenu na iwe hodari, ninyi mnaosikia siku hizi maneno haya kwa vinywa vya manabii, waliokuwapo siku hiyo ulipowekwa msingi wa nyumba ya Bwana wa majeshi; yaani, hekalu hilo; ili lijengwe.Esaïe 35.4 Esdras 5.1-5.2 1 Chroniques 22.13 Ephésiens 6.10 2 Timothée 2.1
10 Maana kabla ya siku zile hapakuwa na ijara kwa mwanadamu, wala hapakuwa na ijara kwa mnyama; wala hapakuwa na amani kwake yeye aliyetoka, wala kwake yeye aliyeingia, kwa sababu ya adui; nami nalimwacha kila mtu kugombana na jirani yake.Amos 3.6 Aggée 2.16-2.18 Amos 9.4 Esaïe 19.2 Juges 5.6-5.7
11 Lakini sasa sitakuwa kwa mabaki ya watu hawa kama nilivyokuwa siku zile za kwanza, asema Bwana wa majeshi.Esaïe 12.1 Aggée 2.19 Psaumes 103.9 Zacharie 8.8-8.9 Esaïe 11.13
12 Kwa maana itakuwako mbegu ya amani; mzabibu utatoa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na hizo mbingu zitatoa umande wake; nami nitawarithisha mabaki ya watu hawa vitu hivi vyote.Deutéronome 33.13 Genèse 27.28 Lévitique 26.4-26.5 Osée 14.5 Ezéchiel 36.30
13 Kisha itakuwa, kama vile mlivyokuwa laana katika mataifa, Ee nyumba ya Yuda, na nyumba ya Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka; msiogope, lakini mikono yenu na iwe hodari.Zacharie 8.9 Psaumes 72.17 Ezéchiel 5.15 Esaïe 19.24-19.25 Jérémie 29.18
14 Maana Bwana wa majeshi asema hivi, Kama vile nilivyoazimia kuwatenda ninyi mabaya, baba zenu waliponikasirisha, asema Bwana wa majeshi, wala mimi sikujuta;Jérémie 31.28 Ezéchiel 24.14 Jérémie 4.28 2 Chroniques 36.16 Esaïe 14.24
15 vivyo hivyo nimeazimia katika siku hizi kuutendea Yerusalemu mema, na nyumba ya Yuda pia; msiogope.Zacharie 8.13 Michée 7.18-7.20 Sophonie 3.16-3.17 Luc 12.32 Jérémie 29.11-29.14
16 Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme kweli na jirani yake; hukumuni kweli na hukumu ya amani malangoni mwenu;Zacharie 7.9 Ephésiens 4.25 Psaumes 15.2 Proverbes 12.19 Esaïe 9.7
17 wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema Bwana.Proverbes 3.29 Zacharie 7.10 Proverbes 6.16-6.19 Habakuk 1.13 Malachie 3.5
18 Tena neno la Bwana wa majeshi likanijia, kusema, 19 Bwana wa majeshi asema hivi, Saumu ya mwezi wa nne, na saumu ya mwezi wa tano, na saumu ya mwezi wa saba, na saumu ya mwezi wa kumi, zitakuwa furaha na shangwe, na sikukuu za kuchangamkia, kwa nyumba ya Yuda; basi zipendeni kweli na amani.Zacharie 8.16 Zacharie 7.5 Jérémie 39.2 2 Rois 25.25 Psaumes 30.11
20 Bwana wa majeshi asema hivi, Itatokea halafu ya kwamba watakuja mataifa na wenyeji wa miji mingi;Zacharie 2.11 Jérémie 16.19 Zacharie 14.16-14.17 Michée 4.1-4.2 Matthieu 8.11
21 wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka tuombe fadhili za Bwana, na kumtafuta Bwana wa majeshi; Mimi nami nitakwenda.Zacharie 7.2 Psaumes 103.22 Psaumes 122.1-122.9 Osée 6.3 Psaumes 146.1-146.2
22 Naam, watu wa kabila nyingi na mataifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana wa majeshi, na kuomba fadhili za Bwana.Zacharie 8.21 Esaïe 25.7 Apocalypse 21.24 Apocalypse 15.4 Michée 4.3
23 Bwana wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.1 Corinthiens 14.25 Esaïe 45.14 Actes 13.47-13.48 Genèse 31.7 Esaïe 66.18

Cette Bible est dans le domaine public.